Skip to main content

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.

 Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU” kama  ifuatavyo :

SEHEMU  YA  PILI   YA  KITABU  “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU “

Wachawi   wakishindwa  kukutengenezea  kesi  kubwa  basi  waatakufunga  kwenye  kifungo  cha  mapenzi.

 Katika  vifungo  vyote anavyo  fungwa  mwanadamu  hakuna  kifungo  kibaya  kama  kifungo  cha  mapenzi.  Usiombee  ufungwe  kwenye  kifungo  cha  mapenzi.

 Ni kifungo hatari  sana na  chenye  madhara  makubwa  sana.  Watu  wengi  wamekufa , wamejiua, wamefiliska  na  kuua  kwa  sababu  ya  kufungwa  kwenye  vifungo  vya  mapenzi.

 Kifungo  cha  mapenzi  ni  pale  mtu  anapo fungwa  kumpenda  mtu  fulani  katika  maisha  yake  yote.

 Ukifungwa  kifungo  hiki  ndugu  yangu  jua  umekwisha.  Ndoa  nyingi  zimeharibika na  watoto kukosa  mwelekeo  kwa  sababu  ya  vifungo  vya  mapenzi.

 Kwa ufupi  mtu  anae  kufunga  kifungo  cha  mapenzi ni mtu mbaya  sana  kwako.

 Kifungo  hiki  ni  kibaya  kwa  sababu  anae  kufunga  na  yeye anakuwa  ana  faidika  kutokana  na  kifungo  chako.

 Hapa  kwa  mfano  mwanamke   A  anakuwa  amemfunga  mwanaume  B  ampende yeye  tu  katika  siku  zote  za  maisha yake  yote.

 Anamfunga  macho, masikio, akili, ufahamu, maarifa  na  kila kitu.

 Mwanaume  anafungwa  amsikilize yeye  tu. Asisikilize  wazazi wake, ndugu zake, rafiki  zake, viongozi  wake wa  dini, mke  wake, watoto  wake, bosi  wake  au  mtu  yoyote  Yule na  badala  yake  asikie, afuate na  kutii  neno  na  maamuzi  ya  mfungaji.

 Gereza  hili  lina  wafungwa wengi  sana  ila  kati yao wanaume  ndio  wengi  zaidi  kuliko  wanawake.

 Zipo njia  nyingi   sana  ambazo  wanawake   huzitumia  kuwafunga  wanaume  kimapenzi.

 Katika  kitabu  hiki  nitaelezea  njia  moja  wapo  kati  ya  hizo, kwa  sababu  maelezo  yake  ni  machache  ikilinganishwa  na  njia  zingine.

 Zoezi  la kumfunga  mtu  kimapenzi  huwa  linaanza  kwa  kupima  kwanza  mwili  wa  mwanamke  ambae  anataka  kumfunga  mwanaume  kichawi.

Hii ni  kwa  sababu  uchawi   hususani wa  masuala  ya  mvuto  huwa  hauwezi  kufanya  kazi  kwa  mtu  mwenye  mwili  mchafu.

Ninaposema  mwili  mchafu  sizungumzii  uchafu  wa  nje  nazungumzia  uchafu  wa  ndani.  Mtu  anakuwa  ametupiwa  majini  wachafu  kwa  lengo  la  kumtia  nuksi, mikosi  na  mabalaa.

 Sasa basi  mtu  mwenye  mwili  uchafu  hawezi  kufanya  ulozi  wa  mapenzi  na  ukakubali.  Ili  ukubali  inabidi  asafishwe  kwanza  mwili  wake.

 Wakati  mwingine  mwili  wa  mtu  unaweza  kuwa  na  nuksi  ambazo  amezipata  yeye  mwenyewe   ila  kurogwa  na  mtu  yoyote.

 Naomba  ieleweke  kwa  watu kwamba,  zipo nuksi, mikosi  na  mabalaa  ambayo  mtu  anaweza  kuyapata  yeye  mwenyewe  bila  kurogwa  na  mtu  yoyote.

 Yapo  mambo mengi  yanayo  weza  kumsababishia  mtu  kupata nuksi, mikosi  na  mabalaa  bila  kurogwa  na  mchawi  au  mtu  yoyote  mbaya.

 Nuksi, balaa  na  mikosi  ya  aina  hii  hutokea  pindi  mtu  anakutana  au  kuingiwa  na  majini  wachafu  ambao  huweza  kumuingia  mtu  huyu  kwa  sababu  mbalimbali.

Zipo  sababu  nyingi  sana  zinazo  weza  kufanya  majini  wachafu  wakamuingia  na  kumvaa  mtu. Katika  kitabu  hiki  nitazitaja  chache  kama  ifuatavyo :

Kupata  nuksi  na  mikosi  sio tu lazima  uwe  umetupiwa  na  wabaya  wako. Wakati  mwingine  unaweza  kufanya  mambo  kadha  wa  kadhaa  eidha  kwa  kujua  au  kutokujua, yakakusababishia  kupatwa  na mikosi, nuksi  na  mabalaa  katika  maisha  yako. Baadhi  ya  mambo  yanayo  weza  kukuletea  nuksi, mikosi  na  mabalaa  katika  maisha  ni  pamoja  na  yafuatayo ; Umetoka  kufanya  mapenzi  bila  kuoga  janaba  halafu  wakati  unaelekea  nyumbani  au  mahali  popote  ukakumbwa  na  “ upepo mbaya”. Huyu  ni  jinni  hatari  sana  wa  njia  panda . Huwakumba  sana  sana  wazinzi  pamoja  na  watu  wanao  fanya  zinaa  halafu  baada  ya  kufanya  zinaa  wakashindwa  kuoga  janaba  au  kuoga  kwa  kutumia  dawa  maalumu.    Uzinzi ;tabia  ya  kufanya  mapenzi  ovyo , hii  inawahusu  sana  wanaume.  

Akienda  bar  akilewa  anaondoka  na  mwanamke, kesho  yake  anafanya  hivyo  hivyo  tena, kulala  na  wanawake  wanao  fanya  biashara  ya  kuuza  miili  yao.   Jambo  hili  ni hatari  sana, watu wengi  wamevuna  mikosi  na  mabalaa  makubwa  kwa  sababu  ya  uzinzi.  Hii  ni  kwa  sababu  tendo  la  ndoa  ni  agano  la  damu. Unapo fanya  mapenzi  na  mwanamke, mnamkuwa  mmefanya  agano  la  kuunganisha  damu  zetu. Na  damu  ndio  uhai  wa  mtu  na  ndio  hubeba, tabia  mustakabali  wa  kila  mwanadamu. Unapo  unganisha damu  na  mtu kwa  njia  ya  mapenzi , maana  yake  ni kwamba  unakuwa  umeunganisha  maisha  yake  na  yako, nyota  yake  na  yako. Sasa  unapokuwa  umekutana  na  mwanamke   mwenye  nuksi, mikosi  na  mabalaa  na  kufanya  nae  mapenzi , maana  yake  ni kwamba  unakuwa  umejifungamanisha  na  mikosi  na  mabalaa  yake.   Unakuwa  kitu kimoja  na  yeye,. Na  unapo  fanya  tendo  hilo  na  wanawake  wengi  zaidi  wenye  mabalaa  na  mikosi  unakuwa  umechukua  mikosi  ya  kila  aina . 

 Kibaya  zaidi  ni  kwamba, hao  wanawake  ambao  unakuwa  unakutana  nao  kimwili  ni  wanawake  Malaya  ambao  hulala  na  kila  mwanaume  na  hivyo  kuchukua  mikosi  ya  kila  mwanaume. Mikosi  na  mabalaa  hayo  huamia  kwako.

Kuwa  makini  sana  na  tabia  ya  kulala  na  kila  mwanamke  hususani  wanawake  wanao  huza  miili  yao. Ni  jambo  baya  sana na  ndio  maana kwenye  maandiko  matakatifu, imeandikwa  “ mwanaume  mzinzi  hana  akili  hata  kidogo, anaiangamiza  nafsi yake  mwenyewe “.  Tafuta  mwanamke  wako  mmoja, mchunguze  vizuri, ukijiridhisha  na  mwenendo  wake,  basi  fanya  nae  agano  la  milele. Wapo watu wengi  sana  wamefanikiwa  kwa  sababu  ya  aina  ya  wanawake  ambao  wame kuwa nao.  Hili  ni  somo  pana  sana  ambalo  linahitaji muda  na  nafasi  ya  kutosha  kulielezea. Ni somo  ambalo kila  mwanaume  na  kila  mwanamke  anapaswa  kulielewa  kwa mapana   na  marefu  yake.

Mambo  mengine  ni  pamoja  na  kukiuka  miiko  inayo  husiana  na  masuala  ya  wafu.   Kukiuka miiko  inayo  husiana  na  masuala  ya  wafu  ni  eneo  ambalo  limesababisha  mabalaa  na  mikosi  kwa  mamilioni  ya  watu  duniani. Katika  kitabu  hiki  nitaelezea   baadhi  ya mambo  yanayo  kiukwa  kuhusu  wafu  na  hivyo  kusababisha  mikosi  kwa  wahusika. Mikosi  na  mabalaa  haya  huwapata  wahusika   na  wahusika  hushindwa  kujua  chanzo cha  tatizo.

Mambo  hayo  ni  pamoja  na  kulaza  kaburi  wazi.  Ni mwiko  kuacha  kaburi  lilale  wazi. Kaburi  huwa  halilali  wazi hata  siku  moja.   Hakikisheni  siku  mtakayo  chimba  kaburi , iwe  ndio  siku  ambayo  mtazika marehemu  wenu.  Mkikiuka   mwiko  huu  basi  mikosi  itawaandama  sana  katika  familia  yenu. Vifo  vya  mara  kwa  mara  tena  vya  ajabu, magonjwa, umasikini na  mabalaa  mbalimbali  yatawaandama  katika  siku  zote  za  maisha  yenu  mpaka  mtakapo  fanya  tambiko  maalumu  la  kuvunja  hiyo  ngulikizi.

Msiache  kaburi  wazi  wakati  mnaenda  kuchukua  mwili  wa  marehemu  kwa  ajili  ya  kuupumzisha. Hakikisheni  wakati  watu  wanaenda  kuchukua  mwili  wa  marehemu  basi  kuwe  na  watu  kadhaa  ambao  watabaki kaburini  kulinda  kaburi  kuhakikisha  hakuna  mtu  yoyote  anakuja  kuchezea  kaburi  hilo.

Mwanamke  mjamzito  asihudhurie  mazishi; Mwanamke mjamzito hatakiwi kuhudhuria kwenye maziko ( makaburini ).Endapo atafanya hivyo basi, roho ya marehemu itamuingia mtoto aliyeko tumboni, na hivyo kusababisha bahati mbaya na mikosi kwa mwanamke huyo wakati wa kujifungua na endapo atajifungua salama, basi mtoto atakae zaliwa anaweza kupoteza uhai, au endapo ataishi basi, mama  huyo  atafariki  na  kumuacha  motto na  mtoto  atakuwa kwa taabu sana na ataandamwa na balaa   mikosi katika  maisha  yake  yote.

Kama itatokea mwanamke huyo akalazimika kuhudhuria kwenye mazishi ( Mfano labda aliyefariki ni mtu wake wa karibu sana kama vile mama yake,baba yake, mume wake, kaka yake, dada yake au mtoto wake ), basi anatakiwa ASITAZAME MWILI WA MAREHEMU wakati wa kuaga.

Endapo atafanya hivyo, basi ile roho ya marehemu itaishaishawishi roho ya mtoto aliyepo tumboni, kwenda kwenye nchi ya wafu, jambo ambalo litasababisha matatizo makubwa sana kwa mama wa mtoto wakati wa kujifungua. Uwezekano wa kujifungua mtoto aliyefariki, utakuwa kwa asilimia mia.

Usizungumze  habari  za  wafu  nyakati  za  usiku. Kuna  watu  huwa  wana  tabia  ya  kuzungumza  kuhusu  habari  za  ndugu, jamaa  na  marafiki  walio  tangulia  mbele  za  haki. Kama  utalazimika  kuzungumza  kuhusu  habari  hizo, nakushauri  usifanye  hivyo  wakati  wa  usiku. Ukizungumza  habari  za  wafu  nyakati  za  usiku, utasababisha  nuksi, balaa  na  mikosi  katika  maisha  yako. Kwani kwa  kufanya  hivyo  utakuwa  unaziamsha  na  kuzivuta  roho  za  wafu  zilizopo  makaburini  katika  maisha  yako  na  hivyo  kukusababishia  nuksi, balaa  na  mikosi. Moja  kati  ya  mabalaa  hayo  ni pamoja  na  kupatwa  na  misiba ya mara kwa  mara. Chunga  sana  hili.,

  Unapopita kwenye eneo la makaburi mida ya saa saba mchana au saa moja usiku, usiache mdomo wako wazi wala kupiga miayo. Endapo utafanya hivyo, roho za wafu zitakuingia na kusababishia matatizo makubwa.

Mnapomzika marehemu, kichwa kiangalie upande wa magharibi na miguu iwe upande wa mashariki.

Mara tu kifo kinapotokea, kitu cha kwanza, unacho takiwa ni kuondoa ama kufunika picha na vioo vyote vilivyomo kwenye chumba alichopo marehemu. Ni nuksi kubwa sana kuacha taswira ya mwili wa marehemu ionekane kwenye kioo. Kama hiyo haitoshi, ni nuksi kubwa sana kutazama taswira yako kwenye kioo hicho, mpaka mwili wa marehemu uatakapo kuwa umeondolewa. Ukitaka kuamini ninacho kisema, jaribu kuingia na kioo kwenye chumba alimo lala marehemu halafu jitazame kwenye hicho kioo. Utakacho kiona, uje ukisimulie hapa.

Naweni mikono kwa dawa maalumu baada ya kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu.

Oga dawa mara baada ya kutoka kaburini.

Kama marehemu amefariki akiwa nyumbani, mnapoenda kuutoa mwili wake, miguu itangulie kutoka, kamwe msifanye kosa mkatanguliza kichwa.

Kitanda anacho lalia mgonjwa mahututi, kitazame mashariki na magharibi, na kamwe sio kaskazini na kusini. Kichwa kiangalie magharibi na miguu itazame mashariki.

Jina la mwisho kutajwa na marehemu wakati anakaribia kukata roho, litakuwa jina la mtu atakae fuatia kufa baada ya marehemu.Hili  kujiepusha  na  balaa  hili, basi  unatakiwa  kufanyiwa  tambiko  maalumu.

Endapo mtu anae karibia kukata roho, atakun’gata, basi na wewe utamfuata baada ya muda mfupi. Ili kujiepusha na kifo cha namna hiyo, basi unatakiwa na wewe umng’ate katika sehemu ile ile aliyo kun’gata.

Kama kiongozi wa familia atafariki dunia, basi mnatakiwa kusimamisha saa kubwa ya ukutani inayo kaa sebuleni, vinginevyo wanafamilia walio baki nao watamfuata ndani ya kipindi kichache, vitatokea vifo mfululizo vya wanafamilia.

Baada ya kuuosha mwili wa marehemu, na kuuvisha nguo zake, unatakiwa kuweka punje moja ya chumvi kwenye kifua cha marehemu ili kuwafukuza roho na majini wabaya.

 Kama marehemu atakufa akiwa ameacha macho wazi , hiyo ni ishara mbaya sana. Maana yake ni kwamba,anatafuta watu ( ndugu zake ) wa kwenda nae kaburini. Kujiepusha na hilo, funikeni macho yake kwa kutumia sarafu .

Usifagie chumba cha marehemu kabla marehemu hajatolewa. Endapo utafanya hivyo, basi amini nakwambia wewe ndie utakae mfuata marehemu. Kama  ulikuwa  haujui  na  ukafanya  hivyo  basi  unatakiwa  kufanyiwa  tambiko  maalumu  la  kuvunja  roho  hiyo  haraka  iwezekanavyo.

Msitoe shuka wala nguo yoyote iliyopo kwenye kitanda alicho kilalia marehemu, na ambacho umauti ulimkuta. Endapo mtakiuka hilo, basi mwanafamilia mwingine atafariki ndani ya mwaka huo huo.  Kama  mlijisahau au  mlikuwa  hamjui  basi  mnatakiwa  mfanye  tambiko  maalumu  la  kuvunja  roho  hiyo.

 Kwa mara nyingine tena narudia, mwili wa marehemu unapotolewa kwenye jengo lolote lile, iwe nyumbani, kanisani, au msikitini ni lazima miguu ndio itangulie kutoka na sio kichwa, vinginevyo roho au mzimu wa marehemu huyo, utatazama katika jengo hilo na kumuita mtu mwingine wa kufuatana nae.

Marehemu azikwe mahali alipo pachagua wakati wa uhai wake, au la sivyo endapo mtaenda kinyume chake, vifo vitatokea katika familia hiyo. Na kama mtalazimisha kusafirisha mwili wa marehemu, basi msafara huo lazima utapata ajali njiani, na mtu mmoja lazima atakufa.

 Ukiugusa mwili wa marehemu, utakuwa na uhakika kwamba, roho ya marehemu haitakusumbua. Na endapo utaugusa mwili wa marehemu usoni, hutoota ndoto mbaya kuhusu marehemu huyo.

 Usipeleke mwili malaloni kwa kutumia gari lako binafsi. Ni nuksi kubwa sana kufanya hivyo. Mwili wa marehemu unapelekwa malaloni kwa kutumia gari maalumu.

 Endapo mtasafirisha mwili wa marehemu kwa basi, kichwa kitazame anapotoka na miguu itazame anapoelekea. \

Usi hesabu magari kwenye maziko (makaburini), ukifanya hivyo unakuwa unahesabu siku zako mwenyewe za kuishi.

Kuwa muangalifu usione taswira yako kwenye gari lililo beba mwili wa marehemu, vinginevyo wewe ndio utakae fuatia kubebwa kwenye gari hilo. MAGARI  MAALUMU YA KUBEBA  MIILI  YA  MAREHEMU  HUWA  YANAN’GAA  KIASI  UNAWEZA  KUJIANGALIA  UKAJIONA. SASA  BASI  EPUKA  KUANGALIA  KWENYE  GARI  HILO. IKITOKEA  UMEANGALIA  NA  KUJIONA  KWENYE  M’NGAO  WA  GARI  HILO  AU HATA KWENYE  KIOO  CHAKE  BASI  WEWE  NDIO  UTAKAE  FUATIA  BAADA  YA  MAREHEMU. KUONDOA  ROHO  HIYO  YA  UMAUTI  NI  LAZIMA  UFANYIWA  TAMBIKO, AU  UOMBEWE  AU  KUFANYIWA  DUWA.

Usiende na mtoto mchanga kwenye msiba, vinginevyo atakufa kabla hajatimiza mwaka mmoja.

Ni nuksi kubwa sana kutangulia makaburini ( kwenye maziko)  au kupita bila kushiriki kwenye maziko . Kama utafanya hivyo, utakufa ndani ya muda si mrefu.

38.  Kama paka mweusi atakatisha mbele wakati wa maziko (makaburini ) mwanafamilia mmoja katika familia ya marehemu atakufa ndani ya siku tatu. Kuvunja roho  hilo  lazima  yafanyike  maombezi, dua  au  tambiko  maalumu.

Kama ndugu yenu amekufa, kwa kuuwawa au mna wasiwasi kwamba ndugu yenu ameuwawa, basi mzikeni huku kichwa kikiwa kinatazama chini. Mtu aliye muua ndugu yenu, kama atakuwa kwenye eneo la maziko, basi hatoondoka eneo hilo hadi atakapo kamatwa. Watu wote wataondoka, lakini yeye atabaki, hapo hapo, atakuwa kama amepagawa  na kupigwa na bumbuwazi. Kama msiporudi kutazama hapo kaburini, basi hata siku tatu mtamkuta, na atakapo waona, basi ata tubu na mtafikisha kwenye vyombo vya dola.

Miaka ya sabini kushuka chini, babu zetu ilikuwa kama ndugu yao amekufa kwa kuuwawa ama kama wanahisi ndugu yao amekufa kwa kuuwawa, mfano amewekewa sumu, amenyongwa n.k,. basi walikuwa wanafanya hivi, wanatoa ini la marehemu, halafu wanazika ini sehemu tofauti na mwili wa marehemu, kwa kufanya tambiko maalumu. Ndani ya siku saba, mtu aliye muua marehemu, atapatikana katika eneo lililozikwa ini.

Kaburi lilisale wazi, likilala wazi, basi mwanafamilia mwingine katika familia ya marehemu atafariki ndani ya mwaka huo huo. Kaburi lizikwe siku liliyo chimbwa.Kaburi likilala wazi  siku ya Jumapili, basi jumapili itakayo fuata, mwanafamilia mwingine kutoka kwenye familia ya marehemu na yeye atamfuata marehemu.

Vifaa vilivyo tumika kuchimba kaburi, vinatakiwa vibakie kaburini kwa siku nyingine saba. Kuvipeleka nyumbani vifaa hivyo siku hiyo hiyo au kabla ya siku saba, ni nuksi kubwa sana.

Kuondoka makaburini kabla kaburi lote halijafukiwa, kutasababisha msiba kwenye familia yako wewe uliye ondoka kabla watu hawajamaliza kuzika. Mvua ikinyesha kwenye kaburi ambalo bado halijafukiwa, ni ishara mbaya sana kwa familia ya wafiwa.  Ili  kuepukana  na  nuksi  hiyo, inabidi  kuwe  na  mtaalamu  wa  kuzuia  mvua.

Ni nuksi  kubwa  sana  kusonta  kaburi.
Ni  nuksi  kubwa  sana kurukia  kwenye  kaburi
Ni  nuksi  kutembelea  makaburini  baada  ya  jua  kuzama.

Wafiwa  wasiondoke  nyumbani  wala  kujichanganya  mtaani na watu  wengine, hadi  matanga  yatakapo  inuliwa. Kwa  mfano  watu wengine, unakuta  mtu  amefiwa, lakini  kabla  hata  matanga  hayajainuliwa, anakwenda  bar kunywa  na  kurudi  msibani. Hayo ni makosa  makubwa  sana. Wengine  huondoka na  kurejea  makazini  kwao  kabla hata  matanga  hayajainuliwa. Jamani acheni  kudharau  mila  na  desturi  zetu. Suala  hili  limesababisha  nuksi, balaa  na  mikosi  kwa  watu  wengi  sana.

Wafiwa wote  wakuu, yaani  ndugu  wa  karibu  wa  marehemu, wasioge  hadi  baada  ya  siku  tatu, ambayo  ndio  siku  ya  kuanua  matanga, na  maji  watakayo  oga  yawe  maji  ya  moto.

Wafiwa  wasishiriki  ngono  hadi  matanga  yatakapo  inuliwa.

Waombolezaji  msibani, wasiongee  kwa  nguvu  wala  kucheka  kwa  nguvu. Ni makosa  makubwa  sana  kufanya  hivyo.

Hayo  ni  baadhi  ya  mambo  ambayo  yanaweza  kusababisha  nuksi, mikosi  na  mabalaa  kwa  mtu  ambayo huja  yenyewe  otomatiki bila  kusababishwa  na  watu  wabaya. Hayo  ni  baadhi  tu  ila  yapo  mengi  sana. Nikisema  niyataje  hapa  basi  itanipasa  kuandika  kitabu  kingine  chenye  mamia  ya  kurasa.

Sasa basi  kabla  ya  kutengeneza  uchawi  wa  kumfunga  mtu  kimapenzi, huwa  linaanza  kwanza  zoezi  la  kupima  mwili  wa  mtu  anae  taka  kumfunga  mwenzake  kimapenzi.

Zoezi  la  kupima  mwili  kama  ni msafi  au  mchafu  huwa  linafanyika  kwa  kutumia  ndege, nyama  ya  utumbo  wa  ng’ombe  au  mbuzi, nyanya, kitabu, maji  pamoja  na  njia  nyingine  nyingi.

Sasa  basi  mwanamke  huyu   akikutwa  ana  mwili  mchafu, zoezi  linalo  fuata  huwa  ni  kumsafisha  mwili  wake  halafu  baada  ya  hapo  anapikwa.

Zoezi  la  kumsafisha  mwili  huwa  linahusisha  dawa  nyingi  sana. Baadhi  ya  dawa  hizo  ni  pamoja  na  tufahaali  jinni  au  tunda  la  majini (  Tufahaal  jinni  ni  mti  wenye  Baraka  kubwa  sana  za  majini, majini  na  maruhani  wote  wazuri  huwa wanakula  tunda  hili , tunda la  mti  huu  pamoja  na  mti  huu, ni moja  kati  ya  vizimba  vikubwa  sana  kwenye   kusafisha  mwili  na  kupandisha  nyota  ya  mtu ). Dawa   na  vizimba  vingine  vinavyo  tumika  hapa  ni  pamoja  na  marashi  yaitwayo  Alwud , Ubani mzuri  (Ubani unaonukia  kuliko  ubani  wote  duniani )   Muharaka , Mpapatiko,   Miski nyeusi  ya  mafuta ( ile  ya  marashi) , Mdalasini  wa  India  na  maji yaliyo tumika  kuoshea  mchele ,   Maandishi  maalumu  karatasi arobaini (maandishi  haya  huandikwa  kwa  kutumia  hinna  au  zaafarani nyekundu ),Dhukuri Jawi ,Huzabara ,Maji  makuu  ,Mafuta  ya  mcheka  na  mbingu, mzizi  wa  mti ulio katisha  njia ,Vichali  vya  ndege  arobaini ,Kichali cha ndege  wa  porini  aitwae fundi chuma , Kamba  iliyo  tumika  kumfunga  ndege  aitwae dudumizi , Mchanga  wa  njia  panda  arobaini, ambao  huchukuliwa  kwa  dua  na  tambiko  maalumu, tumbaku, mchanga  wa  jua  la saa  saba, pamoja  na  dawa  nyingine nyingi.

 Dawa   hizi zinasagwa   pamoja kisha   zinachemshwa  kwenye  chungu, halafu   baada  ya  hapo, mhusika  anatumia  kuoga.

Baada  ya  kusafishwa  mwili, linafuata  zoezi  la  kupikwa . Hapa  huwa  kuna njia  kuu mbili, njia  ya  kwanza  anapikwa  kwenye  pipa  maalumu.

Anaingizwa  huko  kiganga  na  kupikwa  kwa  muda  ambao  mganga  atakuwa  amepokea  maelekezo kutoka kwa  mizimu  wake.

Ila  njia  hii  hutumika  zaidi  kwa  wafanyabiashara  na  watu  wanao  tafuta  kinga  kubwa.

Njia inayo tumika  kwa  mwanamke  anaye  taka  kumfunga  mwanaume  kimapenzi  huwa  inakuwa  hivi; Mwanamke huyo  atatoa  vitu  vya  kwenye  mwili  wake, kama  vile  nywele, ywele  za  kwapa  na  kucha.

 Vitu  hivyo vitachanganywa  na  dawa  maalumu  kisha  vitapikwa  kwenye  chungu  kwa  muda  ambao  utaendana  na  siku  husika.

Baada  ya  zoezi  la   kupikwa  kukamilika, zoezi  linalo fuata  huwa  ni  kupikwa  nyungu.

Zoezi  la  nyungu  huwa  linategemeana  na afya  ya  mhusika.

Kama  mhusika  anasumbuliwa  na  magonjwa  kama  vile  presha  na  kisukari, zoezi  hili  huwa  halifanyiki kwa  sababu  lina  nguvu  sana.

Kama afya  yake  ni nzuri  ndio  anapikiwa  nyungu.

Jinsi  anavyo  pikwa  nyungu, huwa  inachukuliwa  mizizi, matawi  pamoja  na  magamba  kutoka  kwenye miti  mbalimbali  ambayo  idadi yake  huanzia  arobaini  na kuendelea .

 Idadi  na  aina  ya  miti  itakayo  tumika  kwenye  nyungu  hutegemeana  na  siku na  muda  ambao  nyungu hufanyika  pamoja  na ukubwa wa  tatizo  la mteja.

Vitu vingine  vinavyo ongezwa  kwenye  nyungu  ni  pamoja  na  mawe   ya  mtoni  nakadhalika.

Miti  hii  hupikwa  kwenye  chungu  au  sufuria,  kisha  mhusika  anaenda  kufukizwa  akiwa  amevaa  kaniki   na  akiwa  amefunikwa  shuka  ambayo rangi  yake pia  itategemeana  na siku, hali ya magonjwa  na  aina  tatizo  lake.

Nyungu  hii itasaidia  kutoa  majini, mapepo, masheitwani na  roho  zote  chafu ambazo zimo ndani ya  mhusika.

 Na  wakati  majini  hao  wanatoka  huwa  sio  shughuli  ya kitoto.

Nyungu  zipo  za  aina  kuu  tano, aina  ya  kwanza  ni  nyungu  kwa  kutumia  miti  ya  porini pekee, aina  ya  pili  ni  nyungu  kwa  kutumia  dawa za  kiarabu, ya  tatu  ni nyungu kwa  kutumia  mchanganyiko  kati  ya  dawa  za  kiarabu  na  miti  ya  porini ya  nne  ni  nyungu  kwa  kutumia   miti  maalumu  ya  porini  na  ya  tano  ni  nyungu  kwa  kutumia  dawa  maalumu  za  kiarabu.

Watu  wengine  huwa  na   matatizo  maalumu ambayo   huhitaji  aina  fulani  ya  mti .

Anapotokea  mtu wa  aina  hii, basi  hutengenezewa  nyungu  kwa  kutumia  aina  ya  mti  husika.

Kama mhusika  atakuwa na  magonjwa  kama  presha  na  kisukari, basi  kitakacho fanyika  atawekwa katika chumba  maalumu  kisha  atapakwa  mafuta  ya  usiku  yaliyo  changanywa  na  mafuta  ya  miski.

 Mafuta  haya  atapakwa  kwenye  matundu  yote  ya  mwili pamoja na vidole  vyote  vya  kwenye miguu  na  mikono.

 Baada  ya  zoezi  la  nyungu  kukamilika, litafuata  zoezi  la  kufushwa.  Mwanamke  huyu  atafanyiwa  fusho  maalumu  linalo  nukia sana na  ambalo  linaendana  na siku  ya  tukio .

Akimaliza  kufukishwa  atapewa  orodha  ya  mafusho  maalumu ya  kutumia  kwa  siku  maalumu  pamoja  na  aina  ya  mavazi  ya  kuvaa  katika  kila  siku  atakayo  kuwa  anafanya  mafusho  hayo.

Baada  ya  hapo litafuatia  zoezi  la  kuchanjwa  mwili.  Mhusika  atachanjwa  pande  saba  za  mwili  kisha  atapakwa  dawa mbalimbali  kwenye  sehemu  alizo chanjwa.

Dawa  hizo  ni  pamoja  na tumbaku  pamoja  na  ndele  au ndumba  maalumu ya  mvuto  wa  mapenzi ambayo inajumuisha  dawa  na  vizimba  zaidi  ya  ishirini  na  moja.

Dawa  na  vizimba hivyo ni pamojana mpapatiko,mvuto,mwinula,kishinda wachawi, mti mkuu,mfalme wa pori,mzungu pori,lufakale, mkubashengelo,muoshafedha,muharaka  pamoja  na  dawa na  vizimba  vingine  vingi.

Vizimba  hivyo  ni  vingi  sana, siwezi kuvitaja  vyote  kwenye  kitabu  hiki na  hata kama  nitavitaja, sitoweza  kuvielezea  kwa undani, kwa sababu  maelezo yake ni  marefu  sana, ila  nitataja  vichache  na  kuvielezea  vichache  kati  ya  hivyo.

Baadhi ya  vizimba  hivyo  ni  pamoja  na  chupi  arobaini  za  wanawake  Malaya, mkia  wa  kondoo  uliokaushwa  na kusagwa pamoja  na  madawa ya  kiganga, mikia saba ya  mbwa  ambayo  ilikatwa  wakati mbwa  ameufyata  mkia na  kisha  kusagwa  pamoja na  madawa  mengine  ya  kiganga, pamoja na kizimba ambacho  kinatengenezwa  kwa  kuchanganya  miti  saba  ya  porini  pamoja  na majivu  ya mnyama  fulani wa  porini    ambae alichomwa  na  kuunguzwa  wakati akiwa  amemmeza  mnyama  mmoja afugwae.

Ni  hivi  porini  huwa  kuna  mnyama  mmoja mkubwa, huyu  mnyama huwa  anakula  wanyama wenzake.

 Miongoni  mwa  wanyama  anao  wala  ni  pamoja  na  mnyama  mmoja  ambae  hufugwa majumbani.

Jinsi anavyo mkamata  mnyama huyu afugwae  huwa  inakuwa  hivi.  Mnyama  huyu  afugwae  ana uwezo  wa  kuona  mambo  mengine  yasiyo onekana  kwa  macho  ya  kawaida, ndio  maana  hata  majumbani  huwa anafugwa  kwa ajili  ya  kusaidia  kuona  wachawi hasa  wanapokuwa  wamekuja  kuroga usiku  au  wanapokuwa  wanaondoka  usiku.

 Kinacho  mpa  uwezo  huu mnyama  huyu  ni mkuli  wake. Sasa  basi  mkuli  wa  mnyama  huyu  afugwae  unaupenda  sana, kuuheshimu na  kuutukuza  mkuli  wa  mnyama  huyu wa  porini.

Mkuli  wa  mnyama  huyu wa  porini  unatoka  katika “utawala” mmoja  na  mkuli  wa  mnyama huyu  wa  nyumbani.  Katika  utawala  wa  mikuli  ya  wanyama  wa  porini na  majumbani, mkuli  wa  mnyama  huyu  wa  porini  ni  mkubwa  sana  kiitifaki  kwa  mkuli  wa mnyama  huyu  wa  kufugwa.

Mkuli  wa mnyama  huyu  wa  porini  ni  mfalme  wa  mkuli  wa  mnyama  huyu wa kufugwa.  Mkuli wa  mnyama  huyu  wa  kufugwa  unaupenda  sana, unau heshimu  sana  na  kuutukuza  sana  mkuli wa  mnyama  huyu  wa porini.

Mnyama  huyu  wa  porini, akihisi  uwepo  wa  mnyama  huyu wa  nyumbani  katika  eneo  lake la, huwa  anatoa  ishara  ya  uwepo  wake  katika  eneo  hilo  kwa  mnyama  huyu  wa  nyumbani.

Ishara hiyo huwa  katika  mfumo  wa  harufu  maalumu  ambayo  mnyama  huyu  wa  kufugwa  akiisikia tu  basi  anatambua  uwepo  wa  mnyama  huyu wa porini.

Kwa  kuongozwa  na  mkuli wake, mnyama  huyu  wa  kufugwa  hujongea  hadi  mahali  alipo mnyama  huyu  wa  porini  ambapo  bila  kupoteza muda, mnyama  huyu  wa  porini  hummeza mnyama  huyu  wa  nyumbani.

Sasa  basi  wachawi  wa  nchi  wanapo  gundua  juu  ya  uwepo  wa  tukio  la  mnyama  huyu  wa  porini  kummeza  mnyama  huyu  wa  nyumbani, huwa  wanakwenda  haraka  na  kumchukua  mnyama  huyo, anapelekwa  njia panda  saa sita  za  usiku,  wanaitwa  wachawi  wenza  kwa  kutumia  filimbi  ya  kichawi  ambazo  hutengezwa  kwa  kutumia  dhakari ya  mnyama fulani  afugwae  ambae  anapendwa sana  na  wachawi.

Wachawi  wenza wanapo jitokeza, hufanyika  zoezi  la  kumchoma  mnyama  huyu  wa porini akiwa  katika  hali hiyo  hiyo  ya  kummeza  mnyama wa  nyumbani.

Huchomwa  pamoja  na  madawa  ya  kichawi, na  majivu yake  hutumika  katika  kutengeneza  uchawi  wa aina  mbalimbali  kama  vile  uchawi  wa kumkamata  na  kumficha  mtu  kimapenzi, kumuweka  mtu kwenye  chupa, kupambana  na  washindani  wa  kibiashara, kazini  au ushindani  wa  aina  yoyote  ile, kuwatupia  watu  uchawi , kufunika  uchawi  nakadhalika.

(KUFUNIKA  UCHAWI   NI UCHAWI  UNAOFANYWA  NA  WACHAWI  KWA  LENGO  LA  KUWAFUNGA  WATU  WALIO WAROGA  ILI  WASIJUE  KAMA  WAMEROGWA WALA  WASIPATE  WAZO  LA  KUFIKIRIA  AU KUAMINI  KAMA  WAMELOGWA. Mfano  unaweza  kukuta  familia  fulani  inalogwa  ili  kuteketezwa  kwa  ugonjwa  wa  aina  Fulani. Pamoja  na  kwamba  watu  wa  familia  hiyo  wanakuwa  wanaugua  magonjwa  ya  ajabu  na  kufa  katika  mazingira  ya  kutatanisha  lakini  hawezi  kutokea  hata  mtu mmoja  katika  familia hiyo  wa  kusema  kwamba  wamerogwa  na  hivyo  wachukue  hatua  stahiki  kama  vile  kwenda  kwa  waganga  au  kwa  watumishi  wa  Mungu.  Na  hata  ikitokea mmoja  kati  ya  wanafamilia  akapata  wazo  la  kuwashitua  waende  kwa mganga  au  kuwaona  watumishi  wa  Mungu, basi  atapata  upinzani  wa  hali  ya  juu.

Sasa  basi huyu  mwanamke, kila  atakapo  kuwa  anachanjiwa  dawa, huwa  kunakuwa  na   tamko  la  maneno  maalumu.

Kwa  mfano  wakati  anachanjiwa  tumbaku, huwa  kunakuwa na  maneno  maalumu  ambayo  yanakuwa yanatamkwa  wakati  mhusika  anachanjiwa tumbaku.

Na  wakati  anachanjiwa  hiyo  ndele , maneno  yake  maalumu  hutamkwa  pia.

Kesho  yake  asubuhi  na  mapema  mwanamke  huyu  atapewa  kuoga  maji  maalumu.

Maji  haya  huchotwa  mtoni alfajiri  na  mchotaji  anatakiwa  kuwa  ndio  mtu  kwanza  kuchota  maji  hayo  kwa  siku  hiyo.

Maji  haya  huchotwa   kwa  dua  na  tambiko  maalumu.

Maji  haya  yatachemshwa  pamoja  na  dawa  maalumu  na  kisha  mwanamke  huyo  atapewa  kukoga.

Baada  ya  mazoezi  niliyotaja  hapo  juu  kukamilika.Mwanamke  huyu  anakuwa  sasa  amewiva.  Majini  wachafu, mabalaa  na  mikosi  yote  inakuwa  imeondoka  kwenye  mwili  wake.  Na  nyota  yake  inakuwa  imepaa.

Akisha   maliza  kuoga  na  kupumzika  linaanza  kufanyika  zoezi  la  kumtazama  mwanaume  anaye mtaka.

Kupima  nyota  yake  na  kinga  yake. Kuangalia  kama mwanaume  huyo  ana  kifungo  chochote  cha  nafsi kutoka  kwa  mwanamke  mwingine.

Kama  nyota  ya  mwanaume  huyo  ipo  juu  , basi  lazima  nyota  ya  mwanaume  huyo  ishushwe  kwanza .

Hivyo basi  nyota  ya  mwanaume  huyo  itashushwa  hadi  kuwa  chini  kabisa. Hii ndio sababu  wanaume  wengi  wanaofungwa  kimapenzi huwa  wanafilisika  baada  ya  muda  fulani  na  mambo  yao  huwa  yanashuka  na  kuwachachia.

Zoezi  la  kushusha  nyota  ya  mwanaume  huyu  huchukua  lisaa  limoja  hadi  masaa  matatu  kulingana  na ukubwa  wa  nyota  yake.

Zipo  njia  nyingi  zinazo  tumika  kushusha  nyota  moja  wapo  ni  kutumia  misumari  kwenye  mti  wa  mgodo au mti  wa  majini  wabaya.

Kitu  kingine  kitakacho  angaliwa  hapa  ni  kama  mwanaume  huyu  ana  kifungo  chochote  cha  kimapenzi  kutoka  kwa  mwanamke  mwingine  yoyote  Yule.

Kama  atakuwa  na  kifungo  basi  kitaondolewa  na   nyota  ya  mwanamke  huyo  itashushwa   na  kuzikwa  au   watafarakanishwa .

Zoezi  la  kuwafarakanisha  huwa  linafanyika  kwa  kutumia  ndumba moja  chafu  sana, ndumba  hii  inatengenezwa kwa  kutumia  mavi  ya  nyani, mavi ya sokwe, mavi ya  ngedere, mavi ya mtu  ambayo  aliyanya  akiwa  porini, mavi  ya  bundi, mavi  ya  mpambe  wa  bundi ( MPAMBE  WA  BUNDI  NI  NDEGE  MMOJA  WA  PORINI  AMBAE  HUFUATANA NA  BUNDI KILA  MAHALI) Mavi  ya  ndege  wa  porini aitwae  mkatasanda, mavi ya  kinyonga, udongo  wa  kwenye  milima  miwili  ambayo  haionani  pamoja  na  dawa  nyingine  za  kichawi.

Hii ni dawa  hatari  sana. Mke na  mume  wakichomewa  dawa  hii  kama  walilala  wote  wataamka  wote  vizuri  lakini wakisha  achana  tu  kwenda  kazini  basi ndio  hawataonana  tena  wala  kukaa  pamoja  tena.

Ni  uchawi  wa  hatari  sana.  Baada  ya  kusafisha  njia, zoezi  litakalo  fuata  hapa  sasa  ni  kumvuta  mwanaume  huyo  kwa  kutumia  uchawi au  uganga.

Katika  ulozi  wa  kumvuta  mtu  kichawi, zipo  njia  nyingi  sana. Sio  rahisi  kuelezea  njia  zote . Katika  kitabu  hiki  nitazielezea  njia   tatu  ambazo  nimeona  ni  rahisi  kidogo  kuzielezea  kuliko  njia  nyingine.

Kwanza  kabla  sijaelezea  njia  hizi  tatu  moja  baada  nyingine, naomba  nielezee  sababu  kwanini  wanawake  hulazimika  kutumia  uchawi  wa  kuwavuta  wanaume  kichawi?

Sababu  kuu  ni  moja  tu, nayo ni kwamba, mwanamke  hasa  mwanamke  wa  kiafrika  hata  ampende  vipi  mwanaume , huwa  hawezi  kumtamkia  anampenda, sana  sana  atakacho kifanya  ni  kujilengesha  kwa  mwanaume  anae  mtaka  na  si kumtamkia  anampenda.

Ndio  maana  wanawake  wengi  hulazimika  kutumia  uchawi  wa  kuwavuta  wanaume  wanaowataka.  Unavutwa  mwanaume  ili  wewe  mwenyewe  umfuate  mwanamke  huyo  kumtamkia  unampenda

Katika  njia  hii  ya n kumvuta  mwanaume  kwa  kutumia  uchawi,  huwa  kuna  hatua  kuu  tatu  kama  ifuatavyo ( HATA  MWANAUME  ANAWEZA  KUTUMIA  UCHAWI  HUU  KUMVUTA  MWANAMKE )

KUPIKA  DAWA  KWENYE  MAFIGA  MABICHI.
Kwanza  huwa  linaanza  zoezi  la  kumuita  mwanaume  aliye  kusudiwa  kwa  kutumia  mafiga  mabichi  na  majani  ya  mdizi  au mgomba,

Huwa  inakuwa  kama  ifuatavyo : Kwanza  huwa  ni  lazima  kuwe  na  picha ,  nguo  au majina   au kitu  chochote  cha  mwanaume  aliye kusudiwa.

