Skip to main content

Serikali Yatangaza Ajira Mpya 52,436


Serikali Yatangaza Ajira Mpya 52,436

Serikali  inakusudia kuajiri watumishi wapya wa umma 52,436 katika mwaka ujao wa fedha. 

Aidha, madaktari wapya 258 waliokuwa waende kufanya kazi nchini Kenya, lakini wakakwama kutokana na kuwekewa pingamizi la kimahakama na wenzao wao huko na hivyo Rais, Dk John Magufuli kuamuru waajiriwe mara moja nchini, wanatarajiwa kuanza kazi keshokutwa Jumatatu.

Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).

“Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti.

“Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi ya watu 9,700 na tutaendelea kufanya hivyo, na hivi karibuni Rais amebariki kuajiriwa kwa madaktari wapya 258 na Jumatatu (keshokutwa) wanaripoti kazini.

"Tutaendelea kuajiri na wataalamu wa kada nyingine, kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha mwezi Juni tutakuwa tumejiajiri kwa idadi tutakayoipanga kwa awamu, na katika mwaka ujao wa fedha tutaendelea kuajiri watumishi wengine wa umma zaidi ya 52,436,”alisema.

Hata hivyo, alisisitiza Serikali itahakikisha hairudii makosa ya kuajiri watumishi hewa, wasio na sifa na weledi unaohitajika. 

Alisema kwa kiasi kikubwa uhakiki wa watumishi wa umma kwa ujumla umekwisha, lakini kazi hiyo ni endelevu, kwani serikali itaendelea kufanya hivyo mara kwa mara.

Alisema matunda ya uhakiki wa watumishi wa umma umebaini watumishi hewa 19,708 na ambao wameshaondolewa katika orodha ya mishahara ya watumishi wa umma. 

“Hawa wangeachwa, Serikali ingekuwa inapoteza kiasi cha Sh bilioni 19.8 kila mwezi, lakini fedha hizi zimeokolewa kupitia uhakiki wa watumishi wa umma.

"Tunafanya haya kwa nia njema. Mathalani tusingewatoa hawa, si wangeziba nafasi za ajira za wengine na fedha ngapi zingepotea?”alihoji. 

Alisisitiza kuwa, wizara hiyo itaendelea kutimiza majukumu yake kwa vitendo ili kurejesha nidhamu ya serikali na utumishi wa umma kwa kuongeza uwazi na kusimamia sheria, kanuni na taratibu za uwajibikaji wa viongozi wa watumishi wa umma ili wawajibike kwa wananchi ambao ndio wateja na waajiri wakuu wa watumishi wa umma.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, akijibu hoja za wabunge, hasa la uhamisho wa watumishi wakiwemo wanandoa wanaotenganishwa, alikemea tabia ya maofisa watumishi kuzuia wenye ndoa kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwa lengo la kuwafuata wenzao.

Alisema kuwazuia ni kuwanyima haki ya msingi, na kuwaagiza wabunge katika maeneo yao wasaidia kusimamia haki za watumishi. 

"Lazima sheria za utumishi zizingatiwe, walimu hawa au watumishi wanayo haki ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini pia kuishi na wenza wao, lakini utadhani mtumishi anapoomba ni kama anasaidiwa, hapana ni haki yake ya msingi, waheshimiwa tusimamie haki za watumishi,” alisema Simbachawene

Popular posts from this blog

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia.  Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katika miradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato.  Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake k ij iji cha  Itiry o   kusherekea sikukuu ya Pasaka.  Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ...

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4 Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu. Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo  Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni maalum kwa ajili ya bajeti. Ratiba hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne, ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25. Mbali na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017 ==>Itazame hapa ratiba kamili ya mkutano huu...

Hatua 5 za kutatua tatizo lolote unalokutana nalo

Hatua 5 za kutatua tatizo lolote unalokutana nalo Hatua ya kwanza; jua kwa undani tatizo ni nini.  Najua utashangaa lakini ukweli ni kwamba wengi ambao wanakuwa na matatizo huwa hawajui tatizo hasa walilonalo ni nini. Na hivyo wanapokazana kulitatua wanashindwa, kwa sababu kama hujajua kiini cha tatizo huwezi kulitatua. Mara nyingi watu wamekuwa wakiangalia madhara ya tatizo, badala ya kuangalia chanzo kikuu cha tatizo. Huwezi kutibu tatizo kwa kutibu madhara, badala yake unahitaji kuzama ndani na kujua chanzo hasa cha tatizo ni nini. Na njia ya uhakika ya kufikia hilo ni kuuliza swali moja muhimu sana, KWA NINI. Uliza swali hili mara tano, yaani uliza kwa hatua tano. Kwa mfano kama tatizo lako ni kipato kidogo kwenye biashara yako, jiulize kwa nini kipato ni kidogo, jibu linaweza kuwa wateja ni wachache, jiulize tena kwa nini wateja ni wachache, hapo utapata majibu mengine, kwa kila jibu jiulize tena kwa nini? Mpaka utafika mahali na kuona hiki ndio kiini kikuu c...