Skip to main content

Irene Uwoya: Wasanii tusikubali kutawaliwa na siasa

Irene Uwoya: Wasanii tusikubali kutawaliwa na siasa

Baada ya kashikashi za hapa na pale ya wasanii wa bongo movie kuingia kwenye siasa huku Wema Sepetu akihamia CHADEMA na kusema anaidai CCM, swahiba wake, Batuli amekanusha. Wakati vita vya maneno vikiendelea, mwenzao, Irene Uwoya amewachana.

Irene ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno yenye busara ndani:

Katika maisha siku zote ushauri unaruhusiwa kutolewa au kupokelewa… Lakin sio lazima mtu kupokea ushauri unaotolewa… Kila mtu anauhuru wakuamua kitu ambacho anahisi kinamfaa kwenye maisha sababu… Sazingine kwenye maisha Kuna sehemu inafika unacho jiskia kwenye moyo wako sio rahisi mtu mwingine kujiskia … Sasa ni mbaya sana kuishi kwa hisia… Ifikie Wakati tujitaidi kuheshimu hisia Za mtu… Lakin pia kunavitu vingine nazani Nivyema vkabaki kwa wausika wavinaowahusu…yani sio lazima kuongea kila kitu kwenye jamiii… Watu wanatamani sazingine kuskia vtu ambavyo wanahisi vinafaida kwa Jamaniii… Kunavitu vingine ukiongea havina maana.”

Mfano mim ni CCM damu… Lakin kunavitu vinaboa sanaaa Kweli kada mzima wa CCM unasimama hazarani unasema tulilipwa kufanya campaign? hatakama lakini unafundisha Nin Jamiii? Unafundisha jamiii kwamba yote tuliyoongea kuhusu CCM hatukuyaamanisha nikwasababu tulilipwa? Unaiambia jamiii ulikuwa tayari kuwadanganya na mliwadanganya sababu mlilipwa? Hivi Kweli? Kwahiyo jamiii ione Chochote Tutachoonge wasikiamini maana yake tutakuwa tumelipwa? Kwahiyo ata mnayoyaongea mnataka kusema mmelipwa? Minazani tujifunze kunyamaza sazingine kama hamna ulazima wakuongea mnaweza kuhisi mmnajenga kumbe mnaharibu kabisaaa… Embu Tufanye Kazi zinazo tuhusu Jamaniii… Nigeria wenzetu sasa wako Hollywood wanaigiza huko… Sisi ata nigeria kwenyewe bado hatuja pasua… Lakin hapa Tupo busy kushabikia ujinga na vitu vya kipumbafu na visivyo na Msaada kwajamiii… Kwastaili hiii… Hollywood tutaiskia na kuiona kwenye TV.no

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti

Bei ya unga sasa ni mara 12 ya mfuko wa Simenti WAKATI bei ya unga wa sembe ikipanda mpaka kufikia kuuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500 kwa kilo, ile ya mfuko wa saruji wenye uzito wa kilo 50 imeshuka hadi sh. 9,000, sawa na Sh. 180 kwa kilo. Katika masoko na maduka mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambayo Nipashe ilitembelea jana, bei ya sembe ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi hicho kwa rejareja huku wauzaji wa jumla wakiuza kiroba cha kilo 50 kwa kati ya sh.100,000 na sh.98,000. Ibrahim Omary, mfanyabiashara wa Kariakoo alisema anauza unga wa sembe kwa Sh. 2,400 kwa kuwa hununua kwa bei kubwa kutoka kwa wazalishaji. Alisema kampuni inayojulikana kwa jina la Mkulima huwauzia unga huo kwa Sh. 98,000 na Mama Neema huwauzia kwa sh. 100,000 kwa kiroba cha kilo 50. Kwenye baadhi ya maduka ya kula ya Kinondoni, unga umekuwa ukiuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500. Tandika bei ya wastani ni Sh. 2,200, Mwenge Sh. 2,400, Kimara sh. 2,500 na Yombo Vituka sh. 2,200. ...

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla...