VIDEO: “Hakuna mtu atapata uongozi CCM kama hajapita pale” – Humphrey Polepole
Katika kuhakikisha kinajiimarisha zaidi Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ kinatarajia kujenga Chuo cha Uongozi kwa ajili ya wanachama wake na watanzania ambao watatakiwa kusoma chuoni hapo kama wanataka kuwa viongozi kupitia chama hicho.
Akizungumza jana April 30, 2017 katika Mahafali ya Umoja wa CCM Vyuo Vikuu Arusha, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole alisema kuwa chama kitajenga Chuo cha uongozi na hapatokuwa na kiongozi wa chama na serikali kupitia chama hicho ambaye atapatikana bila kusoma Chuo hicho.
“Hiki Chuo kitafundisha wana CCM. Hakuna mtu atapata uongozi kwenye Chama Cha Mapinduzi kama hajapita pale. Hakuna mtu atapata uongozi kwenye serikali kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kama hajapita pale.” – Humphrey Polepole.