Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2017

Mbowe azungumzia watakachofanya sheria mpya vyama vya siasa Ikipita

Mbowe azungumzia watakachofanya sheria mpya vyama vya siasa Ikipita Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema iwapo Sheria Namba Tano ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 itawasilishwa bungeni wa ajili ya kupitishwa watakuwa tayari kufa kuliko kukubali ipitishwe. Akizungumza jana Jumanne jioni wakati wa kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Ibhigi, iliyopo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Emmanuel Simba, Mbowe amesema kama kuna wakati wanaume wanatakiwa kusimama wahesabiwe ni wakati huo. Alisema kupitisha sheria hiyo maana yake ni kuingiza ubatili walioufanya ili uwe sheria kamili, kwamba hakuna mikutano ya vyama vya siasa, hakuna majadiliano ya mustakabali wa nchi. "Wanaanda mkakati wa kubadilisha sheria ya vyama  vya siasa taarifa tunayo,  wanataka kuiingiza sheria hiyo kwa nguvu, Sugu(Joseph Mbilinyi) tunaanzia bungeni, wakati huo ukifika wakituua watuue, wakitunyonga watunyonge hatutakubali tutaandamana mahali popote," alisema Mbowe. Mbowe

Umuhimu wa kusamehe

Umuhimu wa kusamehe Katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasaikolojia miaka ya nyuma, waligundua ya kwamba watu wengi hawana maendeleo yao binafsi kwa sababu hawatambui nguvu ya msamahama iliyovyo na nguvu katika safari ya Mafanikio. Tafiti hizo hizo zinaendelea kusema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wamebeba mizigo mizito ndani nafsi zao. Mizigo hiyo mizito ambayo inawezekana kuna mtu alisabibisha mtu kuwa katika hali hiyo. Kwa mfano inawekana kuna ndugu,rafiki, mzazi aliwahi kufanya au kukutamkia maneno mazito ambayo yanakufanya Leo, kesho mpaka kesho kutwa usiwe kuyasahau. Maneno au vitendo hivyo vimekusababisha kwa kiasi kikubwa hupunguza hamasa za kiutendaji, magonjwa na mawazo mengi (stress). Hebu tuangalie japo kwa uchache ni kwa kiasi gani madhara ya kutokusamehe yanavyoweza kukuathiri. Msipo msamehe mtu kunakupekea kwa kiwango kikubwa kuweza kupunguza uwezo wa kufikiri vitu vipya, hata hivyo pamoja na kupunguza uwezo wa kufikiri kunakupelekea kuzama

Kilimo Bora Cha Nyany

Kilimo Bora Cha Nyanya   Utangulizi: Kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara nyanya hulimwa sehemu nyingi duniani . Asili yake ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.  Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Aina hii Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa) 1. OPV (Open Pollinated Variety) - Aina za kawaida 2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.Nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa na kuzaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuhari

Mbinu 5 za kuanza na kukuza biashara kwa mtaji mdogo

Mbinu 5 za kuanza na kukuza biashara kwa mtaji mdogo 1. Jipe muda, biashara haitaweza kukua haraka kama unavyofikiri Uzuri wa kuanza biashara na mtaji kidogo ni kwamba kila mtu anaweza kufanya hivyo. Lakini pia urahisi huu wa kuanza biashara kwa mtaji kidogo unafanya ukuaji wa biashara kuwa wa taratibu sana. Hivyo unapofanya biashara yoyote ambayo unaanza na mtaji kidogo ni muhimu ukajipa muda ili kuweza kukuza mtaji wako. Usiwe na tamaa ya kutaka kukuza biashara hii haraka, unaweza kuingia kwenye maamuzi ambayo yatakugharimu zaidi. Endelea kufanya biashara yako huku ukijifunza zaidi na kuangalia kila fursa ambayo unaweza kuitumia kukuza biashara yako. 2. Kuza mtaji wako taratibu Kwa mtaji huo mdogo ambao umeanza nao biashara, endelea kuukuza kila siku. Usiendeshe biashara kwa kula kila kipato unachopata, badala yake tenga sehemu ya akiba irudi kwenye biashara yako. Fanya hivi kwa nidhamu ya hali ya juu sana na unahakikisha kila unapopata faida sehemu inarudi kwenye b

Rais Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani

Rais Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani saa chache baada ya jeshi la Zimbabwe kutwaa madaraka, kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari nchini Afrika Kusini. "Mugabe anajiandaa kuondoka madarakani," mtandao wa wa News24 uliandika bila ya kutoa taarifa zaidi. Misukusuko ya kisiasa imekuwa ikiongezeka tangu Mugabe hivi majuzi amfute Emmerson Mnangagwa, mshirika wake wa miaka mingi kama makamu wa Rais. source : BBC

Julio ailipua Simba

Julio ailipua Simba Kocha Jamhuri Kihwelu Julio amesema kwa sasa Simba wanavuna walichokipanda kuhusu usajili wa Shomari Kapombe ambaye tangu amesajiliwa na klabu hiyo bado hajacheza mechi yoyote wala kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine kutokana na kuuguza majeraha. Jana Jumatatu Nov 13, 2017 alisikika Mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba Zacharia Hans Poppe akisema, Kapombe anatakiwa kuchagua kucheza au kutocheza lakini klabu hiyo haitaendelea kumlipa mshahara huku akiwa hafanyi kazi. “Simba wanavuna walichopanda, wakati Simba wanacheza ligi wakiwa katika kumalizia mzunguko wa pili wa msimu uliopita, mimi nilipata bahati ya kuwa mmoja ya wachezaji au kocha wa zamani wa Simba nikitunguza na timu kwa ajili yak u-motivate wachezaji na kuwajenga kisaikolojia ili tuweze kufanikiwa nadhani matanda yalionekana kiasi kwamba hata Mavugo ambaye alionekana yupo chini lakini nilijaribu kukaa nae na akaanza kufunga”amesikika Julio kupitia kituo kimoja cha redio. “Kwa upa

Viongozi wa TSSF watiwa mbaroni

Viongozi wa TSSF watiwa mbaroni Viongozi wa  Taasisi ya Kusaidia Jamii ( TSSF) ambayo ilitangaza kuwa inatoa mikopo ya elimu ya juu wamekamatwa na polisi baada ya kugundulika kuwa ni matapeli. Wakurugenzi hao wamekamatwa jana Jumatatu jioni mara tu baada ya mkutano wa waandishi wa habari na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha wa kuelezea kuhusu uchunguzi uliofanyika baada ya Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi kuomba mwongozo bungeni. Chumi alitaka ufafanuzi kuhusu uhalali wa taasisi hiyo baada ya kutangaza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kulipa Sh 30 000 kama ada ya maombi ya kusajiliwa kuomba mkopo. Hata hivyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema  Serikali haitambui taasisi hiyo na kuahidi kufanya uchunguzi. Akizungumza leo Jumanne, Ole Nasha amesema baada ya uchunguzi huo wamebaini kuwa taasisi hiyo haina uwezo wa kutoa mikopo kwa wanafunzi 50,000 ambao ilitangaza kutoa. Amesema ka

Lady Jaydee akunwa na Aslay

Lady Jaydee akunwa na Aslay  Aslay Isihaka MKONGWE katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee amefungukia kukunwa kwake na kazi za msanii mwenzake, Aslay Isihaka anazozifanya kwa sasa. Akipiga stori na Risasi Vibes juzikati, Lady Jaydee alisema anapohitaji kusikiliza muziki mzuri, husikiliza muziki wa Dogo Aslay na amekuwa akiusikiliza hata kutwa nzima kwa kuwa kazi zake za sasa, zinakata kiu ya burudani anayoitaka. Lady Jaydee “Mimi ni mwimbaji, lakini haina maana kwamba sipati burudani kwa wenzangu, mfano huwa natumia saa nyingi, wakati mwingine nashinda kutwa nzima nasikiliza kazi za Aslay, anajua kuimba na kuandika nyimbo nzuri,” alisema Jaydee

Tambwe arejesha furaha Yanga

Tambwe arejesha furaha Yanga MSHAMBULIAJI AMISSI TAMBWE. Mshambuliaji Amissi Tambwe amerejesha furaha Yanga baada ya jana kwa mara ya kwanza kuanza mazoezi kufuatia kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha. Tambwe amekosa mechi zote za Ligi Kuu Yanga tangu kuanza kwa msimu huu, lakini sasa inaelezwa kuwa anaweza kushuka dimbani baada ya mchezo ujao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Mechi ijayo ya Yanga itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons itakayopigwa Uwanja wa Uhuru Jumamosi ya Novemba 25, mwaka huu. Katika mazoezi ya jana asubuhi, Tambwe alifanya mazoezi mepesi ya peke yake na ametakiwa kufanya hivyo kwa angalau siku tatu kabla ya kuanza kujifua kamili na wenzake. Meneja wa Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, Hafidh Saleh, aliliambia Nipashe baada ya mazoezi hayo jana kwamba, pamoja na Tambwe kuanza kujifua, hatocheza mchezo wa Jumamosi. “Kwa mchezo wa Jumamosi hatowez

Lawrence Masha ajivua CHADEMA

Lawrence Masha ajivua CHADEMA Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha amejivua uanachama wa CHADEMA akidai upinzani hauna nia ya kutafuta fursa ya kuunda Serikali. Lawrence Masha amejivua rasmi uanachama huo wa CHADEMA ikiwa ni miaka miwili tangu ajiunge na chama hicho mwaka 2015 akitokea CCM. Isome hapa barua yake

