Halima Mdee Awapa Ujumbe Mzito Watanzania
Mbunge wa Kawe, Halima James Mdee amewataka watanzania kutumia mwaka mpya wa 2018 kutafakari kwa kina mwelekeo wa Tanzania na kuchukua hatua pale panapohitaji kurekebishwa.
Mh. Mdee ameyasema hayo kwenye salamu za Mwaka Mpya alizozitoa kupitia mtandao wake wa kijamii ambapo amesema kwamba hakuna mwenye wajibu wa ziada bali watanzania.
"Heri ya Mwaka Mpya Watanzania we zangu. Mwaka 2018 tuutumie vyema kutafakari kwa kina mwelekeo wa Taifa letu na tuchukue hatua kila mmoja kwa nafasi yake pale ambapo tunadhani panahitaji kurekebishwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Hakuna mwenye wajibu wa ziada , Tanzania ni yetu!" Halima Mdee.