Skip to main content

Aingia matatani baada ya kupulizia wenzake kemikali usoni

Aingia matatani baada ya kupulizia wenzake kemikali usoni


MADALALI wanne wa madini ya Tanzanite (mawe), wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaumiza macho kwa kemikali aina ya ‘pepper spray’ baada ya kutofautiana malipo na madalali wenzao waliowauzia madini hayo.

Habari kutoka polisi zilithibitisha jana kuwashikilia madalali hao, Schola Mwanga, Margareth Mushi, Sued Mwanga na Dorice Mushi, kwa tuhuma za kufanya kitendo hicho.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo hakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi zaidi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Mount Meru, Dk. Jackline Urio, alithibitisha kupokea wagonjwa watano ambao alisema uchunguzi unaendelea kujua walimwagiwa aina gani ya kemikali.

Alisema kutokana na hali zao, wagonjwa hao walitarajiwa kuhamishiwa Hospitali ya Rufani ya KCMC ya mkoani Kilimanjaro, jana.

Alisema waliojeruhiwa walikuwa katika biashara ya madini na wakaletwa hapa wakilalamika macho yanauma, wakapewa huduma ya kwanza ya kuwaosha macho kwa kushauriana na madaktari bingwa wa macho wa Dar es Salaam.

Aliwataja wagonjwa hao kuwa ni Sabas Laizer, Lucas Soto, George Nyakila, Moringe Mollel na Ngalama Mapena.

Alisema watu hao walidai kumwagiwa ‘spray’ kwenye macho, majira ya saa 10 na walianza kufikishwa hospitalini hapo mmoja mmoja kuanzia saa 12 jioni.

"Lakini kwa sasa tunawahamishia hospitali ya KCMC kwa sababu kule kuna madaktari bingwa wa macho, watachunguzwa vizuri kujua madhara waliyopata," alisema.

Wakizungumzia tukio hilo lililotokea mtaa wa Pangani jijini hapa, baadhi ya watu walioshuhudia, walidai madalali hao walitaka walipwe fedha (kamisheni) ya kuwauzia mawe hayo.

Lakili walisema madalali waliopewa mawe hayo kuuza walishindwa kuwapa fedha hizo kwa kile walichodai walikuwa bado hawajalipwa.

Walisema hali hiyo ilizua kutoelewana kati yao kiasi cha kuzua ugomvi na ndipo dalali mmoja alipoingia ndani ya gari na kuchukua ‘pepper spray’ na kuwapulizia usoni.

“Pepper spray’ ni aina ya kemikali inayowekwa katika kopo maalum mithili ya dawa ya mbu na ikipulizwa usoni kwa mtu inaumiza macho yake na kuyafanya yasione kwa muda.

Katibu wa Chama cha Madakali mkoani hapa, Noel Olovaroya, alisema tukio hilo lilitokea baada ya kutofautiana katika masuala ya biashara.

Alishukuru daktari bingwa wa hospitali hiyo kwa kuwashughulikia vizuri wagonjwa hao na kuomba serikali kuongeza madaktari wa macho katika hospitali hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya madalali wenzake, waliojeruhiwa, Ngalama Mapena ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Madini, alisema chanzo cha tukio hilo ni yeye aliuziwa madini ya Tanzanite na dalali mmoja kwa Sh milioni 3.2 na makubaliano yalikuwa angemlipa kesho yake (juzi)  ambayo ndio siku ya tukio.

"Lakini nikiwa pale baada ya kujibu hivyo nikaona gari RAV 4 rangi nyeusi, wakashuka wanawake wawili ambapo mmoja namfahamu akanipulizia kitu kama perfume usoni na huku akitukana na ghafla nikapoteza fahamu," alisema.
Alisema mwanamke huyo ni dalali mwenzake.

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ ...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...