Skip to main content

Umesikia alichokisema Shaffih Dauda Kuhusu Kukamatwa na TAKUKURU?

Umesikia alichokisema Shaffih Dauda Kuhusu Kukamatwa na TAKUKURU?


Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU kwa mwenyekiti wa chama cha mpira Dar es Salaam DRFA Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza.

Taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kukamatwa kwa watu hao zinadai ni viashiria vya rushwa na kuhusishwa na kampeni za chini kwa chini za uchaguzi Mkuu wa TFF, hivyo TAKUKURU ikawakamata kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa kadhaa kabala ya kuwaachia kwa dhamana.

Baada ya kurejea Dar es Salaam akitokea Mwanza Shaffih Dauda alipokuwa amekwenda na viongozi wa DRFA kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup kupitia Clouds FM ameeleza tukio la kukamatwa kwao lilivyokuwa ambalo linadaiwa kulenga kuwachafua katika uchaguzi Mkuu wa TFF.

“Nimehojiwa na TAKUKURU nikiwa Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup ambayo inaweza kuanza Mwezi wa 9, nilichogundua ni siasa za uchaguzi wa TFF, nilikutana na viongozi wa mpira Mwanza kwa ajili ya mipango ya Ndondo Cup Nilikua na viongozi wa DRFA tulioanzisha nao Ndondo Dar”: Shaffih Dauda

“Viongozi wa DRFA walikuwepo Mwanza kuwaeleza uzoefu viongozi Mwanza kabla hawajafanya na wao mwaka huu, baadhi ya watu na mawazo yao walitoa taarifa za uongo na kufanya mipango ya hovyo wakijua nafanya mipango ya uchaguzi, sigombei TFF kutaka cheo, nagombea kuleta mabadiliko kwenye soka, ndio maana napambana kupeleka Ndondo Cup kila sehemu

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ ...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...