Okwi ananuka fedha Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi. KUANZIA leo Jumatano, zitakuwa zimebaki takribani siku 11 kabla ya usajili wa dirisha kubwa Tanzania Bara halijafungwa ambapo timu kadhaa zimekuwa zikiimarisha vikosi vyao. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa siku 52 kwa timu za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kujenga vikosi vyao kwa kufanya usajili kuanzia Juni 15 mpaka Agosti 6, mwaka huu. Tangu kufunguliwa kwa dirisha hilo, kumekuwa na vurugu kwa wachezaji kuhama timu moja kwenda nyingine huku tukishuhudia baadhi ya timu zikigombania mchezaji mmoja na kila upande ikihitaji saini yake. Katika vurugu hizo, kuna wachezaji wamesajili kwa madau makubwa na kuwafanya kuwa wachezaji ghali katika soka la Bongo kwa sasa. Championi ambalo tangu siku ya kwanza ya usajili limekuwa makini kufuatilia mchakato huo, linakuletea tathmini ya kile kilichofanyika mpaka sasa na kubainisha nani amesajili kwa mkwanja mrefu. EMMANUEL OKWI Mganda...