Wauguzi kumnyima kura muhimu Kenyatta?
Nairobi, Kenya. Chama cha Wauguzi Kenya (NNAK) kimejiingiza katika siasa za uchaguzi baada ya kutoa tishio la “kuiaibisha” serikali ya Jubilee kwa madai ya kukawiza majadiliano kuhusu mzozo wa malipo yao.
Wafanyakazi hao wa idara ya afya wanautazama uchaguzi uliopangwa Agosti 8 kama kete yao wakisema kurejeshwa tena mamlakani kwa Rais Uhuru Kenyatta kutakuwa hatarini ikiwa madai yao hayatatekelezwa kwa wakati.
Mwenyekiti wa NNAK, Alfred Obengo alisema: “Tutakuwa na uchaguzi Agosti na sisi tuko 40,000 huku mshindi anatakiwa kupata asilimia 50 jumlisha moja. Idadi yetu haiwezi kupuuzwa.”
Aliongeza: “Kwa hiyo wakati wewe (Rais Uhuru) unaendelea na kampeni, usifikiri hata wakati mmoja kwamba kura za wauguzi si muhimu.”
Waguzi walipiga kambi katika viwanja vya Uhuru Park kulalamikia ukimya wa serikali katika mpango wa malipo ambao wanadai walifikia makubaliano na mwajiri wao.
Walivamia ofisi za Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) lakini haikusaidia kwani mwenyekiti wa tume hiyo Sarah Serem alisema alikuwa akisubiri mawasiliano kutoka kwa magavana.
Uhuru ahimiza kujitokeza
Naye akitambua tishio la kukosa kura 40,000 Rais Uhuru ameendelea kuwaambia wafuasi wake katika ngome zake muhimu kwamba matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 yataamuliwa na jinsi watakavyojitokeza kumpigia kura na si vinginevyo.
Rais aliwataka wasichezee suala hilo kamwe “kwa kuwa hali halisi ni kuwa mkijitokeza kwa wingi na mnipigie kura, basi huyu mtu wa kutusumbua (mpinzani wake Raila Odinga) kila uchao atakuwa amepata nauli ya kuelekea kwake nyumbani kustaafu.”
Akiwa katika Kaunti ya Murang’a, Uhuru alisema kuwa “kile sitachoka kuwaambia ni kuwa, kwa wakati huu nawahitaji kwa dhati. Kwa unyenyekevu nawapa tahadhari kuwa mkinichezea mzaha na kura zenu, basi mambo yataishia kwa sisi kushindwa. Mkijitokeza kwa wingi, mambo yatakuwa kwa manufaa yetu.”
Sababu za kususa mdahalo
Kuhusu kutohudhuria kwake mdahalo wa wagombea urais, Uhuru alisema: “Ratiba yangu ya kampeni na ambayo niliwasilisha kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka haikuorodhesha mdahalo huo kama jukwaa langu la kampeni.”
Alisema kuwa hadi sasa haoni ni kwa nini kumezuka gumzo kuhusu kususia kwake mdahalo huo ilihali haoni ulikuwa kwa manufaa gani akijitokeze katika ukumbi kujibizana na huyo mtu ambaye kila saa amejawa na uhasama na propaganda dhidi ya serikali yake.
Alisema kuwa kura haziko kwenye runinga na midahalo bali ziko katika mikono ya Wakenya ambao haja yao ni kusaidiwa kujiinua kimaisha “siyo katika safu ya kupewa maneno matupu ya majadiliano.”
Kwingineko Rais Kenyatta alisema aliamua kutoshiriki mdahalo huo kwa kuwa ulikuwa upotevu wa muda.
Kenyatta alisema asingeweza kufanya mdahalo na “mtu ambaye hana agenda kwa nchi hii.”

- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps