Polepole amesema Chama chake hakitampokea Mtu adi afuate taratibu
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) hakitampokea yeyote anayetaka kurudi ndani ya chama hicho bila kufuata utaratibu. Kauli hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni(CUF), Maulid Said Abdallah Mtulia kutangaza kujiuzulu nafasi zake zote za uongozi alizokuwa akizishikilia kwenda CCM
Polepole aliyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi wa CCM mkoa wa Mara katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama.
“Ameamua kule aliko haoni itikadi,haoni siasa, haoni mwelekeo, Chama kina baba wawili huwezi kuwa na nyumba ina baba wawili alafu utasikiliza watoto watamsikiliza nani, basi amehama,” alisema Polepole.
“Sasa mimi niko hapa Musoma mimi nitumie fursa hii anayemuunga mkono ni Rais wetu ambaye ni mwana CCM kwelikweli na ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ikimpendeza afuate utaratibu akiona mazuri ya Rais yule asione vinaelea kwa mazuri yale asione vimeshushwa vimeundwa na wanaounda mambo mazuri ya Magufuli ni Chama cha Mapinduzi.”
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps