Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2018

Onyo Zito Latolewa Kampeni za Uchaguzi Katika Jimbo la Nyalandu

Onyo Zito Latolewa Kampeni za Uchaguzi Katika Jimbo la Nyalandu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, ameonya kuwa watu watakaovuruga mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Singida Kaskazini, serikali itawashughulikia kwa mujibu wa sheria. Dk. Nchimbi alitoa onyo hilo katika Kijiji cha Mtinko Wilaya ya Singida Vijijini alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kwenye uzinduzi wa kampeni hizo. Alisisitiza kwamba ili watambue kuwa ni mtumishi aliyetumwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ajitokeze mtu yeyote na kuthubutu kuvuruga ratiba ya mikutano ya kampeni. Hata hivyo, aliwahakikishia wananchi kuwa mikutano ya kampeni itakuwa salama pamoja na uchaguzi huo kwani serikali imejipanga kikamilifu kudhibiti yeyote atakayeonekana anataka kuvuruga uchaguzi huo. “Na ole wake na atokee mtu yeyote yule mwingine atakaeingilia katika njia hii ya uchaguzi salama, amani na utulivu ndipo mtakapotambua kwamba nimetumwa

Tundu Lissu Kataja Kitu Ambacho Hatakisahau Tangu Apelekwe Nairobi

Tundu Lissu Kataja Kitu Ambacho Hatakisahau Tangu Apelekwe Nairobi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu amekiri kwamba hatakuja kusahau tukio la mkazi wa Iringa aliyekwenda hospitali Nairobui alikolazwa kwa ajili ya kumuombea ili apate kupona baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Lissu ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini, amedai kwamba mama huyo alimgusa sana kwa upendo aliouonyesha juu yake huku akizingatia kwamba ametokea mbali sana huku akionekana ni mtu wa hali ya chini. "Ukiwa mgonjwa kisha akaja mtu kukutembelea ni faraja sana. Nawashukuru maelfu ya watanzania na watu wote waliofika Nairobi kunijulia hali. Lakini sitakaa kuweza kumsahau mama mmoja aliyetoka Iringa kwa ajili ya kuja kuniombea," Lissu. Lissu ameongeza "Aliniambia Mheshimiwa nimetokea Iringa na mpaka nimefika hapa nimetumia siku tano. Nikamwambia mama asante niombee kisha akapiga magoti na kuniombea. Alinig

TRA Wakomaa na Askofu Kakobe.....Wadai Hawana muda wa Kubishana nae Zaidi ya Kuchunguza Utajiri wake

TRA Wakomaa na Askofu Kakobe.....Wadai Hawana muda wa Kubishana nae Zaidi ya Kuchunguza Utajiri wake Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imemuibukia kivingine, Askofu wa Kanisa la Full Gosper Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe, kuhusu utajiri alionao ikisema haina muda wa kulumbana naye, bali inatekeleza maelekezo ya Kamishna Mkuu. Aidha, mamlaka hiyo imesema haitaki kuwa kwenye malumbano na askofu huyo wakati ikiendelea na uchunguzi dhidi ya vitega uchumi vyake na kuangalia kama analipa kodi ya serikali. Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo, jana alisema maofisa wao wanaendelea kutekeleza tamko la Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere, la kuchunguza utajiri wa Askofu Kakobe. "Sisi (TRA) hatutaki kuwa kwenye malumbano na Kakoke, tulichosema tumeishia hapo. Alichosema Kamishna Mkuu tunaishia hapohapo, hatutakiwi kujibishana naye," Kayombo alisema. Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumam

Rais Magufuli Aomboleza Msiba Wa Mke Wa Naibu Waziri Kangi Lugola

Rais Magufuli Aomboleza Msiba Wa Mke Wa Naibu Waziri Kangi Lugola Mhe. Rais John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Alphaxard Lugola aliyefiwa na Mkewe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Kikosi cha Polisi Reli Tanzania.  Alifariki dunia jana tarehe 01 Januari 2018 katika hospitali ya Rabinisia Memorial Tegeta Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Msiba upo Gerezani Railway Club Jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.  

Spika Ndugai Amjibu Tundu Lissu

Spika Ndugai Amjibu Tundu Lissu Spika  wa Bunge Job Ndugai amefunguka na kusema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na familia yake hawatambui kuwa Serikali hasa Bunge limeanza kufanya mazungumzo na watu wanaotaka kumsafirisha kwenda nje kwa matibabu zaidi. Ndugai amedai anatambua kuwa Tundu Lissu atasafirishwa na kwenda kwa matibabu zaidi nje ya Kenya ingawa hajajua ni lini lakini amesema kuwa watu ambao wamepanga kumpeleka huko kwenye matibabu tayari walishamtafuta yeye na kusema watashirikiana nao katika masuala ya matibabu. "Ni kweli kwamba atapelekwa nje zaidi ya Nairobi ila bado sijui mpaka sasa ni lini kwa kuwa sijajua tarehe bado japo nadhani itakuwa hivi karibuni na wale wanaomgharamia kumpeleka nje wameshawasiliana na mimi na hakika familia ya Lissu hata Tundu Lissu mwenyewe hajui hilo, anafikiri ni wao peke yao lakini najua na walishafika kwangu na kusema watagharamia wao" alisema Ndugai Spika Ndugai alizidi kueleza kuw

Mh. Sugu aitwa Polisi kuhojiwa

Mh. Sugu aitwa Polisi kuhojiwa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu' na mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameitwa Polisi wakisema hawajui sababu ya wito huo. Hata hivyo, wawili hao wamesema wanahisi wito huo unatokana na mkutano wa hadhara alioitisha Sugu katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Akizungumza kwa simu leo Jumanne Januari 2,2018 Sugu amesema juzi jioni alipigiwa simu na  Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) kwamba pamoja na Masonga wafike jana ofisini kwake kuzungumza lakini alimueleza ilikuwa ni siku ya sikukuu hivyo itakuwa ngumu kwenda, hivyo walikubaliana wafike leo. "Walinipigia simu juzi jioni wakinitaka mimi na Masonga twende makao makuu ya polisi jana, nikawaambia itakuwa ni sikukuu hivyo tukakubaliana leo asubuhi, hivyo tupo njiani tunaelekea huko kuitika wito. Sijajua sababu, lakini nadhani ni uchochezi," amesema Sugu. Masonga amesema a

Tuhuma Mpya Za Tundu Lissu kwa Spika na Bunge

Tuhuma Mpya Za Tundu Lissu kwa Spika na Bunge Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ambaye yuko Nairobi nchini Kenya kwa matibabu, amesema kuwa Bunge la Tanzania halijatoa pesa yoyote kugharamia matibabu yake, kauli ambayo inatofautiana na Bunge ambayo ilisema imetuma fedha. Akizungumza kwenye mahojiano na moja ya television za hapa nchini, Tundu Lissu amesema hakuna pesa yoyote iliyotolewa na Bunge wala serikali, kwa ajili ya matibabu yake huko nchini Kenya. "Bunge halijatoa hata senti moja ya matibabu yangu, serikali haijatoa hata senti moja, familia yangu na ndugu zangu inasema mbunge amelazwa tangu Septemba 7, Spika wa Bunge hajaenda, Naibu Spika wa Bunge hajaenda, Katibu wa Bunge hajaenda, Tume ya huduma za Bunge haijaja, haijatoa hata senti 10 kugharamia matibabu yangu", amesema Tundu Lissu. Mnamo Septemba 7, 2017, Mbunge Tundu Lisu alipigwa risasi na watu wasiojulikana, tukio ambalo limemfanya alazwe hospitali kwa

Halima Mdee Awapa Ujumbe Mzito Watanzania

Halima Mdee Awapa Ujumbe Mzito Watanzania Mbunge wa Kawe, Halima James Mdee amewataka watanzania kutumia mwaka mpya wa 2018 kutafakari kwa kina mwelekeo wa Tanzania na kuchukua hatua pale panapohitaji kurekebishwa. Mh. Mdee ameyasema hayo kwenye salamu za Mwaka Mpya alizozitoa kupitia mtandao wake wa kijamii ambapo amesema kwamba hakuna mwenye wajibu wa ziada bali watanzania. "Heri ya Mwaka Mpya Watanzania we zangu. Mwaka 2018 tuutumie vyema kutafakari kwa kina mwelekeo wa Taifa letu na tuchukue hatua kila mmoja kwa nafasi yake pale ambapo tunadhani panahitaji kurekebishwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Hakuna mwenye wajibu wa ziada , Tanzania ni yetu!" Halima Mdee.

