Shilole afungukia mume atakae muoa
Zuwena Mohammed, ‘Shilole’.
MSANII wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed, ‘Shilole’ amefunguka kuwa mwanaume atakayemuoa atawashangaza wengi kwani atakuwa ni wa tofauti na watu wanavyodhani.
Akizun-gumza na Showbiz Xtra, Shilole alisema watu watashangaa kwa mwanaume atakayemuoa kwa sababu atakuwa ni mwanaume wa kawaida ila mwenye mapenzi ya dhati.
“Wengi watamshangaa sana mwanaume atakayekuja kunioa, kwa sababu atakuwa ni wa kawaida tofauti na niliowahi ku-date nao. Kikubwa ni kupata penzi la dhati na heshima, maisha yanasonga,” alisema.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps