Skip to main content

Mbinu 5 za kuanza na kukuza biashara kwa mtaji mdogo

Mbinu 5 za kuanza na kukuza biashara kwa mtaji mdogo



1. Jipe muda, biashara haitaweza kukua haraka kama unavyofikiri
Uzuri wa kuanza biashara na mtaji kidogo ni kwamba kila mtu anaweza kufanya hivyo. Lakini pia urahisi huu wa kuanza biashara kwa mtaji kidogo unafanya ukuaji wa biashara kuwa wa taratibu sana. Hivyo unapofanya biashara yoyote ambayo unaanza na mtaji kidogo ni muhimu ukajipa muda ili kuweza kukuza mtaji wako. Usiwe na tamaa ya kutaka kukuza biashara hii haraka, unaweza kuingia kwenye maamuzi ambayo yatakugharimu zaidi. Endelea kufanya biashara yako huku ukijifunza zaidi na kuangalia kila fursa ambayo unaweza kuitumia kukuza biashara yako.

2. Kuza mtaji wako taratibu
Kwa mtaji huo mdogo ambao umeanza nao biashara, endelea kuukuza kila siku. Usiendeshe biashara kwa kula kila kipato unachopata, badala yake tenga sehemu ya akiba irudi kwenye biashara yako. Fanya hivi kwa nidhamu ya hali ya juu sana na unahakikisha kila unapopata faida sehemu inarudi kwenye biashara yako. Pia endelea kuangalia kwa mazingira uliyonayo na kwa biashara unayofanya ni kwa jinsi gani unaweza kukuza mtaji wako zaidi. Kama utafikiria hili kila siku, hutakosa majibu ambayo yatakusaidia.

3. Punguza gharama za biashara na za maisha pia
Kuwa kwenye biashara haimaanishi kwamba ndio una uhuru wa kufanya chochote unachotaka na fedha za biashara hiyo, kwa sababu tu ni zako. Wewe sasa upo kwenye wakati mgumu wa kukuza biashara yako huku ukiwa huna njia nyingi za kufanya hivyo. Hebu kwa sasa punguza kabisa gharama zako za kibiashara na za maisha pia. Kama kitu sio muhimu sana basi usikigharamie. Punguza matumizi yote ambayo ni ya anasa tu na sio kwa ukuaji wa biashara. Katika kupunguza gharama zako za biashara na maisha, jijengee nidhamu nzuri sana ya fedha. Usitumie fedha kiholela tu, kuwa na mahesabu na sababu kwa nini umetumia fedha fulani, hasa kwa matumizi ambayo sio ya kawaida.

4. Angalia watu ambao unaweza kushirikiana nao
Baada ya kuiendesha biashara yako vizuri na ukaona inaenda kwa faida, unaweza kuangalia watu ambao unaweza kushirikiana nao kwenye biashara hiyo. Kuna watu wengi ambao wanaweza kuwa na mtaji lakini hawana muda wa kufanya biashara. Lakini pia watu hawa wanataka mtu ambaye wanaweza kumwamini. Hivyo kama unaweza kuaminika angalia watu unaoweza kushirikiana nao kibiashara. Andaa mpango mzuri ambao utamshawishi mtu ni jinsi gani yeye atafaidika kama atawekeza kiasi kidogo kwenye biashara yako. Ikiwa unaendesha biashara yako kitaalamu itakuwa rahisi zaidi kushawishi watu kushirikiana na wewe.

5. Rasimisha biashara yako ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata mkopo
Hata kama biashara yako ni ndogo kiasi gani, irasimishe. Iendeshe kisheria kwa kuwa na namba ya mlipa kodi na hata leseni pia. Hivi vitakuwezesha wewe kutambulika na taasisi za kifedha pale utakapohitaji msaada zaidi wa kifedha. Mkopo kwenye taasisi za kifedha ni chanzo muhimu ila usikimbilie kama bado hujaweza kuiendesha biashara yako kwa faida. Hakikisha umeiweka biashara yako vizuri kwanza na inajiendesha kwa faida ili unapochukua mkopo unajua unauweka wapi na kuendelea kupata faida zaidi.

Kuikuza biashara pale ambapo umeanza na mtaji kidogo ni kitu ambacho kinawezekana. Ila unahitaji kujitoa na kujenga nidhamu kubwa. Unahitaji kufanya kazi zaidi ya wafanyabiashara wengine, unahitaji kuwa mbunifu wa hali ya juu na pia unahitaji kujijengea uaminifu. Ukishajua wewe biashara yako ni ndogo na inahitaji kukua, basi hakikisha kila mara unaumiza akili yako ifikirie njia zaidi za kuikuza. Na kama utaweza kufanya hivi basi utaziona fursa nyingi zilizokuzunguka za kuikuza biashara yako.

Popular posts from this blog

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU” kama  ifuatavyo : SEHEMU  YA  PILI   YA  KITABU  “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU “ Wachawi   wakishindwa  kukutengenezea  kesi  kubwa  basi  waatakufunga  kwenye  kifungo  cha  mapenzi.  Katika  vifungo  vyote anavyo  fungwa  mwanadamu  hakuna  kifungo  kibaya  kama  kifungo  cha  mape

Faida nyingine za kula chungwa

Faida nyingine za kula chungwa Siku kadhaa zilizopita tuliangalia kwa uchache kuhusu faida za kula chungwa hivyo, pia siku ya leo naomba tuendelee kwa kuangalia faida nyingine za kula chungwa. 1. Ulaji wa machungwa husaidia kutibu mapafu. Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu. 2. Husaidia kuimarisha mifupa ya meno. Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno. 3. Husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini. Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake. 4. Hupunguza kupatwa magonjwa wa figo. Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaid

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi?

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi? Unafikili ni wazo zuri kuamka  saa 11 za asubuhi na kufanya mazoezi? Je, ingekuwa vipi kama ungetumia muda huo kulala? Wataalamu wa afya wanashauri kuwa binadamu kwa kwaida anapaswa kulala angalau masaa 7 wakati wa usiku ili kuupa mwili afya bora. Kulala kwa muda mfupi au masaa machache husababisha matatizo ya afya, ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, unyogovu, ugonjwa wa kisukari, na kupunguzwa kinga kukabiliana na chanjo. Ni vyema ukatumia muda wako vizuri mchana ili usiku ukapata muda mwafaka wa kuweza kuupumzisha mwili ili kuepukana na magonjwa hatari ya shinikizo la damu, kisukari na kupungua kwa kinga mwilini. Najua mazingira yetu waafrika ya kimaisha wakati mwingine yanachangamoto nyingi, lakini pale upatapo mwanya kidogo tu, basi utumie yani "kila penye tundu, penyeza lupia" au wawenzetu wazungu wanasema "one chance two goals".