Skip to main content

Pichaz + Video: Watu Wafariki, Wanasa Kwenye Jengo Linalowaka Moto London

Pichaz + Video: Watu Wafariki, Wanasa Kwenye Jengo Linalowaka Moto London

 Jengo hilo liliteketea kutokana na kile kilichodaiwa friji bovu, japokuwa kikosi cha zimamoto hakijathibitisha ripoti hiyo.

WATU kadhaa wamethibitika kufariki baada ya moto mkubwa kutokea usiku wa manane katika jengo moja magharibi mwa Jiji la  London, Uingereza, ambao unasemekana ulisababishwa na friji mbovu.

Familia zinazokaa katika jengo hilo, zilisikika zikipiga kelele kuomba msaada, wakati wengine wanenasa sehemu mbalimbali ndani ya jengo hilo lenye ghorofa 27 linaloteketea na kutishia kuanguka.

Zaidi ya wakati 600 jengoni humo walijaribu kujiokoa ambapo huduma za magari ya wagonjwa zimesema watu 50 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali za jiji hilo.

Habari zaidi zinasema watu walionasa ndani yake walifunga mashuka yao na kuyatumia kama kamba na kujirusha kupitia madirishani ili kujiokoa.

Mashuhuda wamesema waliwaona watu wengine wakiruka kutoka katika ghorofa ya 15 ili kujiokoa na wengi wao wakipiga kelele huku vikosi vya waokoaji vikiwatoa wengine katika miali ya moto.

Wakazi zaidi ya 600 waliokuwa wakiishi katika jengo hilo walijaribu kujiokoa kwa njia mbalimbali.
Tukio hilo la moto limeelezwa kuwa ni kubwa zaidi ambalo halijawahi kutokea jijini London katika miaka ipatayo 30 iliyopita. 





















Tazama video hapa chini:


Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti WAKATI bei ya unga wa sembe ikipanda mpaka kufikia kuuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500 kwa kilo, ile ya mfuko wa saruji wenye uzito wa kilo 50 imeshuka hadi sh. 9,000, sawa na Sh. 180 kwa kilo. Katika masoko na maduka mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambayo Nipashe ilitembelea jana, bei ya sembe ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi hicho kwa rejareja huku wauzaji wa jumla wakiuza kiroba cha kilo 50 kwa kati ya sh.100,000 na sh.98,000. Ibrahim Omary, mfanyabiashara wa Kariakoo alisema anauza unga wa sembe kwa Sh. 2,400 kwa kuwa hununua kwa bei kubwa kutoka kwa wazalishaji. Alisema kampuni inayojulikana kwa jina la Mkulima huwauzia unga huo kwa Sh. 98,000 na Mama Neema huwauzia kwa sh. 100,000 kwa kiroba cha kilo 50. Kwenye baadhi ya maduka ya kula ya Kinondoni, unga umekuwa ukiuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500. Tandika bei ya wastani ni Sh. 2,200, Mwenge Sh. 2,400, Kimara sh. 2,500 na Yombo Vituka sh. 2,200. ...

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla...