Skip to main content

Lissu aachiwa kwa dhamana

Lissu aachiwa kwa dhamana




Lissu akipelekwa mahakamani.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini, Tundu Lissu mapema leo asubuhi.

Lissu ametakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja ataweka bondi ya dhamana ya shilingi milioni 10 huku akiwekewa zuio la kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali maalum cha mahakama.
Aidha kesi yake imepangwa kusikilizwa Agosti 24 mwaka huu baada ya wadhamini wake kukamilisha taratibu zote za kumdhamini.

Tundu  Lissu ambaye alikamatwa Alhamisi, Julai 20 mwaka huu, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akijiandaa kuelekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki (EALS), alifikishwa Mahakamani hapo Jumatatu Julai 24 na kusomewa mashtaka  ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, kosa ambalo anadaiwa kulitenda Julai 17.

Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo ya kuleta chuki dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alipotakiwa kukubali ama kukataa  makosa hayo na Hakimu Mashauri, Lissu alisema kusema kweli haijawahi kuwa kosa la jinai. Mahakama ya Kisutu ilimnyima dhamana Tundu Lissu, kesi iliahirishwa hadi leo Julai 27, 2017 ambapo amepewa dhamana.

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ ...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...