CHADEMA Wamjibu Lawrence Masha

CHADEMA Wamjibu Lawrence Masha Baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao baada ya mwanachama wao Lawrence Masha kujivua uanachama na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa kama sababu za kujivua kwake. Kwenye kurasa zao mbali mbali za mitandao ya kijamii Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika ujumbe akisema safari ya kupigania usawa na haki ni safari ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo ni aibu kwani kuna wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa safari. “Lawrence Masha , struggle ya kupigania usawa,haki na demokrasia, ni safari ndefu na ngumu ,wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na wanawake imara wanaendelea na safari,sio uamuzi mbaya uliochukua ila ni uamuzi wa aibu . Utajua baadaye na sio sasa”, ameandika Godbless Lema. Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo wan

CCM Wampuuza Lowassa.....Wawataka Wananchi Wasidanganyike na Ahadi

CCM Wampuuza Lowassa.....Wawataka Wananchi Wasidanganyike na Ahadi Wakazi wa Kata ya Moita wameombwa kumchagua mgombea wa CCM ili wapate maendeleo na kuachana na ahadi alizowapa, Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati kuu, Chadema, Edward Lowassa. Lowassa aliyewahi kuwa mbunge wa Monduli ndiye aliyezindua kampeni za udiwani za Chadema katika kata hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwaahidi wananchi kuwa hatawasahau na ataendelea kushirikiana nao, kwani aliwaacha wakiwa tayari wana umeme, maji na shule mbili za kata. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaban Mdoe akizungumza katika kampeni eneo la Moita Bwawani, alisema wananchi wasidanganyike. Mdoe alisema kwamba wakimchagua mgombea wa CCM, Prosper Meyani kero zao zitapatiwa ufumbuzi, ikiwamo kero ya maji na barabara. “Msidanganywe na Chadema, hawawezi kutatua kero zenu, alikuwepo diwani wao, hadi amejiuzulu, mbunge wa zamani Lowassa hivi sasa hawezi tena kuwasaidia,” alisema.

Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga Wahalifu Si Mugabe

Jeshi la Zimbabwe: Tunawalenga Wahalifu Si Mugabe Jeshi  la Zimbabwe limesoma taarifa kwenye kituo cha runinga cha serikali ZBC, likisema kuwa linachukua hatua ya kuwalenga wahalifu nchini humo.  Hata hivyo, limesema kuwa hayo si mapinduzi ya kijeshi na Rais Mugabe yuko salama. Milio mikubwa ya risasi ilisikika katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu Harare mapema jana.  Taarifa hiyo ya jeshi ilikuja saa kadhaa baada ya jeshi kudhibiti kituo cha utangazaji cha  ZBC. Grace Mugabe anaonekana kukaribia kukirithi kiti cha mumewe Mwanamume mmoja ambaye alikuwa amevaa sare za jeshi alisema kuwa jeshi linataka kukabiliana na watu ambao wanatenda uhalifu unaoleta madhara ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe. “Wakati tutakapomalizia wajibu wetu, tunatarajia kuwa hali itarudi kuwa kama kawaida.” Taarifa hiyo ilisema kuwa Mugabe,  93, na familia yake wako salama.  Haijulikani ni nani anaongoza hatua hiyo ya kijeshi.  Magari ya wanajeshi waliojihami kwa sila

Breaking News: Mume wa Irene Uwoya Afariki Dunia

Breaking News: Mume wa Irene Uwoya Afariki Dunia Aliyekuwa  mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji Hamad Ndikumana (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo, chanzo cha kifo chake kikisemekana ni matatizo ya moyo ambapo jana alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida. Mpaka anakutwa na umauti alikuwa akicheza katika timu ya APOP Kinyras Peyias FC ya  Cyprus.  Alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia alikuwa ametengana na Uwoya kwa mingi na alikuwa ndiye mkewe waliyefunga naye ndoa katika Kanisa Katoliki na walibahatika kupata mtoto mmoja  ambaye jina lake ni Krish.

Picha: Bilionea Wa Nyumba za Lugumi Alivyopanda Daladala Baada ya Kujidhamini Polisi

Picha: Bilionea Wa Nyumba za Lugumi Alivyopanda Daladala Baada ya Kujidhamini Polisi 'Bilionea' wa nyumba za Lugumi, Dk Louis Shika  jana aliachiwa na kwenda kupanda daladala kuelekea nyumbani huku akisema mpango wake wa kununua nyumba za Lugumi uko palepale. Baada ya kuachiwa na polisi jana Jumanne jioni alisema kwamba bado mpango wake wa kununua nyumba hizo uko palepale. Alisema anachosubiri sasa ni fedha kuingizwa kwenye akaunti yake na kulipa asilimia 25 anayodaiwa. "Siku nikipeleka fedha nataka Yono na TRA waite waandishi wa habari waone na wautangazie umma," alisema. Alisema vyombo vya habari vimetoa taarifa zake lakini vitaumbuka siku akienda kupeleka fedha hizo. Aliendelea kusisitiza kwamba nyumba hizo zinahitajiwa na kampuni yake ambayo hakuitaja. Njiani wakati akielekea kwenye kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja, Dk Shika alikuwa kivutio kwa watu aliokuwa akipishana nao. Alipopanda daladala la Tabata Mawenzi,