Pili  huwa  ni  lazima  iwepo dawa  ya  kiganga  iitwayo  ukurubizo pamoja  na  dawa  nyingine  za  porini  ambazo  ni Mpapatiko, Mkubashengelo, Mzungupori,  Kishinda wachawi, Mti mkuu,  Mfalme  wa  pori, Inama nikuchume   (  Hii  inama nikuchume . Ukitaka  kuichuma  inainama, ukisha  chuma  inarudi  katika  hali  yake  ya  kawaida )

Tatu  kuwe  na  Mafiga  ya  miti  mibichi . Nne  kuwe  na  mafuta  ya  usiku, Tano  kuwe  na  majani  ya  mgomba  makavu  ambayo  yatatumika  kama  kuni  za  kupikia  uganga.  ( Mti  wa  mgomba  una  matumizi mengi sana  katika  uganga, uchawi  na  tiba  )

Sita  mwanamke  huyu  lazima  awe  amevaa  vazi  maalumu  la  kiganga  kwa  ajili ya  shughuli  ya  kupika  huu  uganga  wa  kumuita  mwanaume.              

Siku  hiyo  jua  halitazama, mtu huyo  atakutafuta .  Kama  unaishi nae  katika  mji  mmoja  atakuja  siku  hiyo  hiyo. Kama  anaishi  mkoa  wa  mbali  au nje ya  nchi, atapanga  safari  yake  siku  hiyo  hiyo  na  kesho  atakutaarifu  anakuja.

Itachukuliwa  picha  au jina  au  kitu chochote  cha  mwanaume  huyo  vitawekwa  kwenye  chungu, pamoja  na  maji, dawa  nilizo zitaja  hapo  na  mafuta  ya  usiku. Chungu  hiki  kitawekwa  kwenye  mafiga  mabichi  ambayo  yatachochewa  kwa  kutumia  majani  makavu  ya  mgomba.

Vitu  vyote  hivyo  vitapikwa  kwenye  hicho  chungu  huku  maneno  maalumu  ya  kiganga  yakitamkwa. Zoezi  hili  litafanyika  kwa  muda  wa  dakika arobaini.

Baada  ya  hapo itafuata  hatua  ya  pili  ambayo  hujulikana  kama  herufi  za  moto. Katika  njia  hii  huchukuliwa  mayai  saba  ya  kuku  wa  kienyeji , kila yai  litaandikwa  herufi saba  za  moto. Hizi  herufi  ni  herufi za  majini  na  kila  herufi  inasimama  badala  ya  majini  mia  saba  wa  moto  na mvuto  wa  mapenzi.  Ni herufi  hatari  sana.  Herufi hizi  zitaandikwa  kwa  kutumia  hina. Yaani  hina  itatumika  kama  wino  na  kijiti  kitakacho  tumika  kuandikia  herfu  hizo lazima  kiwe  kijiti cha  mti  wa  msufi  ambacho  kilichumwa  kwa  kutumia  tambiko  maalumu . Mti  wa  msufi una  Baraka  kubwa  sana  za  majini  na  maruhani  wazuri. Ni  sawa  na  mti  wa  mkomamanga, mkuyu, mzeituni au mkunanazi.

Hina ina  majini  na  maruhani  wakali  sana  wa  mapenzi, ambao  nikisema  niwaelezee  hapa  mmoja  mmoja  pamoja  na  kazi zao  na  jinsi  wanavyo  tumika, nitatakiwa  kuandika  vitabu  vingine  mia  moja.

Ndio  maana  mabibi  harusi  na wanawake wa  Pwani  ya  Afrika  Mashariki kwa  ujumla huwa   wanapenda  sana  kujiremba  kwa  kutumia  hina. Hii  ni kwa sababu  hina ina  maruhani  wenye  mvuto mkali  sana  wa  mapenzi. Nashauri  kila  mtu  ajifunze  jinsi  ya  kutumia  hina  kwenye mvuto  wa  mapenzi, kwa  sababu  ipo  namna  maalumu  ya  kutumia  hina  kwenye  mvuto  wa  mapenzi.

Hina  inapochanganywa  na  dawa  nyingine tatu  za  porini, na  kutumika  kuogea , huwa  na  mvuto  mkubwa  sana  wa  mapenzi. Nashauri  kila  mwanandoa  au  kila  aliye  kwenye  ndoa, atumie  dawa  hizi kwa  ajili  ya  kuogea. Atapata  matokeo mazuri  sana  kwenye  ndoa  yake. Anaweza  kutumia  kwa  kuchanjiwa  pia.

  Kijiti cha  mti  wa  msufi, kinachovwa  kwenye  hina iliyopondwa  na  kukorogwa  na  maji  kisha  kinatumika  kuandika  hizo  herufi  saba  za  moto  wa  mapenzi.

Herufi  hizi  huandikwa  kwenye  yai  kwa  lugha  maalumu ya  kitabibu.

 Kila  herufi  huwa  ina  majini  wakali  wa  mapenzi  wapatao  mia saba. Huu  ni  uchawi  mkali  sana  wa  kimapenzi  na  unashauriwa  usimfanyie  mtu  kwa  kumkomoa.

Baada  ya  kuandika  herufi  hizi  saba  kwenye  kila  yai, unachukua  hayo  mayai  unakwenda, ima njia  panda, ima kando kando ya  mto, ima kando kando ya  ziwa, ima  kando  kando  ya  bahari, ima  porini au  sehemu  yoyote   iwe  nyumbani  kwao  au  mahali  popote  utakapo  ona  pana  faa.

 Ukifika  sehemu  hiyo  unachimba  shimo, ndani  ya  shimo  hilo  una mwaga  dawa iitwayo  kishinda  wachawi,  pamoja  na  mti wa  hina, unaweka  mayai  yako, kisha  unanyunyizia  mafuta  ya  usiku,  unafukia  halafu baada  ya  hapo, unaweka  mkaa  juu  ya  shimo  hilo, unawasha  mkaa  huo  huku  ukitamka  maneno  maalumu  ya  kiganga. Unapokuwa  unaweka  mayai  yako, hakikisha  unakadiria  kuwa  moto  au  joto  la  moto  wako  litayafikia  mayai.

Huu  ni uchawi  hatari  sana. Uliemkusudia ataanza  kufanya  mipango ya  kuja  kukuona  wakati  huo  huo.

Hii   ni   hatua  ya  pili. Katika  hatua  hii  ya  tatu  huwa  vinachukuliwa  vitu  vifuatavyo :Chumvi  ya  mawe  punje  21, Mtama  mweupe  punje 21 Mpapatiko , Mwita ,Mvuti, Mkurungu ,Mwinula ,Maseko , Mfupa  wa  nyama  au  samaki  iliyo  tupwa  zamani ikakauka..inatwangwa  na  kuwa  kama  ubani.

 Vitu  vyote  hivi  vinachanganywa  na  kusagwa  kwa  pamoja  kisha  kinatafutwa  kigae  cha  chungu  au  mtungi  ulio pasuka wenyewe  zamani.

Dawa  hii  inachukuliwa  na  kisha inawekwa  kwenye  kigae  cha  chungu  au  mtungi  ulio pasuka  zamani.  Zoezi  la kumuita  mtu  aliye kusudiwa  litafanyika  kupitia  kwenye  kigae  au  chungu  kilicho  pasuka. Baada  ya  hatua  hii  itafuata hatua  ya  nne, katika  hatua  hii  ya  nne,. Litafanyika  zoezi  la  kumuita  mtu  kwa  kutumia  koroboi.

Hapo  wachawi  huchukua   kipande  cha  sanda  iliyo tumika  kumvisha maiti ,  mwita, mpapatiko,kalimukamwi,mafuta  ya  mbarika ndogo, kishinda wachawi, mfalme  wa  pori pamoja  na  mafuta  ya  taa  ambayo  hutakiwi kuyaomba  wala  kuyanunua.  Kipande  hiki cha  sanda  ndio  kitatumika  kama  utambi  wa  kumuita  mtu  aliye  kusudiwa  na  huviringishwa  pamoja na  dawa  nilizo zitaja hapo  juu  pamoja  na  mafuta  ya  mbarika  ndogo.  Hutakiwi  kutumia  mafuta  ya  taa  uliyo nunua  au  uliyo yaomba, kwa  sababu  huyu mtu  haumbembelezi,. Ila unamuita  kwa  lazima.

Utambi  utawashwa  na  mhusika  atakuwa  anatamka  maneno  maalumu  ya  kumuita  mpenzi  wake.  Kama  anae  fanya  zoezi  hili  ni  mwanaume, lazima  awe  na  mti  wa  mnyaa.  Hii  inawahusu  wale  wanaume  ambao wamekimbiwa  na  wake  zao. Mti wa  mnyaa, kipande  kitafungwa  mlangoni, hal;afu  kipande  kitatumika  kuchora  kuanzia  mlangoni  kwenda  hadi  uvunguni  mwa  kitanda  anacho  lalia yeye  na  ambacho  amekusudia  huyo  mke  wake  aje  alale  hapo, na  akisha  lala  kipande  hicho  cha  mnyaa  kitachukuliwa  na  kutengenezwa ndumba  nyingine.  Hii  inaweza  kufanya  na  mwanamke  pia  ila  sharti awe  amevaa  vazi  maalumu.

Mtu  akiitwa  kwa  njia  hii, huja  haraka  sana  na  anapokuja  zoezi  linalo  fuatwa  huwa  ni  kufungwa.

Zoezi  la  kumfunga  mwanaume  kichawi  hufanyika  kwa  lengo  la  kumfunga  mwanaume  asibanduke  kwa  mwanamke huyo, na  awe  nae  na  kufuata  kila  kitu  anacho  kitaka  mwanamke  huyo  katika  siku  zote  za  maisha  yake.  Zoezi  hili  hufanyika  kwa  kutumia dawa  za  kulisha, kuogesha  na  kulisha.

Baadhi  ya  vizimba  vinavyo  tumika  katika  kutengeneza  ndumba  ya  kumlisha  mwanaume  kwa  lengo  la  kumfunga  asiondoke  ni  pamoja  na :  Vinachukuliwa  vizimba  zaidi  ya  arobaini, vinaunguzwa  na  kusagwa  halafu  mwanaume  analishwa .

Jinsi  anavyo  lishwa. Siku  ya  kwanza   mwanamke  anakaa  uchi  wa  mnyama, anachukua  dawa  anapaka  kwenye  viganja  vyake  kisha   vyote  kisha  anasugua  dawa  hiyo  pamoja  na  uchafu  wa  kwenye  viganja  vyake. Uchafu  huo  unachanganywa  na  dawa  nyingine,kisha  mwanaume  analishwa  kupitia  chakula. Wakati  anakwangua  uchafu  wa  kwenye  viganja  vyake  anakuwa  anatamka  maneno  maalumu.

Siku  ya  pili, anajipaka  dawa  hiyo  na  asali  mwili  mzima  kisha  anakaa  kwenye  beseni  na  kujisugua  uchafu  wa  mwili  mzima kisha  uchafu  huo  ulio changanyikana  na  dawa hiyo  unachanganywa  na  dawa  nyingine  kisha  mwanaume  husika  analishwa.

Siku  ya  tatu   anachukua  mchele  kilo  tatu  anauchanganya  na  MAJI  MAKUU  lita  tano  anauacha  usiku  kucha, ikifika  asubuhi  anauengua  mchele  anabaki  na  maji, halafu  anayachukua  hayo maji  Anaya  chemsha  pamoja  na  mdalasini  wa  India  ulio  sagwa,  anapasuliamo  mayai arobaini  ya  kuku  wa  kienyeji,  anaongezamo  marashi  ya  rose  pamoja  na  dawa  ya  kishinda  wachawi, mkubwa  shengelo, mafuta  ya  mcheka  na  mbingu.

Vitu  hivyo  vikisha changanyikana, anaoga  akiwa  juu  ya  meza  huku  anatamka  maneno  maalumu.

Kesho  yake, anatafuta  njiwa  saba  au  kuku  saba  anawalisha  ule  mchele  wote  anabakiza  kiasi kidogo  ambacho  kitapikwa  na  mmoja  kati  ya  kuku  alio walisha  mchele, na  wakati  wa  kuliwa  kitaliwa  kikiwa  mgongoni  mwake , yaani  mgongo  wake  utatumika  kama meza.

Hili  ni  tambiko  hatari  sana na  hufanyika kwa  ajili  ya  mwanamke  kutaka  kumtawala  mume  wake.

Jinsi  ya  kumzindua  mwanaume  au mwanamke  aliye  fungwa  kwenye  uchawi  wa  mapenzi, huwa  yanafanyika  matambiko  ya  aina  mbalimbali. Matambiko  haya  yana  hatua  nyingi  sana  siwezi  kuelezea  kila  hatua  kwenye  kitabu  hiki, ila kwa  ufupi  yamegawanyika  katika  aina  kuu mbili; Aina  ya  kwanza  ni  pale  mhusika  anapokuwa  mbali  na  aina  ya  pili  ni  pale  mhusika  anapokuwa  karibu. 

Kama  mhusika  yupo karibu  atalishwa  dawa  maalumu  na  kutapika  uchawi  kisha  uchawi  huo  utaenda  kuteketezwa  njia  panda. Na  kama  mhusika  yupo  mbali, tambiko  huwa  linaenda  kufanyikia  chini  ya  mti  mmoja  mkubwa  sana  katika  uganga.

Mti  huu  una  sifa  moja  kubwa. Kwanza, huwa  hakuna  kitu  chochote  kibaya  kinacho  kaa  katika  mto  huu, kiwe  nyoka, kiwe  mdudu  mbaya  au  kiwe  jinni  au  shetani  mbaya.  Na  pili  mti huu  una  tibu  magonjwa  karibu yote  na  unatumika kuogea  kwa  ajili  ya  kuondoa  mabalaa  na  kupandisha  nyota.

Kikubwa  mti  huu  hutumika  kubatilisha  mabalaa  na  uchawi  wa  aina  zote.  Mti  ambao  katika  kila  nyumba  ya  mganga  lazima  uwepo. Ni mti  ambao  kila  nyumba  inatakiwa  kuwa  nao.

Mganga  atakwenda  kwenye  mti  huu  muda  maalumu  ambao  utaendana na  siku  husika. Atakwenda  na  pemba  nyeupe  arobaini, kuku weupe  saba, mayai  arobaini  ya  kuku  wa  kienyeji na  punda  mmoja  mwenye  alama  ya  msalaba  shingoni.

Akifika  katika  eneo la  mti  huo, atatoa  kafara  kisha  litafanyika  tambiko  maalumu  la  kubatilisha   uchawi. Mambo  mengi  yatakayo  fanyika  siku  hiyo  yatakuwa  yakifanyika  huku  mganga  akiwa  anatembea  kinyume, Mfano  atauzunguka  mti  huo  kinyume  nyume  mara  arobaini na  kadhalika.

Kwa  ufupi  ili  kuepukana  na   shari  za  wachawi  na  watu wabaya, ni  vyema  kujilinda  na  kujikinga  ili  kujiepusha  na  usumbufu usio kuwa  wa  lazima.

Popular posts from this blog

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia.  Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katika miradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato.  Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake k ij iji cha  Itiry o   kusherekea sikukuu ya Pasaka.  Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ...

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4 Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu. Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo  Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni maalum kwa ajili ya bajeti. Ratiba hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne, ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25. Mbali na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017 ==>Itazame hapa ratiba kamili ya mkutano huu...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...