Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2017

Waziri Mkuu: Ni Marufuku Wazee wa Miaka 60 Kutozwa Kodi za Majengo

Waziri Mkuu: Ni Marufuku Wazee wa Miaka 60 Kutozwa Kodi za Majengo WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka maofisa wa Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania (TRA) wakusanye kodi za majengo kwa kuzingatia sheria na wasitoze kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60. “TRA ijipange kukusanya kodi za majengo kuanzia Julai mosi 2017. Katika kutekeleza jukumu hilo, zingatieni sheria. Tusisikie mnawadai kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 kwa majengo wanayotumia kama makazi yao,” alisema Majaliwa. Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa Wilaya ya Chato waliohudhuria uzinduzi wa jengo la TRA wilayani humo mkoani Geita. Waziri Mkuu amewataka moafisa hao wakusanye kodi ya majengo kwenye maeneo ya mjini na siyo vijijini kwani kodi hiyo haiwahusu. “Msiende vijijini. Nyumba za nyasi au za tembe hazihusiki. Tembeleeni nyumba za mijini. Piteni kwenye mitaa, muainishe aina zote za nyumba zinazostahili kulipiwa kodi. Mkishafanya sens

Shahidi ( OCCID) Asimulia Jinsi Alivyomkamata Tundu Lissu

Shahidi ( OCCID) Asimulia Jinsi Alivyomkamata Tundu Lissu Mkuu  wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu (ZCO), Camilius Wambura kumtaka afanye hivyo. Mgonja ambaye ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa. Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, shahidi huyo alidai kuwa Juni 28, mwaka jana, Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama hiyo. Alidai kuwa Juni 29 mwaka jana saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni, ambapo alimkamata na kumfikisha katika ofisi ya ZCO na kumkabidhi. “Nilipewa amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamla

Bunge lapinga ongezeko la ushuru vinywaji baridi

Bunge lapinga ongezeko la ushuru vinywaji baridi Serikali  imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2017 wenye marekebisho ya sheria 15 ikiwamo Sheria ya Ushuru wa Bidhaa. Kwa mujibu wa marekebisho hayo, ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi umeongezeka kutoka Sh 58 kwa lita hadi Sh 61 ikiwa ni sawa na ongezeko la shilingi tatu.  Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imepinga ongezeko hilo la shilingi tatu kwenye vinywaji baridi ikisema hatua hiyo itazorotesha ukuaji wa viwanda nchini. Akiwasilisha Muswada huo jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema sheria hizo zinahusu masuala ya fedha, kodi, ushuru, tozo, na mawasiliano ili kupunguza, kurekebisha, au kufuta viwango vya kodi, ushuru, ada na tozo mbalimbali ili kuboresha ukusanyaji wa kodi. Dk Mpango alisema marekebisho hayo yamezingatia mkakati wa taifa wa kukuza uchumi wa viwanda, na kwamba kiwango cha ushuru kwa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini kimepunguzwa au

Madiwani na Naibu Meya CHADEMA Watiwa Mbaroni Arusha

Madiwani na Naibu Meya CHADEMA Watiwa Mbaroni Arusha Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Viola Likindikoki, pamoja na madiwani wengine wawili wa Chadema wamekamatwa jana na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika. Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesema Viola pamoja na madiwani hao wawili walikamatwa  jana Alhamisi  wakiwa katika mkutano wa ndani uliokuwa ukisikiliza kero za wananchi. “Nipo Tanga kikazi na nilimkaimisha nafasi yangu Viola, kwa kawaida Alhamisi tunasikiliza kero za wananchi, wakati wakiendelea kusikiliza kero ndipo walipokamatwa,” alisema. Wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni diwani wa viti maalumu (Chadema), Kata ya Ngarenaro Happiness Charles na diwani wa Viti Maalumu kata ya Olorieni, Sabrina Francis. Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kwa kifupi kwamba jeshi lake linawashikilia kwa uchunguzi. Diwani wa viti maalumu (Chadema), Jenipher Lomayan  amesema madiwani hao wal

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 23

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 23

Pichaz + Video: Watu Wafariki, Wanasa Kwenye Jengo Linalowaka Moto London

Pichaz + Video: Watu Wafariki, Wanasa Kwenye Jengo Linalowaka Moto London  Jengo hilo liliteketea kutokana na kile kilichodaiwa friji bovu, japokuwa kikosi cha zimamoto hakijathibitisha ripoti hiyo. WATU kadhaa wamethibitika kufariki baada ya moto mkubwa kutokea usiku wa manane katika jengo moja magharibi mwa Jiji la  London, Uingereza, ambao unasemekana ulisababishwa na friji mbovu. Familia zinazokaa katika jengo hilo, zilisikika zikipiga kelele kuomba msaada, wakati wengine wanenasa sehemu mbalimbali ndani ya jengo hilo lenye ghorofa 27 linaloteketea na kutishia kuanguka. Zaidi ya wakati 600 jengoni humo walijaribu kujiokoa ambapo huduma za magari ya wagonjwa zimesema watu 50 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali za jiji hilo. Habari zaidi zinasema watu walionasa ndani yake walifunga mashuka yao na kuyatumia kama kamba na kujirusha kupitia madirishani ili kujiokoa. Mashuhuda wamesema waliwaona watu wengine wakiruka kutoka katika ghorofa ya 15 ili kujiokoa na wengi