VIDEO: Waziri Mwakyembe amekizindua kitabu cha ‘The color of Life’
Jana April 30 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alikizindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Ritha Tarimo ambapo katika hotuba yake aliyoitoa amesisitiza suala la vijana kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.
“Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa yeye ametuonyesha Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki niwaambie ukweli kina maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha”-Mwakyembe
Kwa upande wake Mwandishi Ritha Tarimo ameishukuru Serikali kwa kukubali wito wa kukizindua kitabu chake na pia utayari wa Serikali katika kumuunga mkono ili uandishi wake uwe wenye tija kwa jamii ya Watanzania.