Skip to main content

VIDEO: Agizo la Rais Magufuli alilolitoa leo mkoani Kilimanjaro

VIDEO: Agizo la Rais Magufuli alilolitoa leo mkoani Kilimanjaro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 30 Aprili 2017, alikutana na kuzungumza na viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali na kuuagiza viongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kutatua kero zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo kufuatia malalamiko ya baadhi ya viongozi wa dini kueleza kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na manyanyaso yanayofanyiwa na wafanyakazi wa Wakala wa Maegesho ya magari mkoani humo.
Kufuatia malalamiko hayo, Rais Magufuli amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kuchunguza mkataba uliongiwa kati ya Manispaa ya Moshi na Wakala wa Maegesho ya magari mkoni humo ili kujua uhalali wake kwani kumekuwa na ubadhirifu mkubwa wa upotevu wa mapato yatokanayo na makusanyo ya maegesho hayo.
‘Uangalie ule mkataba wa parking wa hapa Moshi,kama kuna ufisadi wowote peleka Mahakamani,lakini haya ya administration kayaangalie wasinyanyase watu, huwezi hata ukamuona sheikh unafunga gari lake,ukimuona Mchungaji na kola yake unafunga tu ni ushetani, sasa saa nyingine wale vijana wanaofanya ile kazi wanajisahau, hawaheshimu utu wa Watanzania’Rais Magufuli.
Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Manisapaa ya Moshi kutoa kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Uchunguzi wa maradhi kilichoombwa na mwananchi mmoja mkoani humo ili aweze kuendelea na ujenzi huo kutokana na kutopewa kibali hicho kwa muda mrefu. 
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema kutokana na Serikali kuzuia unywaji wa pombe aina ya viroba idadi ya vifo katika mkoa wa Pwani imepungua kutoka 80 hadi 20 na hata ajali za pikipiki maarufu Bodaboda nazo zimepungua nchini.
Aidha, Rais Magufuli ametaka uongozi wa Wilaya ya Hai kufanya kazi bila kutishwa na madiwani ikiwa ni pamoja na kubadili sheria ndogondogo wilayani humo ili kupunguza kero za utitiri wa ushuru kwa wananchi. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo wakati alipokutana na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro, Vyama vya Siasa na watendaji wa Serikali mkoani humo na kula nao chakula cha mchana kilichoandaliwa na mkoa wa Kilimanjaro.


Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti WAKATI bei ya unga wa sembe ikipanda mpaka kufikia kuuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500 kwa kilo, ile ya mfuko wa saruji wenye uzito wa kilo 50 imeshuka hadi sh. 9,000, sawa na Sh. 180 kwa kilo. Katika masoko na maduka mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambayo Nipashe ilitembelea jana, bei ya sembe ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi hicho kwa rejareja huku wauzaji wa jumla wakiuza kiroba cha kilo 50 kwa kati ya sh.100,000 na sh.98,000. Ibrahim Omary, mfanyabiashara wa Kariakoo alisema anauza unga wa sembe kwa Sh. 2,400 kwa kuwa hununua kwa bei kubwa kutoka kwa wazalishaji. Alisema kampuni inayojulikana kwa jina la Mkulima huwauzia unga huo kwa Sh. 98,000 na Mama Neema huwauzia kwa sh. 100,000 kwa kiroba cha kilo 50. Kwenye baadhi ya maduka ya kula ya Kinondoni, unga umekuwa ukiuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500. Tandika bei ya wastani ni Sh. 2,200, Mwenge Sh. 2,400, Kimara sh. 2,500 na Yombo Vituka sh. 2,200. ...

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla...