Neymar azima tambo za Manchester United
Baada ya tambo nyingi zilizoletwa na ushindi wa michezo yao yote ya kujiandaa na msimu wa ligi hatimaye usiku wa kuamkia leo ngebe za mashabiki wa Manchester United zilitulizwa.
Manchester United walikuwa uwanjani katika mchezo wao wa mwisho barani America waliocheza dhidi ya wababe wa kutoka Hispania klabu ya Barcelona.
Mchezo ambao ulijaza mashabiki wengi na huku watu wengi waliutazama kutokana na fomu ya sasa ya United na ubora ambao wakonao klabu ya Barcelona.
Alikuwa Neymar Dos Santos mchezaji anayezungumzwa sana kwa sasa na vyombo vya habari ndiye aliyeimaliza United katika dakika ya 31 ya mchezo.
United kupitia kwa Lukaku na Rashford walijitahidi sana kulishambulia sana lango la Barcelona lakini umahiri wa golikipa Jasper Cillessen ulizizima jitihada za United.
United sasa wanarudi barani Ulaya kwa michezo miwili ya kirafiki zidi ya Vilarenga nchini Norway na ule zidi Sampdoria kabla ya kukutana na Real Madrid katika fainali ya Super Cup.
Katika mchezo mwingine mkubwa wa kirafiki PSG walikubali kipigo cha mabao 3 kwa 2 toka kwa Juve huku Claudio Marchisso akiifungia Juve mara mbili,Higuain moja na yale ya PSG yakifungwa na Goncalo Guede na Javier Pastore.

- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps