Tuhuma Mpya Za Tundu Lissu kwa Spika na Bunge
Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ambaye yuko Nairobi nchini Kenya kwa matibabu, amesema kuwa Bunge la Tanzania halijatoa pesa yoyote kugharamia matibabu yake, kauli ambayo inatofautiana na Bunge ambayo ilisema imetuma fedha.
Akizungumza kwenye mahojiano na moja ya television za hapa nchini, Tundu Lissu amesema hakuna pesa yoyote iliyotolewa na Bunge wala serikali, kwa ajili ya matibabu yake huko nchini Kenya.
"Bunge halijatoa hata senti moja ya matibabu yangu, serikali haijatoa hata senti moja, familia yangu na ndugu zangu inasema mbunge amelazwa tangu Septemba 7, Spika wa Bunge hajaenda, Naibu Spika wa Bunge hajaenda, Katibu wa Bunge hajaenda, Tume ya huduma za Bunge haijaja, haijatoa hata senti 10 kugharamia matibabu yangu", amesema Tundu Lissu.
Mnamo Septemba 7, 2017, Mbunge Tundu Lisu alipigwa risasi na watu wasiojulikana, tukio ambalo limemfanya alazwe hospitali kwa zaidi ya miezi mitatu mpaka sasa akipatiwa matibabu, na Bunge lilitoa taarifa kuwa limetuma pesa za matibabu, ambazo hospitali ambayo Tundu Lissu yupo akitibiwa ilikiri kuzipokea kwenye acount yake.