Polepole: Lema 2020 utalisikia hewani tu jimbo la Arusha Mjini

Polepole: Lema 2020 utalisikia hewani tu jimbo la Arusha Mjini Katibu wa Itikadi na Uenezi  wa  Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amemtahadharisha Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwakumwambia kuwa  kipindi hiki ni cha mwisho kuongoza Jimbo hilo la Arusha Mjini. Hayo yamekuja mara baada ya Mbunge huyo kupitia kurasa zake za twitter kujibizana huku Lema akionyesha kumhoji Polepole kama familia yake huwa inamuelewa kweli anachokizungumza. “Term ya mwisho Arusha, tunataka Mbunge wa Masuala na si wa Matukio, hata mkichezesha draft ili uende Hai, haitawezekana maana hata “fly to…” maji yako shingoni, na ukiamua kurudia kazi yako ya zamani. anko Siro is very serious,”ameandika Polepole

Mapato ya Korosho Mikoa Minne Yafikia Trilioni Moja

Mapato ya Korosho Mikoa Minne Yafikia Trilioni Moja MAPATO kutokana na mauzo ya korosho katika msimu wa 2017/2018 katika mikoa minne ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma yamepanda na kufikia sh. trilioni 1.08 ikilinganishwa na misimu miwili iliyopita. Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Bw. Hassan Jarufu alitoa taarifa hiyo Jumapili, Desemba 31, 2017 wakati akitoa ufafanuzi juu ya uzalishaji na mauzo ya zao la korosho nchini hadi kufikia mwisho wa mwaka 2017. “Ukiangalia msimu wa mwaka 2015/2016, utaona kuwa korosho zilizozalishwa zilikuwa kidogo zaidi. Msimu huo ziliuzwa kilo 155,244,645 zikiwa na thamani ya sh. 388,474,530,906.00 ikilinganisha na msimu wa 2016/2017 ambapo jumla ya kilo 265,237,845.00 ziliuzwa zikiwa na thamani ya sh. 871,462,989,284.00,” alisema. Alisema katika minada 10 ya msimu wa 2017/2018, mauzo ya korosho yamefikia kilo 285,828,205 zenye thamani ya sh. 1,082,200,383,581.00. “Mnada wa 10 ulikuwa tarehe 21 Desemba, 20

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Rais Kabila wa DRC kumtaka ajiuzulu

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Rais Kabila wa DRC kumtaka ajiuzulu Umoja wa Mataifa umemwambia Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila kutimiza ahadi aliyoiweka ya kuachia madaraka na kupisha uongozi mwingine kuiongoza nchi hiyo hususani wakati huu ambapo nchi hiyo imejaa migomo na maandamano ya kushinikiza ajiuzulu. Rais Kabila mwenye miaka 46, ameiongoza DRC kwa miaka 17 na msimu wake wa mwisho wa uongozi uliisha tangu December 31, 2016 na akatakiwa aachie ngazi lakini uchaguzi wa kupata Rais na viongoi wapya umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara. Suala hili limesababisha vurugu na maandamano ya raia wa DRC ambao hata hivyo inaelezwa kuwa wamekuwa wakipigwa na askari polisi jamabo ambalo kwenye taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa December 31, 2017 imelaani vikali vitendo hivyo hususani Jijini Kinshasa ambapo watu watano waliuawa na polisi siku hiyo vya Jumapili kwenye maandamano.

Mjerumani auawa kwa kisu Zanzibar....Wanawake Wanne Watiwa Mbaroni

Mjerumani auawa kwa kisu Zanzibar....Wanawake Wanne Watiwa Mbaroni Raia wa Ujerumani Gerd Winkdl (60), amefariki dunia Zanzibar akidaiwa kuchomwa kisu na marafiki zake wa kike kutokana na wivu wa kimapenzi huku wanawake wanne wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na kifo hicho. Tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya Shangani Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Hassan Nassir Ali, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 9:30 usiku baada ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2018 akiwa na marafiki zake hao. Alisema kabla ya kukutwa na umauti, Winkdl akiwa na marafiki zake wanne ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi, waligombana na baadaye ugomvi huo kusababisha kuchomwa kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake. Kamanda Ali alisema watuhumiwa hao wanne ambao wote ni wanawake, raia wa Tanzania na Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikiliwa kwa ajili ya kuwahoji na kukamilisha taratibu za kiuchunguzi.

Breaking News: Televisheni 5 Nchini Zapigwa Faini na TCRA kwa Kukiuka Maadili ya Utangazaji

Breaking News: Televisheni 5 Nchini Zapigwa Faini na TCRA kwa Kukiuka Maadili ya Utangazaji Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, imevipiga faini vituo vitano vya Televisheni  kwa makosa ya ukiukwaji wa taratibu za kutangaza taarifa ya habari hapa nchini. Adhabu hiyo imetangazwa leo na Makamu mwenyekiti wa kamati   ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) , Joseph Mapunda Kituo cha runinga cha EATV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 15, kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30, na kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 6. Aidha, TCRA imekitoza faini ya TZS milioni 15 kituo cha Runinga cha Channel ten, kwa makosa ya kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi, kutangaza habari za uchochezi, na kutozingatia mizania. Pia kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kuanzia leo. Kituo cha runinga cha

Breaking News: Babu Seya na Mwanaye Watinga Ikulu Kumshukuru Rais Magufuli kwa Kuwasamehe

Breaking News: Babu Seya na Mwanaye Watinga Ikulu Kumshukuru Rais Magufuli kwa Kuwasamehe Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza walipofika Ikulu jijini Dar Leo Januari 2, 2018 kumshukuru Rais Magufuli kwa msamaha wake aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa ameshikana Mikono na kuomba dua na Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza walipofika Ikulu jijini Dar Leo Januari 2, 2018 kumshukuru kwa msamaha wake aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia

Waziri Mkuu: Vijana Jitokezeni Mlime Korosho

Waziri Mkuu: Vijana Jitokezeni Mlime Korosho WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wanaioishi kwenye mikoa ambayo zao la korosho linastawi wachangamkie kilimo cha zao hilo kwa sababu lina fursa nyingi. “Mahitaji ya korosho ni makubwa duniani, korosho zinatumika mahotelini na kwenye mikutano mikubwa, zinatumika kwenye ndege, kwa hiyo bei yake lazima iwe kubwa,” alisema. Ametoa wito huo Jumapili, Desemba 31, 2017 wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni: “Korosho ni dhahabu ya kijani, tuitunze, itutunze”. Waziri Mkuu alisema anaamini kuwa kijana yoyote mwenye nguvu ya kufanya kazi hawezi kushindwa kulima zao hilo kwa sababu halihitaji uangalizi mkubwa. “Kijana yeyote anaweza kulima zao hili kwa sababu ekari moja ina miche 37 hadi 40. Kuna mtu atashindwa kuangalia miche 37 hadi ikue?” aliuliza. Waziri Mkuu alisema kilimo cha ko

Waziri Mkuu Atoa Kadi Za CHF Kwa Wazee 4,000

Waziri Mkuu Atoa Kadi Za CHF Kwa Wazee 4,000 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kumudu gharama za matibabu bila kulazimika kuwa fedha taslimu. Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Ruangwa na vijiji vya jirani katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CWT, mjini Ruangwa, mkoani Lindi. “Leo hii nimetoa kadi za CHF kwa wazee 4,000 wa wilaya hii. Ninaishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kutenga fedha na kuwalipia wazee hawa ili wanufaike na bima hii ya afya kama ambavyo imeelekezwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi.” “Ninatoa wito kwa wananchi wengine walipie sh. 15,000 kwa mwaka ili wapatiwe kadi kwa ajili ya watu sita wa familia zao; yaani mhusika, mwenza wake na watoto wanne. Bima hii inasaidia kwa vile unapata matibabu hata kama huna fedha taslimu,” alisema. Waziri Mkuu alikabidhi kadi kwa Mzee Is