Skip to main content

HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS IJUMAA APRIL 28,2017

HAFLA YA KUCHANGIA SERENGETI BOYS IJUMAA APRIL 28,2017



Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa hafla maalumu ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya Serengeti Boys
inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 17 nchini Gabon. Fainali hizi zitafanyika kufanyika
kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017. 

TFF inatambua kuwa wadau
mbalimbali wamekuwa wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama
vile namba 0687 333 222 kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka
fedha kwenye akaunti Na. 00 866 280 03 katika Benki ya Diamond Trust
(DTB).

Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa hafla
maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi
maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo
itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja
jioni.

TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi wa
makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni
rasmi.

Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa
kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF
inaomba wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao
wamekusanya michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi
michango ya makundi yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.

Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma email kwenda fdf@tff.or.tz,
kwa kupiga simu 0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787
176767 ambayo pia inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.

Aidha
wawakilishi wa makundi mengine kama idara za Serikali, mashirika ya
umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao wamechangia nao pia
tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi michango yao
siku hiyo ya Ijumaa.

TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.

Mungu Ibariki Tanzania

Mungu ibariki Serengeti Boys 

Popular posts from this blog

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia.  Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katika miradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato.  Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake k ij iji cha  Itiry o   kusherekea sikukuu ya Pasaka.  Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ...

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4 Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu. Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo  Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni maalum kwa ajili ya bajeti. Ratiba hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne, ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25. Mbali na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017 ==>Itazame hapa ratiba kamili ya mkutano huu...

Umesikia alichokisema Shaffih Dauda Kuhusu Kukamatwa na TAKUKURU?

Umesikia alichokisema Shaffih Dauda Kuhusu Kukamatwa na TAKUKURU? Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU kwa mwenyekiti wa chama cha mpira Dar es Salaam DRFA Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza. Taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kukamatwa kwa watu hao zinadai ni viashiria vya rushwa na kuhusishwa na kampeni za chini kwa chini za uchaguzi Mkuu wa TFF, hivyo TAKUKURU ikawakamata kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa kadhaa kabala ya kuwaachia kwa dhamana. Baada ya kurejea Dar es Salaam akitokea Mwanza Shaffih Dauda alipokuwa amekwenda na viongozi wa DRFA kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup kupitia Clouds FM ameeleza tukio la kukamatwa kwao lilivyokuwa ambalo linadaiwa kulenga kuwachafua katika uchaguzi Mkuu wa TFF. “Nimehojiwa na TAKUKURU nikiwa Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup ambay...