Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

Wakulima watakiwa kuheshimu mkataba wa Kampuni za ununuzi

Wakulima watakiwa kuheshimu mkataba wa Kampuni za ununuzi Chama Kikuu cha Ushirika (Kacu), kimewatahadharisha wakulima wa tumbaku kuheshimu mkataba wa kampuni za ununuzi ili kusijitokeze kama yaliyowakuta msimu uliopita, baada ya zaidi ya kilo milioni tatu kukosa soko. Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Kacu, Emmanuel Peter baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa uchaguzi. Alisema mwaka huu wakulima wameingia mkataba na kampuni za ununuzi kuzalisha kilo milioni nane za tumbaku, hivyo wanapaswa kulima bila kuzidi. Mwaka jana, tumbaku iliyozidi kwa Kahama ilikuwa kilo milioni 3.25 ambayo ilikuwa ni ziada ya mkataba wa kuzalisha kilo milioni sita ambazo kampuni ziligoma kununua ziada hiyo. Hata hivyo, baada ya mazungumzo ya muda mrefu zilikubali kwa masharti ya kununua kwa bei ya dola 1.25 za Marekani (Sh2,700) kwa kilo kwa tumbaku ya daraja la kwanza badala ya Sh5,000 au Sh6,000 kwa bei iliyotumika awali. “Wakulima acheni kulima nje ya idadi iliyopo kwenye mkataba wa ka

CUF ya Lipumba Yawaomba radhi wapiga kura Kinondoni Baada ya Mbunge wake Maulid Mtulia Kujiuzulu

CUF ya Lipumba Yawaomba radhi wapiga kura Kinondoni Baada ya Mbunge wake Maulid Mtulia Kujiuzulu Chama cha Wananchi  (CUF), upande wa Profesa  Ibrahim  Lipumba kimewaomba radhi wapiga kura wa jimbo la Kinondoni  baada ya aliyekuwa mbunge  wa jimbo hilo kupitia chama hicho, Maulid Mtulia kujiuzulu. Kauli imetolewa  leo, Jumatatu  Desemba 4, 2017 na Mkurugenzi  wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Abdul  Kambaya wakati akizungumza  na wanahabari kwenye makao makuu ya chama hicho Buguruni. Amesema CUF iliwaaminisha wakazi wa Kinondoni  kwa kumpeleka Mtulia kugombea jimbo hilo kwa kuwa ni mtu makini na mambo mengi alishaanza kuyatekeleza ikiwamo kuzuia bomoa bomoa lakini wanasikitika kujiuzulu kwake. "CUF  haikutarajia kuingia katika uchaguzi mdogo hasa jimbo la Kinondoni  kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 labda kingetokea kifo. Tunawaomba radhi wakazi wa Kinondoni," amesema Kambaya. Kambaya amesema sababu za kujiuzulu  alizozitoa Mtu

CUF ya Maalim Seif Yachekelea Maulid Mtulia kujiuzulu Ubunge

CUF ya Maalim Seif Yachekelea Maulid Mtulia kujiuzulu Ubunge Uamuzi wa Maulid Mtulia kujivua ubunge na uanachama haujakishtua chama chake cha CUF, badala yake kimesema bado wengine wawili ambao kingependa waondoke haraka. Hilo lilisemwa jana na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye anaongoza upande mmojapo kati ya mbili zinazokinzana. Upande mwingine unaongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba. N aibu katibu mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwa, Mtulia ni mmoja wa wabunge watatu wanaomuunga mkono Profesa Lipumba. “Hatukutarajia kama Mtulia ataondoka wakati huu, bali tulijua ataendelea kudumu. Lakini kama ameondoka ni faraja kwetu kwa sababu katika mipango yetu tulishamuondoa,” alisema Mazrui. “Tunawaombea dua wale wawili waliobaki waondoke hata leo kwa sababu kuendelea kukaa kwao ndani ya CUF ni kukidhoofisha chama hiki.” Mazrui aliwataka wabunge kutoshangaa endapo wenzao hao watatangaza kujiuzulu nafasi zao akidai k

Rais Magufuli kuzindua ya kampeni Uzalendo na Utaifa

Rais Magufuli kuzindua ya kampeni Uzalendo na Utaifa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ itazinduliwa Ijumaa hii Disemba 8 2017 kupitia ‘Usiku Wa Kitendawili’ mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ndio wataouratibu usiku huo wa Kitendawili. Usiku wa Kitendawili ulianzishwa baada ya msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kuachia wimbo ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo. Akiongea na wadau wa sanaa katika Maandalizi ya Kampeni hiyo ya Kitaifa itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, Mrisho Mpoto amesema kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hal

Ndoa yampapresha Shilole

Ndoa yampapresha Shilole WAKATI akisubiri kufunga ndoa na mchumba wake, Uchebe Ashraf siku chache zijazo, staa wa muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ yu gonjwagonjwa, Ijumaa Wikienda limedokezwa. Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao kilieleza kuwa, ndoa hiyo inampa presha Shilole kwani alizidiwa hivi karibuni na kwenda kulazwa hospitali licha ya kwamba kwa sasa anaendelea vizuri tofauti na awali. “Unajua Shilole anatarajia kufunga ndoa na Uchebe hivi karibuni, kwa hiyo ana presha ya ndoa na ukizingatia na watu walivyozusha kuwa amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda ndiyo wakamchanganya kabisa,” kilidai chanzo hicho. Ili kuujua ukweli wa habari hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shilole baada ya kuona picha alizosambaza mchumba wake Uchebe zikimuonesha mwanamama huyo akiwa amelazwa hospitalini ambapo alikiri kuzidiwa lakini akasema presha ya ndoa bali ni malaria. “Jamani nililazwa hospitali kwa Dokta Mvungi kwa sababu nina malaria kali. Nilik

TBA yakiri mabweni ya UDSM kuwa na nyufa

TBA yakiri mabweni ya UDSM kuwa na nyufa Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa. Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za 'expansion joint' ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake. "Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu", amesema Bwana Mwakalinga. Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila

Mawaziri, wakuu wa Wilaya wa awamu zilizopita kidedea ndani ya Uchaguzi CCM

Mawaziri, wakuu wa Wilaya wa awamu zilizopita kidedea ndani ya Uchaguzi CCM Wanachama waliokuwa mawaziri na wakuu wa wilaya katika uongozi wa Serikali za awamu zilizopita, wameibuka kidedea kwenye uchaguzi ndani ya CCM unaoendelea kote nchini. Mawaziri wawili wa zamani, Kate Kamba na Anthony Diallo wameibuka kuwa wenyeviti wa mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza. Kamba aliwahi kuwa naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto na naibu waziri wa Viwanda na Biashara kati ya mwaka 1994 na 1995. Pia, aliwahi kuwa mbunge wa Afrika Mashariki. Kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2000 na 2008, Diallo aliwahi kuwa naibu waziri wa Maji na Mifugo, naibu waziri wa Viwanda na Biashara; waziri wa Maendeleo ya Mifugo na waziri wa Maliasili na Utalii. Juzi, msimamizi wa uchaguzi wa CCM mkoani Dar es Salaam, William Lukuvi alimtangaza Kamba kuwa mshindi baada ya kupata kura 443. Wapinzani wake, Brigedia Jenerali mstaafu Ryakitimbo Magige alipata kura 22 na Malima Bunara kura 12. Kamb

Mpango wa kutengeneza fedha mpya watangazwa

Mpango wa kutengeneza fedha mpya watangazwa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangaza mpango wa kutengeneza fedha mpya ya nchi hiyo katika kujaribu kuunusuru uchumi wa nchi hiyo. Amesema fedha hiyo iitwayo Petro itaimarishwa na utajiri wa Venezuela utokanao na mafuta, gesi, pamoja na dhahabu. Uchumi wa Venezuela umedorora mno kutokana na kushuka kwa mapato ya mafuta pamoja na kuporomoka kwa thamani ya fedha yake ya sasa ya bolivar.

Bunduki ya Nassari yachunguzwa

Bunduki ya Nassari yachunguzwa Wakati mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari akilihusisha tukio la kuvamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na masuala ya kisiasa, polisi inashikilia bunduki ya mwanasiasa huyo kwa uchunguzi. Polisi mkoani Arusha imesema imeanza uchunguzi wa kina wa kuwasaka washukiwa, huku ikichunguza silaha ya Nassari aina ya shotgun, ikisema tukio hilo lina utata kutokana na mazingira lilivyotokea. Kamanda wa polisi wa mkoa, Charles Mkumbo aliliambia gazeti hili kuwa wameanza uchunguzi wa kina ili kubaini endapo kulikuwa na tukio au la. “Tunaifanyia uchunguzi bunduki yake, tunataka kujiridhisha endapo kulikuwa na tukio au la,” alisema Mkumbo. Hata hivyo, kamanda huyo alisema msako unaendelea ili kuwabaini washukiwa na kwamba hawajapata maganda ya risasi zinazodaiwa kutumika katika uvamizi huo. Juzi Nassari aliwaambia waandishi wa habari kuwa nusu saa baada ya kuwasili nyumbani kwake alisikia hali isiyo ya kawaida ndani ya uzio wa nyu

Aliyekuwa Waziri Mkuu Misri hajulikani alipo

Aliyekuwa Waziri Mkuu Misri hajulikani alipo  Familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Misri, Ahmed Shafiq imesema haina taarifa wapi aliko ndugu yao baada ya kutangaza ana azma ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwakani. Shafiq ambaye ni kamanda wa zamani wa jeshi la anga la Misri na waziri mkuu katika utawala wa Hosni Mubarak, anaonekana kuwa mgombea mwenye nguvu ya kuchuana na Rais Abdel Fattah al Sisi ambaye anatarajiwa kugombea muhula wa pili katika uchaguzi huo. Familia ya Shafiq aliyerejea mjini Cairo jana kwa kutumia ndege binafsi imesema haijui lolote kuhusu hatima yake. Wakili wake pia amesema hajawasiliana naye, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ikisema haihusiki na suala la Shafiq. Ripoti zinasema Shafiq aliwasili Misri jana jioni na alionekana mjini Cairo. Maofisa wa Falme za Kiarabu wamethibitisha kuwa Shafiq aliondoka nchini humo.

Kujiengua kwa Mtulia haujakishtua chama cha CUF

Kujiengua kwa Mtulia haujakishtua chama cha CUF Uamuzi wa Maulid Mtulia kujivua ubunge na uanachama haujakishtua chama chake cha CUF, badala yake kimesema bado wengine wawili ambao kingependa waondoke haraka. Hilo lilisemwa jana na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye anaongoza upande mmojapo kati ya mbili zinazokinzana. Upande mwingine unaongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba. Lakini upande wa Profesa Lipumba umesema unatafakari uamuzi huo wa Mtulia ambaye anakuwa mbunge wa pili kujivua uanachama. Wakati sakata hilo la kuhamahama vyama likipamba moto, aliyekuwa naibu waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana wa Serikali ya Awamu ya Nne, Makongoro Mahanga amesema amekuwa akifuatwa na watu tofauti ambao “pengine hawafahamiani” wakimshawishi arudi CCM, lakini amesema kamwe hataondoka Chadema. Hamahama ya wanasiasa imesababisha baadhi ya kata kufanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi zilizoachwa wazi na madiwani waliohamia CCM, huku jimbo moja liki

Madaktari watangaza kimakosa kuwa mtoto amefariki

Madaktari watangaza kimakosa kuwa mtoto amefariki Mtoto ambaye alikuwa ametangazwa kuwa amefariki na madaktari mara baada ya kuzaliwa kwenye hospitali moja huko Delhi India, alipatikana akiwa hai wakati akipelekwa kufanyiwa mazishi. Madaktari kwenye hospitali ya kibinafsi ya Max walikuwa wamemtangaza mtoto kuwa amefariki saa chache baada ya pacha mwenzake kutangazwa kufariki baada ya kuzaliwa. Wazazi wake walisema kuwa walifahamu kuwa mtoto huyo alikuwa hai ndani ya mfuko ambao madaktari walikuwa wamemweka. Kisa hicho kimezua hasira na mjadala kuhusu hali ya viwango katika hospitali za kibinafsi ambazo mara nyingi ni ghali mno. Mkuu wa jimbo la Delhi aliandika katika Twitter kuwa ameamrisha kisa hicho kufanyiwa uchunguzi. Kulingana na babu yake mtoto, familia hiyo iliyokuwa imepigwa na mshangao ilimkimbiza mtoto kwenda hospitali iliyokuwa karibu ambapo waliambiwaa kuwa mtoto huyo alikuwa hai. Katika taarifa kwa waandishi wa hababi , hospitalia ya Max ilishangazwa na kisa

Mbunge amchumbia mwanaume mwenzie Bungeni

Mbunge amchumbia mwanaume mwenzie Bungeni Tim Wilson Mbunge mwanamume nchini Australia ameposa kwa mpenzi wake wa kiume wakati wa kikao cha bunge cha kujadili kuhalalishwa ndoa za jinsia moja. Tim Wilson alimchumbia Ryan Bolger ambaye alikuwa ameketi eneo la umma. Wawili hao wamekuwa wapenzi kwa miaka 9. Mswada huo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja uliwasilishwa bungeni siku ya Jumatatu baada ya kupitia bunge la Senate wiki iliyopita. "Katika hotuba yangu ya kwanza, ninatambua uhusiano wetu kwa pete iliyo kwenye mikono yetu yote ya kushoto. Pete hii ni jibu kwa maswalii ambayo hatutawezi kuyauliza," Bw Wilson alisema. "Kwa hivyo kuna kitu kimoja tu ambacho kimebaki kufanywa. Ryan Patrick Bolger utakubalia nikuoe ?" Swali hilo lilizua shangwe na pongezi, kaala ya Bw Bolger kujibu kwa sauti na kusema "ndiyo" Mapema Bw. Wilsni alizungumzia maisha yake ya kukua kama kijana mpenzi wa jinsia moja na kukumbana na unyan

Wafanyabiashara waishauri Halmashauri kuboresha huduma ya Kodi

Wafanyabiashara waishauri Halmashauri kuboresha huduma ya Kodi Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mbeya, kimeshauri Jiji la Mbeya kuangalia namna bora ya kuboresha na kukusanya tozo za kodi ya huduma kutoka kwa wafanyabiashara ili kuboresha kiwango cha huduma. Mratibu wa TCCIA Mkoa wa Mbeya, Emily Malinza alibainisha hilo juzi jioni kwenye mkutano uliowakutanisha uongozi wa jiji la Mbeya, wadau wa masuala ya kodi na wafanyabiashara kwenye majadiliano ya pamoja kuhusu programu ya kukuza uwekezaji na biashara kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kwa jiji hilo. Malinza alisema wafanyabiashara wamekuwa wakifika TCCIA kuuliza tozo za kodi wanazotozwa na jiji namna zinavyowanufaisha, kwa kukuwa wanatozwa tu lakini hawaoni huduma. Wafanyabiashara wengi wanauliza tozo wanazolipa zinakokwenda, wakati hakuna huduma wanayoipata kutoka jiji kwa mujibu wa sheria inayoelekeza. “Sasa jibu ni rahisi tu kwamba kodi inayochukuliwa ni chache kiasi hat

Jinsi ghorofa 10 jengo la Tanesco zitakavyobomolewa

Jinsi ghorofa 10 jengo la Tanesco zitakavyobomolewa Wakati ukumbi wa mikutano na ofisi za mapokezi za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vikivunjwa Wakala wa Majengo (TBA) umeeleza namna jengo la ghorofa 10 litakavyobomolewa. Meneja wa Kikosi cha Ujenzi wa TBA, Humphrey Killo alisema jana kuwa uvunjaji wa ofisi na ukumbi ulifanyika usiku wa kuamkia juzi ikiwa ni maandalizi ya kuvunja sehemu ya jengo la ghorofa 10 lililoko eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam ambalo liko kwenye hifadhi ya Barabara ya Morogoro. Ubomoaji huo unafanyika pia ili kupisha utekelezaji wa mradi wa barabara za juu eneo la Ubungo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli. Novemba 15, Rais Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka alama za X kwenye jengo hilo katika sehemu zilizo katika hifadhi za barabara. Akizungumzia uvunjaji wa jengo hilo, Killo alisema kwa sasa wanafanya maandalizi yakiwemo ya vifaa kama vile mitambo na malori ya kubebea vifusi. “Maandalizi haya

Makamu wa Rais ameitaka Jamii kuwapa kipaumbele walemavu kwenye maendeleo

Makamu wa Rais ameitaka Jamii kuwapa kipaumbele walemavu kwenye maendeleo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameitaka jamii kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawaachwi nyuma kwenye nyanja zote za maendeleo. Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Watu wenye ulemavu duniani iliyofanyika mkoa wa Kusini, Unguja, Zanzibar. Akihutubia mamia ya watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu kwenye kwenye viwanja vya Skuli ya Uzini, Makamu wa Rais alisema tumejumuika leo hapa kuungana na wenzetu duniani kote kuadhimisha kilele cha siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo imebeba kauli mbiu isemayo “Mabadiliko kuelekea jamii Jumuishi na Maendeleo Endelevu kwa wote”­­­­­­ ujumbe huu unalenga kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanajumuishwa katika mipango yote ya maendeleo ili kuweza kufikia malengo endelevu ya dunia ifikapo mwaka 2030 pia inakwenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2020; Ilani ya Chama

Yanga kurejea mazoezini leo

Yanga kurejea mazoezini leo Kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, kinatarajia kurejea mazoezini leo Jumatatu baada ya mapumziko ya zaidi ya siku tatu. Uongozi wa Yanga uliamua kuwapumzisha wachezaji wake kwa muda wakati michuano ya Chalenji inaanza huko Kenya. Awali ilielezwa kuwa mazoezi yangeanza Ijumaa, lakini baadaye ilibadilishwa na mazoezi kupelekwa hadi leo. Baadhi ya wachezaji wako katika kikosi cha Tanzania Bara maarufu kama Kili Stars kinachoshiriki Chalenji. Wengine pia wako katika kikosi cha Zanzibar Heroes pia kianshiriki michuano hiyo ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Bi. Hindu ajisalimisha kwa MO

Bi. Hindu ajisalimisha kwa MO Kama unakumbuka, shabiki na mwanachama mkongwe wa Simba Chuma Suleiman maarufu kama Bi. Hindu alikuwa hataki kusikia kabisa habari za mambo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndani ya klabu yao hususan masuala ya hisa na kampuni. Leo December 3, 2017 MO ameshinda kwa kishindo zabuni ya kuwekeza ndani ya Simba, baada ya MO kutangazwa mshindi na wanachama wengi waliohudhuria mkutano huo kuridhia, Bi Hindu alijitokeza na kwenda hadi MO kumpongeza. ShaffiDauda.co.tz ikapiga story na bibi huyo kutaka kujua msimamo wake upo kwa sasa baada ya kuwa miongoni mwa wanachama waliokuwa wakipinga mchakato huo. “ Tuliambiwa wanachama tutafukuzwa tutakuwa hatukanyagi klabuni, ndio kitu kilichokuwa kinaniuma rohoni kwa sababu klabu hii imejengwa na wauza vitumbua, wapasua kuni, lakini baada ya kueleweshwa nimeelewa na nipo safi. Atakaenifata  kuniuliza nitamweleza akielewa ataungana na sisi kama hataki basi namuacha.” Bi. Hindu amesema wapo watu watakaosem

Marekani yatakiwa isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Marekani yatakiwa isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel Ayman Safadi alisema alimuambia waziri wa mashauri wa nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuwa hatua kama hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiisalmu. Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni. Jared Kushner, mkwe wa Trump alisema kuwa bado hakuna uamuzi uliofanywa. Ubalozi wa Marekani kuhamia Jerusalem? Palestina: Uhamisho wa ubalozi utaathiri amani Katika mtandao wa Twitter, Bw Safadi alisema: #Nilizungumza na waziri Rex Tillerson kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Hatua kama hiyo inaweza kusababisha ghadhabu kwenye nchi za kiarabu na kwa ulimwengi wa kiislamu na kuzua misukosuko na pia kuhujumu jitihada za amani." Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi ya

Polepole amesema Chama chake hakitampokea Mtu adi afuate taratibu

Polepole amesema Chama chake hakitampokea Mtu adi afuate taratibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitampokea yeyote anayetaka kurudi ndani ya chama hicho bila kufuata utaratibu. Kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni(CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi alizokuwa akizishikilia kwenda CCM Polepole aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama. “Ameamua kule aliko haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina baba wawili huwezi kuwa na nyumba ina baba wawili alafu utasikiliza watoto watamsikiliza nani, basi amehama,” alisema Polepole. “Sasa mimi niko hapa Musoma mimi nitumie fursa hii anayemuunga mkono ni Rais wetu ambaye ni mwana CCM kwelikweli na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ikimpendeza afuate utaratibu akiona mazuri ya Rais yule asione

TBS latolea ufafanuzi taarifa zilizosambazwa mtandaoni kulihusu

TBS latolea ufafanuzi taarifa zilizosambazwa mtandaoni kulihusu