Ndoa yampapresha Shilole
WAKATI akisubiri kufunga ndoa na mchumba wake, Uchebe Ashraf siku chache zijazo, staa wa muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ yu gonjwagonjwa, Ijumaa Wikienda limedokezwa.
Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao kilieleza kuwa, ndoa hiyo inampa presha Shilole kwani alizidiwa hivi karibuni na kwenda kulazwa hospitali licha ya kwamba kwa sasa anaendelea vizuri tofauti na awali.
“Unajua Shilole anatarajia kufunga ndoa na Uchebe hivi karibuni, kwa hiyo ana presha ya ndoa na ukizingatia na watu walivyozusha kuwa amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda ndiyo wakamchanganya kabisa,” kilidai chanzo hicho.
Ili kuujua ukweli wa habari hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Shilole baada ya kuona picha alizosambaza mchumba wake Uchebe zikimuonesha mwanamama huyo akiwa amelazwa hospitalini ambapo alikiri kuzidiwa lakini akasema presha ya ndoa bali ni malaria.
“Jamani nililazwa hospitali kwa Dokta Mvungi kwa sababu nina malaria kali. Nilikuwa hoi, nikawekewa dripu, lakini kwa sasa ninaendelea vizuri na nimetoka hospitali,” alisema Shilole kwa sauti ya unyonge.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps