Skip to main content

Mama, watoto wamwagiwa tindikali

Mama, watoto wamwagiwa tindikali


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, MOHAMED MPINGA.

VUMILIA Shengema (31) na watoto wake wawili wamemwagiwa tindikali wakati wakitokea dukani kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamsaka mtuhumiwa huyo, Emmy Kyando (40, mkazi wa Sai jijini Mbeya ambaye aliwafanyia kitendo hicho cha kinyama watu hao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga, aliwataja wengine waliomwagiwa tindikali kuwa ni Loveness John (11), mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Sinde na  Nancy Peter (5), wakazi wa Mtaa wa Mwanshinga, Kata ya Manga jijini Mbeya.

Walimwagiwa na kujeruhiwa na tindikali hiyo usoni, kifuani na mikononi Julai 19, mwaka huu saa tatu usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mpinga alisema Emmy anadaiwa  kufanya kitendo hicho kutokana na wivu wa kimapenzi kwa kuwa ni mke mwenza  wa mwathirika.

Mpinga alifafanua kuwa baada ya mtuhumiwa kufanya kitendo hicho alikimbia  kusikojulikana na wasamaria wema waliwakuta waathirika wakiwa katika hali mbaya na kuwapeleka katika Hospitali ya Rufani ya Mbeya kwa ajili ya kupata matibabu.

Kamanda Mpinga alieleza kuwa juhudi za kumtafuta mtuhumiwa  kwa kushirikiana na mume wa muathirika huyo  aliyefahamika kwa jina la Lausi Kidagile ambaye naye ni mkazi wa Sae zinaendelea.

 “Jeshi la Polisi linalaani vikali kitendo hicho na tunaomba mwananchi yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha  kumkamata mtuhumiwa atupatie ili hatua za kisheria zichukuliwe,” alisema Kamanda Mpinga.

Akizungumza na Nipashe kwa taabu akiwa wadi namba mbili katika Hospitali ya Rufani Kanda ya Mbeya, muathirika wa tukio hilo, Vumilia Shangema, alisema mtuhumiwa alikuwa akimtolea lugha za vitisho mara kwa mara na aliahidi kuwa kuna siku atamjeruhi.

 “Nikiwa njiani  na wanangu ghafla nikaona mwanamke mmoja niliyemfahamu kwa jina la Emmy akinimwagia kitu usoni na sikuweza kuona tena, lakini nikakumbuka kuwa Emmy  aliwahi kuniambia kuwa atanifanyizia huku akinitolea vitisho vikali vilivyotishia usalama wa maisha yangu,” alisema  Shangema.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufani Kanda ya Mbeya, Goodlove Mbwanji, alithibitisha kuwapokea wagonjwa katika hali mbaya hususani mama wa watoto Shangema, akiwa ameharibika usoni na macho kutokuona kabisa huku mtoto Loveness akiendelea kupata matibabu na afya yake kuimarika pamoja na Nancy ambaye alitibiwa na kuruhusiwa.

Mbwanji alisema wanaendelea na matibabu kwa mama huyo na kwamba idara ya upasuaji pamoja na madaktari wengine bingwa wamemuwekea uangalizi mzuri ili apate matibabu stahiki.

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ ...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...