Skip to main content

CHADEMA Wamjibu Lawrence Masha

CHADEMA Wamjibu Lawrence Masha


Baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao baada ya mwanachama wao Lawrence Masha kujivua uanachama na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa kama sababu za kujivua kwake.

Kwenye kurasa zao mbali mbali za mitandao ya kijamii Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika ujumbe akisema safari ya kupigania usawa na haki ni safari ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo ni aibu kwani kuna wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa safari.

“Lawrence Masha , struggle ya kupigania usawa,haki na demokrasia, ni safari ndefu na ngumu ,wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na wanawake imara wanaendelea na safari,sio uamuzi mbaya uliochukua ila ni uamuzi wa aibu . Utajua baadaye na sio sasa”, ameandika Godbless Lema.

Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo wanaheshimu mamuzi yake.

“Tunaojua sababu za Masha kutoka CHADEMA zile kwenye barua yake tunajua ni danganya toto, tunajua sababu na tunaziheshimu. Kuthibitisha kuwa CHADEMA imejipanga kuingia ikulu, angalia takwimu za ushindi wa madiwani na wabunge nchini kuanzia 1995 hadi sasa. Ikulu ni suala la muda, tena si mrefu”, ameandika Joshua Nasari.

Pia Katibu Mkuu wa chama hiko Vicent Mashinji aesema Masha kuondoka CHADEMA ni haki yake kisheria, lakini ni vyema akaweka wazi ukweli wa sababu za yeye kuondoka.

“Mheshimiwa Masha ana haki kisheria, namtakia heri, lakini lazima auambie umma nini hasa kilichotokea”, ameandika Mashinji.

Lawrence Masha hapo jana ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA akisema chama hiko hakina malengo ya kushika dola, kama ambavyo malengo ya vyama vya upinzani huwa.

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ ...

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti WAKATI bei ya unga wa sembe ikipanda mpaka kufikia kuuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500 kwa kilo, ile ya mfuko wa saruji wenye uzito wa kilo 50 imeshuka hadi sh. 9,000, sawa na Sh. 180 kwa kilo. Katika masoko na maduka mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambayo Nipashe ilitembelea jana, bei ya sembe ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi hicho kwa rejareja huku wauzaji wa jumla wakiuza kiroba cha kilo 50 kwa kati ya sh.100,000 na sh.98,000. Ibrahim Omary, mfanyabiashara wa Kariakoo alisema anauza unga wa sembe kwa Sh. 2,400 kwa kuwa hununua kwa bei kubwa kutoka kwa wazalishaji. Alisema kampuni inayojulikana kwa jina la Mkulima huwauzia unga huo kwa Sh. 98,000 na Mama Neema huwauzia kwa sh. 100,000 kwa kiroba cha kilo 50. Kwenye baadhi ya maduka ya kula ya Kinondoni, unga umekuwa ukiuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500. Tandika bei ya wastani ni Sh. 2,200, Mwenge Sh. 2,400, Kimara sh. 2,500 na Yombo Vituka sh. 2,200. ...