VIDEO: Tottenham wameendeleza rekodi yao imara msimu huu
Tottenham Hotspurs wameendelea tena jana Jumapili ya April 30 2017 katika mbio zao za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu England kwa kucheza na Arsenal, Spurs waliikaribishaArsenal katika uwanja wao wa White Hart Lane ambao msimu huu wana rekodi imara katika uwanja huo.Spurs ambao wapo nyuma ya Chelsea kwa tofauti ya point nne wakiwa wote wamecheza michezo 34 kati ya 38, wameendeleza jitihada zao za kuhakikisha wanawania taji la EPLhadi mwisho kwa kuifunga Arsenal kwa jumla ya magoli 2-0, magoli yakifungwa na Delle Allidakika ya 55 na Harry Kane kwa mkwaju wa penati dakika ya 58.
Ushindi huo wa Tottenham dhidi ya Arsenal unakuwa ni ushindi wao wa 20 msimu huu katika mechi za mashindano tofauti tofauti wakiwa wana rekodi ya kutofungwa katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane msimu huu, wakiwa wamefunga magoli 62, wakiruhusu kufungwa magoli 11 sare mechi 2 lakini wamecheza pia mechi 15 bila kuruhusu goli.