Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2017

EXCLUSIVE: Mashuhuda wasimulia tetemeko lilivyotokea Kagera usiku wa kuamkia leo

EXCLUSIVE: Mashuhuda wasimulia tetemeko lilivyotokea Kagera usiku wa kuamkia leo Habari nyingine kubwa kutokea Kagera usiku wa kuamkia April 30, 2017 ni kuhusu kutokea kwa tetemeko la ardhi katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo ambapo Reporter wa AyoTV na millardayo.com alifanya kazi ya kuzungumza na baadhi ya mashuhuda ambao walikubali kutuelezea walichokiona mwanzo mwisho. Video yote nimekuwekea hapa chini ruksa kuitazama…

VIDEO: “Hakuna mtu atapata uongozi CCM kama hajapita pale” – Humphrey Polepole

VIDEO: “Hakuna mtu atapata uongozi CCM kama hajapita pale” – Humphrey Polepole Katika kuhakikisha kinajiimarisha zaidi Chama cha Mapinduzi   ‘CCM’   kinatarajia kujenga Chuo cha Uongozi kwa ajili ya wanachama wake na watanzania ambao watatakiwa kusoma chuoni hapo kama wanataka kuwa viongozi kupitia chama hicho. Akizungumza jana April 30, 2017 katika Mahafali ya Umoja wa CCM Vyuo Vikuu Arusha, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM   Humphrey Polepole   alisema kuwa chama kitajenga Chuo cha uongozi na hapatokuwa na kiongozi wa chama na serikali kupitia chama hicho ambaye atapatikana bila kusoma Chuo hicho. “Hiki Chuo kitafundisha wana CCM. Hakuna mtu atapata uongozi kwenye Chama Cha Mapinduzi kama hajapita pale. Hakuna mtu atapata uongozi kwenye serikali kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kama hajapita pale .”   – Humphrey Polepole.

VIDEOMPYA: King kapita amerudi na hii, ameifanya nchi tatu tofauti ‘Vizabina’

VIDEOMPYA: King kapita amerudi na hii, ameifanya nchi tatu tofauti ‘Vizabina’ Mkali kutoka kwenye  Bongoflevani   King Kapita   ambaye alishawahi kuzichukua headline na mdundo wake ‘ Kuna Tatizo kwani ‘, jana April 30 2017 alitualika kuitazama video ya mdundo wake mpya ‘   Vizabina ‘ aliyoifanyia nchi ya Tanzania, Botswana na South Africa.

Ifahamu sababu kuu ya vifo vingi nchini India

Ifahamu sababu kuu ya vifo vingi nchini India Takwimu zilizowekwa na Jeshi la Polisi   India   zimeonesha kuwa watu wengi wamekuwa wahanga wa   ‘mapenzi’   zaidi ya ugaidi. Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa na   Times of India , kati ya mwaka 2001 na 2015, mapenzi yalikuwa sababu rasmi ya vifo   38,585   ikilinganisha ugaidi ambao ulisababisha vifo vya watu   20,000,   wakijumuisha raia wa kawaida na maafisa wa usalama. Professor mstaafu na mtaalamu wa masuala ya jinsia,   Uma Chakravarti,   aliiambia Times of India:   “Kuzielewa ghasia hizi katika kuharibu uhuru wa chaguo la mtu linapokuja suala la ndoa, mtu anatakiwa kuelewa hasa.”

VIDEO: Waziri Mwakyembe amekizindua kitabu cha ‘The color of Life’

VIDEO: Waziri Mwakyembe amekizindua kitabu cha ‘The color of Life’ Jana April 30 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alikizindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Ritha Tarimo ambapo katika hotuba yake aliyoitoa amesisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.  “Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa yeye ametuonyesha Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki niwaambie ukweli kina maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha ”-Mwakyembe Kwa upande wake Mwandishi Ritha Tarimo ameishukuru Serikali kwa kukubali wito wa kukizindua kitabu chake na pia utayari wa Serikali katika kumuunga mkono ili uandishi wake uwe wenye tija kwa jamii ya Watanzania.

VIDEO: Tottenham wameendeleza rekodi yao imara msimu huu

VIDEO: Tottenham wameendeleza rekodi yao imara msimu huu Tottenham Hotspurs   wameendelea tena jana Jumapili ya April 30 2017 katika mbio zao za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu   Englan d kwa kucheza na Arsenal,   Spurs   waliikaribisha Arsenal   katika uwanja wao wa   White Hart Lane   ambao msimu huu wana rekodi imara katika uwanja huo. Spurs   ambao wapo nyuma ya   Chelsea   kwa tofauti ya point nne wakiwa wote wamecheza michezo 34 kati ya 38, wameendeleza jitihada zao za kuhakikisha wanawania taji la   EPL hadi mwisho kwa kuifunga   Arsenal   kwa jumla ya magoli 2-0, magoli yakifungwa na   Delle Alli dakika ya 55 na   Harry Kane   kwa mkwaju wa penati dakika ya 58. Ushindi huo wa   Tottenham   dhidi ya   Arsenal   unakuwa ni ushindi wao wa 20 msimu huu katika mechi za mashindano tofauti tofauti wakiwa wana rekodi ya kutofungwa katika uwanja wao wa nyumbani wa...

VIDEO: ‘Inawezekana inatafsiriwa mimi ni mtu katili, wa ajabu’-Rais Magufuli

VIDEO: ‘Inawezekana inatafsiriwa mimi ni mtu katili, wa ajabu’-Rais Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 30 Aprili 2017, aliungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi, Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo. Rais Magufuli alisema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU. ‘ Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu’- Rais Ma...

PICHA 21: Kutoka kwenye harusi ya Madam Frola na Daudi Kusekwa.

PICHA 21: Kutoka kwenye harusi ya Madam Frola na Daudi Kusekwa. Staa wa muziki wa Injili Tanzania   Madam Flora  jana April 30 2017 alifunga ndoa na   Daudi Kusekwa  ikiwa ni baada ya kutengana na aliyekuwa mumewe   Emmanuel  picha 25 kutoka kwenye harusi hi yo Madam Flora na mumewe Daudi Kusekwa                                      

VIDEO: Agizo la Rais Magufuli alilolitoa leo mkoani Kilimanjaro

VIDEO: Agizo la Rais Magufuli alilolitoa leo mkoani Kilimanjaro Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 30 Aprili 2017, alikutana na kuzungumza na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali na kuuagiza viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kutatua kero zinazowakabili wananchi wa mkoa huo. Rais Magufuli alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya baadhi ya viongozi wa dini kueleza kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na manyanyaso yanayofanyiwa na wafanyakazi wa Wakala wa Maegesho ya magari mkoani humo. Kufuatia malalamiko hayo, Rais Magufuli amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kuchunguza mkataba uliongiwa kati ya Manispaa ya Moshi na Wakala wa Maegesho ya magari mkoni humo ili kujua uhalali wake kwani kumekuwa na ubadhirifu mkubwa wa upotevu wa mapato yatokanayo na makusanyo ya maegesho hayo. ‘Uangalie ule mkataba wa parking wa hapa Moshi,kama kuna ufisadi wowote peleka Mahakamani,lakini haya ya a...

VIDEO: Asley na Khadija Kopa walivyoizindua ‘Usiitie Doa’ DAR…..

VIDEO: Asley na Khadija Kopa walivyoizindua ‘Usiitie Doa’ DAR….. Ni Usiku wa kuamkia  1 May, 2017   ambapo msanii kutoka Yamoto Band,   Asley  na mwimbaji wa Taarabu, Khadija Kopa waliizindua single yao mpya iitwayo   Usiitie Doa   kwenye ukumbi wa   Maisha Club, itazame hii video hapa.

Leo ni Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ......Mgeni Rasmi Kitaifa ni Rais Magufuli

Leo ni Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ......Mgeni Rasmi Kitaifa ni Rais Magufuli Rais John Magufuli leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa. Kwa mujibu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), sherehe hizo zitafanyika kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU). Rais Magufuli aliwasili mjini Moshi juzi akitokea mkoani Dodoma na jana alishiriki Ibada za Jumapili katika makanisa mawili tofauti, na leo anatarajiwa kuongoza maelfu ya wakazi wa Moshi na miji jirani katika kilele cha sherehe hizo za Mei Mosi, huku wafanyakazi wakililia hali bora makazini. Akizungumza wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa Tucta, Yahaya Msigwa alisema, “Tayari tumemwandikia Rais Dk Magufuli kumuomba awe mgeni rasmi, kimsingi sherehe zote kitaifa mgeni rasmi ni yeye...tunazo ajenda za kumpa Rais, lakini moja ya mambo ambayo ni kero ni hili la mikataba ya hali bora kazini, wafanyakazi wengi wanafan...