Skip to main content

Rais Magufuli kuzindua ya kampeni Uzalendo na Utaifa

Rais Magufuli kuzindua ya kampeni Uzalendo na Utaifa


Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ itazinduliwa Ijumaa hii Disemba 8 2017 kupitia ‘Usiku Wa Kitendawili’ mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi cha Sanaa cha Mpoto Theatre Gallery na wadau wa sanaa za Ubunifu ndio wataouratibu usiku huo wa Kitendawili.

Usiku wa Kitendawili ulianzishwa baada ya msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto kuachia wimbo ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo.

Akiongea na wadau wa sanaa katika Maandalizi ya Kampeni hiyo ya Kitaifa itayokuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere, Mrisho Mpoto amesema kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza ndani ya Taifa letu.

Alisema mambo ambayo yatayozingatiwa katika kampeni hiyo ni pamoja na kudhubiti na hatimaye kukomesha kabisa mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa Umma, kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka ufisadi, ubadhilifu wa mali za Umma pamoja kuongeza hari ya kufanya kazi na Uzalendo.

“Usiku wa Kitendawili utatumika kama jukwaa la kuwaleta pamoja watanzania pamoja na viongozi wao ili kukumbushana kuhusu wajibu na kujadili mustakabali wa Taifa. Kutakuwa na vivutio mbalimbali pamoja na wimbo maalumu kutoka kwa wasanii maalumu Mwaka Huu,” alisema Mpoto.

Aliongeza,”Tumekuja kuunadi Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ kwasababu tunaamini Uzalendo na Utaifa lazima uwepo ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili kuunga mkono juhudi za Raisi Dkt.

John Pombe Magufuli za kujenga Taifa lenye Uzalendo, Utu, Weledi na Uadilifu uliotukuka. Mimi ni mzalendo ndio maana hata kwenye hizi harakati nipo toka nimetoa wimbo wangu wa kwanza, ukiangalia nyimbo zangu zote ni za kuonganisha jamiii 120 za watanzani,”

 “Naamini kwenye kufanya kazi ambayo itawafanya watanzania pamoja na kizazi kijacho kitambue kuna watu ambao walifanya kazi kubwa kwenye hili taifa, kuacha alama ambazo haziwezi kufutika katika maisha ya historia ya nchi hii, kwa sababu hivi vyote ambavyo vinaenda kufanywa ni kufufua upya na kuiweka pamoja mitazamo ya watanzania ili kujenga Taifa la Wazalendo na Wachapakazi kuiga nyayo zilizoachwa na hayati Baba wa Taifa,” alifafanua zaidi.

Mpoto amesema lengo kuu la maadhimisho hayo kuambatana na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa kuanzia mwaka 2018 ni kutumia jukwaa hilo kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kujenga na kuendeleza Utaifa.

Alisema baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo wiki hii huko Dodoma, itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni chini ya Uwenyekiti wa Mkuu wa Mkoa na  Wilaya.

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti WAKATI bei ya unga wa sembe ikipanda mpaka kufikia kuuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500 kwa kilo, ile ya mfuko wa saruji wenye uzito wa kilo 50 imeshuka hadi sh. 9,000, sawa na Sh. 180 kwa kilo. Katika masoko na maduka mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambayo Nipashe ilitembelea jana, bei ya sembe ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi hicho kwa rejareja huku wauzaji wa jumla wakiuza kiroba cha kilo 50 kwa kati ya sh.100,000 na sh.98,000. Ibrahim Omary, mfanyabiashara wa Kariakoo alisema anauza unga wa sembe kwa Sh. 2,400 kwa kuwa hununua kwa bei kubwa kutoka kwa wazalishaji. Alisema kampuni inayojulikana kwa jina la Mkulima huwauzia unga huo kwa Sh. 98,000 na Mama Neema huwauzia kwa sh. 100,000 kwa kiroba cha kilo 50. Kwenye baadhi ya maduka ya kula ya Kinondoni, unga umekuwa ukiuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500. Tandika bei ya wastani ni Sh. 2,200, Mwenge Sh. 2,400, Kimara sh. 2,500 na Yombo Vituka sh. 2,200. ...

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla...