Skip to main content

VIDEO: ‘Inawezekana inatafsiriwa mimi ni mtu katili, wa ajabu’-Rais Magufuli

VIDEO: ‘Inawezekana inatafsiriwa mimi ni mtu katili, wa ajabu’-Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 30 Aprili 2017, aliungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi, Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.
Rais Magufuli alisema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU.
Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu’-Rais Magufuli.
‘Nafikiri mnaweza mkaona sura yangu, ni inawezekana inatafsiriwa mtu katili, wa ajabu, siko hivyo, mimi ni mpole, mnyenyekevu, mwenye upendo mkubwa, ninayeogopa dhambi na mwenye hofu ya Mungu lakini ukweli mimi ni mkali kwa maovu’-Rais Magufuli.
 


Popular posts from this blog

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU” kama  ifuatavyo : SEHEMU  YA  PILI   YA  KITABU  “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU “ Wachawi   wakishindwa  kukutengenezea  kesi  kubwa  basi  waatakufunga  kwenye  kifungo  cha  mapenzi.  Katika  vifungo  vyote anavyo  fungwa  mwanadamu  hakuna  kifungo  kibaya  kama  kifungo  cha  mape

Faida nyingine za kula chungwa

Faida nyingine za kula chungwa Siku kadhaa zilizopita tuliangalia kwa uchache kuhusu faida za kula chungwa hivyo, pia siku ya leo naomba tuendelee kwa kuangalia faida nyingine za kula chungwa. 1. Ulaji wa machungwa husaidia kutibu mapafu. Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu. 2. Husaidia kuimarisha mifupa ya meno. Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno. 3. Husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini. Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake. 4. Hupunguza kupatwa magonjwa wa figo. Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaid

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi?

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi? Unafikili ni wazo zuri kuamka  saa 11 za asubuhi na kufanya mazoezi? Je, ingekuwa vipi kama ungetumia muda huo kulala? Wataalamu wa afya wanashauri kuwa binadamu kwa kwaida anapaswa kulala angalau masaa 7 wakati wa usiku ili kuupa mwili afya bora. Kulala kwa muda mfupi au masaa machache husababisha matatizo ya afya, ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, unyogovu, ugonjwa wa kisukari, na kupunguzwa kinga kukabiliana na chanjo. Ni vyema ukatumia muda wako vizuri mchana ili usiku ukapata muda mwafaka wa kuweza kuupumzisha mwili ili kuepukana na magonjwa hatari ya shinikizo la damu, kisukari na kupungua kwa kinga mwilini. Najua mazingira yetu waafrika ya kimaisha wakati mwingine yanachangamoto nyingi, lakini pale upatapo mwanya kidogo tu, basi utumie yani "kila penye tundu, penyeza lupia" au wawenzetu wazungu wanasema "one chance two goals".