Skip to main content

Shahidi ( OCCID) Asimulia Jinsi Alivyomkamata Tundu Lissu

Shahidi ( OCCID) Asimulia Jinsi Alivyomkamata Tundu Lissu



Mkuu  wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu (ZCO), Camilius Wambura kumtaka afanye hivyo.

Mgonja ambaye ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, shahidi huyo alidai kuwa Juni 28, mwaka jana, Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama hiyo.

Alidai kuwa Juni 29 mwaka jana saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni, ambapo alimkamata na kumfikisha katika ofisi ya ZCO na kumkabidhi.

“Nilipewa amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamlaka hayo bila kuwa na hati ya ukamataji naweza kukukamata; kwani makosa yoyote ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati hiyo,” alidai Mhonja.

Pia alidai kuwa kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa, ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.

Katika mashitaka yake, Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, ‘huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu’. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

Popular posts from this blog

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia.  Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katika miradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato.  Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake k ij iji cha  Itiry o   kusherekea sikukuu ya Pasaka.  Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ...

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4 Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu. Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo  Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni maalum kwa ajili ya bajeti. Ratiba hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne, ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25. Mbali na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017 ==>Itazame hapa ratiba kamili ya mkutano huu...

Hatua 5 za kutatua tatizo lolote unalokutana nalo

Hatua 5 za kutatua tatizo lolote unalokutana nalo Hatua ya kwanza; jua kwa undani tatizo ni nini.  Najua utashangaa lakini ukweli ni kwamba wengi ambao wanakuwa na matatizo huwa hawajui tatizo hasa walilonalo ni nini. Na hivyo wanapokazana kulitatua wanashindwa, kwa sababu kama hujajua kiini cha tatizo huwezi kulitatua. Mara nyingi watu wamekuwa wakiangalia madhara ya tatizo, badala ya kuangalia chanzo kikuu cha tatizo. Huwezi kutibu tatizo kwa kutibu madhara, badala yake unahitaji kuzama ndani na kujua chanzo hasa cha tatizo ni nini. Na njia ya uhakika ya kufikia hilo ni kuuliza swali moja muhimu sana, KWA NINI. Uliza swali hili mara tano, yaani uliza kwa hatua tano. Kwa mfano kama tatizo lako ni kipato kidogo kwenye biashara yako, jiulize kwa nini kipato ni kidogo, jibu linaweza kuwa wateja ni wachache, jiulize tena kwa nini wateja ni wachache, hapo utapata majibu mengine, kwa kila jibu jiulize tena kwa nini? Mpaka utafika mahali na kuona hiki ndio kiini kikuu c...