Ufafanuzi Juu Ya “Uzushi” Ulioenea Kwenye Mitandao Ya Kijamii Kuhusu Kufukuzwa Nchini Raia Wa Kenya, Wilayani Longido, Mkoa Wa Arusha. Kumekuwepo taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya kijamii kuwa, Serikali ya Tanzania inafanya operesheni maalum inayolenga kuwaondoa Raia wa Kenya wanaoishi nchini bila kuwa na Vibali halali huko Wilayani Longido, Mkoa wa Arusha, huku wakimhusisha Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika utekelezaji wa ‘zoezi’ hilo. Taarifa hizi zimezua tafrani na kutishia hali ya usalama iliyopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga.Tunapenda kutoa ufafanuzi kuhusu Taarifa hizo zinazoendelea kuenezwa kuwa:- 1.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijafanya operesheni yoyote inayolenga kuwakamata na kuwaondoa nchini raia wa Kenya au Taifa lolote lile wanaoishi katika Wilaya ya Longido Mkoani Arusha k...