Skip to main content

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia. 

Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katikamiradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato. 

Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake kijiji cha  Itiryo kusherekea sikukuu ya Pasaka. 

Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ujumla.
 
Alisema awali, wilaya hiyo ilikuwa na sifa mbaya nchini na kimataifa, kutokana na kuzuka kwa mapigano ya koo za makabila ya Wakurya na Waluo, yaliyochochewa na wizi wa mifugo. 

Waitara alisema ipo haja kwa jamii inayoishi kando ya Hifadhi ya Serengeti, kuthamini rasilimali za wanyamapori kuwa ni miongoni mwa tunu za taifa na hakuna budi kuzitunza na kuzilinda kwa ajili vizazi vya sasa na vijavyo. 

"Ni muhimu jamii yetu itambue kuwa, wanyama waliopo ni wetu kwa faida yetu na taifa la leo na vizaz vijavyo. Kuendekeza uwindaji haramu kunasababisha hasara kubwa dhidi ya rasilimali hiyo, hivyo ni muhimu jamii yetu ikatumia fursa zilizopo katika utalii ili kunufaika nazo,"alisema. 

Kuhusu miradi ya kijamii inayoibuliwa na vijiji na kisha kupitishwa na kamati za maendeleo za kata, kama vipaumbele vyao vya kutekelezwa na Hifadhi ya Mbuga ya Taifa ya Serengeti (SENAPA), alisema utekelezaji wake utasubiri kutokana na bajeti ya hifadhi hiyo.

Popular posts from this blog

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi?

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi? Unafikili ni wazo zuri kuamka  saa 11 za asubuhi na kufanya mazoezi? Je, ingekuwa vipi kama ungetumia muda huo kulala? Wataalamu wa afya wanashauri kuwa binadamu kwa kwaida anapaswa kulala angalau masaa 7 wakati wa usiku ili kuupa mwili afya bora. Kulala kwa muda mfupi au masaa machache husababisha matatizo ya afya, ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, unyogovu, ugonjwa wa kisukari, na kupunguzwa kinga kukabiliana na chanjo. Ni vyema ukatumia muda wako vizuri mchana ili usiku ukapata muda mwafaka wa kuweza kuupumzisha mwili ili kuepukana na magonjwa hatari ya shinikizo la damu, kisukari na kupungua kwa kinga mwilini. Najua mazingira yetu waafrika ya kimaisha wakati mwingine yanachangamoto nyingi, lakini pale upatapo mwanya kidogo tu, basi utumie yani "kila penye tundu, penyeza lupia" au wawenzetu wazungu wanasema "one chance two goals".

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4 Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu. Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo  Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni maalum kwa ajili ya bajeti. Ratiba hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne, ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25. Mbali na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017 ==>Itazame hapa ratiba kamili ya mkutano huu, am