Skip to main content

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti

WAKATI bei ya unga wa sembe ikipanda mpaka kufikia kuuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500 kwa kilo, ile ya mfuko wa saruji wenye uzito wa kilo 50 imeshuka hadi sh. 9,000, sawa na Sh. 180 kwa kilo.

Katika masoko na maduka mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambayo Nipashe ilitembelea jana, bei ya sembe ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi hicho kwa rejareja huku wauzaji wa jumla wakiuza kiroba cha kilo 50 kwa kati ya sh.100,000 na sh.98,000.

Ibrahim Omary, mfanyabiashara wa Kariakoo alisema anauza unga wa sembe kwa Sh. 2,400 kwa kuwa hununua kwa bei kubwa kutoka kwa wazalishaji.

Alisema kampuni inayojulikana kwa jina la Mkulima huwauzia unga huo kwa Sh. 98,000 na Mama Neema huwauzia kwa sh. 100,000 kwa kiroba cha kilo 50.

Kwenye baadhi ya maduka ya kula ya Kinondoni, unga umekuwa ukiuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500. Tandika bei ya wastani ni Sh. 2,200, Mwenge Sh. 2,400, Kimara sh. 2,500 na Yombo Vituka sh. 2,200.

Nipashe ilitembelea mashine zinazozalisha sembe katika eneo la Tandale ambako bei ya jumla kwa mfuko wa kilo 50 ni kati ya Sh. 92,000 na Sh. 94,000 huku kilo ya mahindi ikiuzwa kati ya sh. 1,300 na 1,500.

Baadhi ya wateja walikuwa wakilalamika gharama hizo za unga huku wakieleza kuwa kwa sasa wamepunguza matumizi ya unga wa sembe na kuamua kutumia mchele.

Janeth Masawe, mkazi wa Mwenge alisema kwa sasa wamekuwa hawanunui unga wa sembe mara kwa mara kama ilivyokuwa zamani kwa kuwa sembe inazidi gharama ya mchele.

“Bora ninunue mchele... maana naweza kupata mchele kwa sh. 1,800 kwa kilo lakini unga wa sembe ni mpaka niwe na sh. 2,400,” alisema.

Kupanda kwa bei ya unga kumetokana na kupanda kwa bei ya mahindi kulikosababishwa na uhaba wa chakula hicho kutokana na ukame ambao ulikumba maeneo mengi ya nchi kabla ya mvua za masika zilizoanza mwezi uliopita.

Gunia moja la mahindi linauzwa kwa bei ya wastani wa Sh. 112,000 kwa sasa katika maeneo ambayo ni chanzo kikuu cha zao hilo, uchunguzi wa Nipashe umeonyesha.

TWIGA JENGA
Tangazo kwa wafanyakazi wote lililotolewa na kiwanda cha saruji cha Twiga Jumatano wiki hii, lilibainisha kuwa mauzo ya mfuko mmoja wa Twiga Jenga kuwa sh. 9,000, Twiga Extra sh. 9,500 na sh. 10,000 kwa Twiga Plus.

Tagazo hilo lililoandikwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Jesse Shuma, lilitaka kuwaarifu wafanyakazi hao kuwa saruji "inauzwa kiurahisi na kwa bei nafuu katika eneo letu la maegesho ya magari lililoko Kizuga, nje ya kiwanda."

"Tafadhali mjulishe mfanyakazi mwenzako, rafiki, ndugu na jamaa.

"Wote mnakaribishwa."

Kuporomoka kwa bei ya saruji ambayo miaka miwili iliyopita ilikuwa ikiuzwa sh. 15,000 kwa mfuko wa kilo 50, kwa kiasi kikubwa kumetokana na ufunguzi wa Kiwanda cha Dangote mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa tovuti ya serikali ya mkoa wa Mtwara, "kiwanda hiki ni kikubwa kuliko vyote katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati" na kina uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu za saruji kwa mwaka.

Kilianza uzalishaji rasmi Septemba, mwaka jana, baada ya uwekezaji wa dola za Marekani milioni 500 (sawa na Sh. trilioni 1.1).

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla...