Skip to main content

Ufafanuzi Juu Ya “Uzushi” Ulioenea Kwenye Mitandao Ya Kijamii Kuhusu Kufukuzwa Nchini Raia Wa Kenya, Wilayani Longido, Mkoa Wa Arusha.

Ufafanuzi Juu Ya “Uzushi” Ulioenea Kwenye Mitandao Ya Kijamii Kuhusu Kufukuzwa Nchini Raia Wa Kenya, Wilayani Longido, Mkoa Wa Arusha.


Kumekuwepo taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya kijamii kuwa, Serikali ya Tanzania inafanya operesheni maalum inayolenga kuwaondoa Raia wa Kenya wanaoishi nchini bila kuwa na Vibali halali huko Wilayani Longido, Mkoa wa Arusha, huku wakimhusisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika utekelezaji wa ‘zoezi’ hilo. 
 
Taarifa hizi zimezua tafrani na kutishia hali ya usalama iliyopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga.Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu Taarifa hizo zinazoendelea kuenezwa kuwa:-
 
1.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijafanya operesheni yoyote inayolenga kuwakamata na kuwaondoa nchini raia wa Kenya au Taifa lolote lile wanaoishi katika Wilaya ya Longido Mkoani Arusha kama inavyoenezewa kwenye Vyombo vya Habari na Mitandao mbalimbali ya kijamii.

2.Shughuli za udhibiti wa raia wa kigeni wanaokiuka Sheria za Uhamiaji nchini hazifanywi kwa kulenga Taifa lolote lile, bali hufanywa kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi. Wahusika wanaokiuka Sheria, Kanuni na Taratibu za uhamiaji hukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa makosa yao binafsi na sio kwa msingi wa utaifa wao.

3.Kukamatwa kwa raia wa kigeni ambao walibainika kuwa ni raia wa Kenya ni sehemu ya shughuli za kawaida za Idara ya Uhamiaji kama Chombo cha Ulinzi na Usalama katika kuhakikisha kwamba raia wa kigeni wanatambuliwa na kuishi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.
 
4.Suala la kukamatwa kwa raia hao wa Kenya ambao walibainika kukiuka Sheria ya Uhamiaji nchini halihusiani kwa njia yoyote ile na Serikali ya Tanzania kulenga kuwakamata raia wa nchi yoyote na wala si agizo la Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyoripotiwa, bali ni utaratibu wa kawaida ambao unafanywa na nchi yoyote katika kuhakikisha kwamba ukaazi wa wageni unazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi husika. Kwa mfano, katika mwezi Februari 2017, Idara ya Uhamiaji imewakamata wageni 396 kutoka mataifa mbalimbali kwa makosa ya kiuhamiaji na kuwachukulia hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria.

5.Tanzania na Kenya tunao uhusiano mzuri sana ambao ni wa kihistoria na nchi hii ni mwanachama mwenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa uhusiano huo, wapo watanzania wengi wanaokwenda nchini Kenya kwa sababu mbalimbali kama vile matembezi, biashara, masomo nk. Pia wapo raia wengi wa Kenya wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa sababu kama hizo hizo na hatuna tatizo nao, alimradi hawavunji Sheria za nchi yetu.

6.Mwisho, tunatoa wito kwa Wageni wote wanaoishi hapa nchini kwa shughuli mbalimbali kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za uhamiaji nchini. Wapo baadhi ya wageni wanaoingia nchini kihalali, lakini wanaendelea kuishi nchini hata baada ya muda waliopewa kuishi nchini kumalizika. Aidha, wapo baadhi ya wageni wengine wanaoingia nchini kinyume cha sheria na kuendelea kuishi nchini kinyume cha Sheria. Wale wanaobainika kukiuka Sheria, Kanuni na taratibu za uhamiaji nchini watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria bila kujali utaifa wao.

7.Taarifa zinazoenezwa kupitia Vyombo vya Habari na Mitandao ya kijamii kwamba Tanzania inawalenga raia wa Kenya, kuwakamata na kuwaondoa nchini si sahihi na zipuuzwe kwani zinalenga kuchafua na kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi zetu mbili na wananchi wake, pamoja na kudhoofisha shughuli za udhibiti wa wahamiaji haramu nchini.

8.Tunafahamu kuwa Tanzania haiwezi kuishi kama kisiwa. Hivyo, tutaendeleza na kuimarisha ushirikiano na Mataifa mengine pamoja na kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa wageni kuja na kuishi nchini kwa shughuli mbalimbali, zikiwemo biashara, uwekezaji, utalii, matembezi na nyinginezo.  

Imetolewa na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
BARABARA YA LOLIONDO, KURASINI,
 S.L.P 512, DAR ES SALAAM.
31 MACHI, 2017.
www.immigration.go.tz

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ ...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...