Waziri Mkuu: Ni Marufuku Wazee wa Miaka 60 Kutozwa Kodi za Majengo WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka maofisa wa Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania (TRA) wakusanye kodi za majengo kwa kuzingatia sheria na wasitoze kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60. “TRA ijipange kukusanya kodi za majengo kuanzia Julai mosi 2017. Katika kutekeleza jukumu hilo, zingatieni sheria. Tusisikie mnawadai kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 kwa majengo wanayotumia kama makazi yao,” alisema Majaliwa. Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa Wilaya ya Chato waliohudhuria uzinduzi wa jengo la TRA wilayani humo mkoani Geita. Waziri Mkuu amewataka moafisa hao wakusanye kodi ya majengo kwenye maeneo ya mjini na siyo vijijini kwani kodi hiyo haiwahusu. “Msiende vijijini. Nyumba za nyasi au za tembe hazihusiki. Tembeleeni nyumba za mijini. Piteni kwenye mitaa, muainishe aina zote za nyumba zinazostahili kulipiwa kodi. Mkishafanya sens...