Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Miti Ya Kwenye Kitanda Cha Sokwe Mtu Katika Kutengeneza Na Kutuma Uchawi Hatari Wa Kuwafilisi Watu .
Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Miti Ya Kwenye Kitanda Cha Sokwe Mtu Katika Kutengeneza Na Kutuma Uchawi Hatari Wa Kuwafilisi Watu .
Na. DOKTA MUNGWA KABILI……..0744 000 473
Haya ni maelezo yanayo patikana ndani ya kitabu “ Kitanda Cha Sokwe Mtu “
Lugwisha aliletwa kwangu saa nne kamili za asubuhi na nikaanza kumshughulikia saa saba kamili mchana.
Zoezi la kwanza lilikuwa kupima aina na kiwango cha uchawi alicholishwa.
Zipo njia mbalimbali za kumpima mtu ili kujua kiwango na aina ya uchawi aio lishwa, Njia moja wapo ni kulishwa dawa maalumu ya kutapisha uchawi au kuumfanya aharishe uchawi husika.
Njia za kutapisha pia zipo za aina mbili, aina ya kwanza ni kutapisha uchawi kwa njia ya kawaida na aina ya pili ni kutapisha kupitia nyongo.
Sasa basi kwenye kutapisha uchawi, huwa kuna mti mmoja wa porini hatari sana katika kutapisha uchawi. Mti huu huwa unatapisha uchawi wa aina yoyote ile.
Ni moja kati ya miti iliyo katika daraja la juu kabisa katika miti ya uganga. Mti huu una maruhani na majini wakali zaidi ya mia tatu.
Mti huu unapatikana porini. Unataka kuujua ni mti gani ? Soma maelezo yafuatayo;
Porini huwa kuna ndege mmoja mwenye maajabu makubwa sana. Ndege huyu ana tumbo la rangi nyekundu au rangi ya pinki. Kichwa chake huwa kina rangi sawa sawa na rangi ya tumboni na mgongo wake huwa na rangi nyeusi ambayo hutapakaa hadi kwenye mkia wake.
Ndege huyu ana sifa moja kubwa na ya kipekee. Ni kwamba, chochote utakacho mfanyia kiwe kibaya au kizuri, basi kitarudia wewe mwenyewe . Kwa mfano ukimtoboa jicho, basi na wewe hazitapita siku saba utatobolewa jicho.
Ukimkata mguu, na wewe ndani ya siku saba uta katwa mguu nakadhalika.
Kiota chake kina maajabu yanayo fanana na ndege mwingine wa porini aitwae fundi chuma.
Ni kwamba uki haribu kiota chake, kama una nyumba basi nyumba yao nayo itaharibiwa eidha kwa mafuriko, kimbunga, moto au chochote kile.
Na kama haujawahi kujenga basi ndio hautajenga katika maisha yao yote.
Huyu ndege huwa anakula matunda ya kwenye mti mmoja tu. Huu mti nao una majini wengi wabaya kwa wazuri.
Wachawi huwa wana utumia mti huu kwa mambo mengi sana, moja wapo ni kumtupia mtu mkuli wa paka kwa lengo la kumtengeneza awe banda la kufugia mapepo wachafu.
Jinsi wanavyo fanya, mchawi anatafuta paka mweusi. Paka huyu mweusi lazima akutane nae usiku wa kuanzia saa sita na awe amekutana nae kwa bahati mbaya, asipange kukutana nae, vinginevyo amuite paka huyu kwa kutumia uchawi.
Paka huyu akisha patikana huchukuliwa na kupelekwa hadi kwenye mti huu, na kuchinjwa kisha damu yake kumwagwa kwenye mti huo kwa tambiko maalumu.
Baada ya hapo matawi matatu yatachukuliwa kutoka kwenye mti huo, kisha mchawi atakwenda nao mpaka kaburini.
Akifika kaburini anaenda kuamsha mkuli wa kwenye kaburi husika na kuunganisha na mkuli wa paka aliyetolewa kafara kisha vyote kwa pamoja vinaunganishwa na majini ya huo mti na kutumwa kwa mtu aiyekusudiwa kwa lengo la kumtupia ugonjwa wa kumfanya awe analia kama paka na kujikuna kama paka.
Sasa basi mizizi ya mti huu ndio kiungo kikuu kinacho tumika katika kumtapisha mtu uchawi kwa lengo la kugundua kiwango cha uchawi na aina ya uchawi alio tupiwa.
Mtu aisha lishwa dawa hii atatapika ama kuharisha uchawi wote alio lishwa, muchaw huu utachukuliwa na kwenda kuchomwa njia panda kwa kutumia miti maalumu.
Katika zoezi la kuchoma uchawi huu kwa kutumia miti hiyo maalumu ndipo itajulikana aina ya uchawi alio tupiwa mtu.
Kwa kutumia njia ya kuteketeza uchawi huu kwa kutumia miti maalumu unaweza kugundua aina ya uchawi ulio tumika na kijiji ulipo tumiwa.
Katika ulimwengu wa wachawi kila kijiji kina kazi yake.
Mfano mchawi anapotaka kumwambia mwenzake anataka kuzungumzia uchawi wa aina Fulani, badala ya kutaja uchawi huo, yeye atataja jina la kijiji kinacho husiana na uchawi huo na moja kwa moja mchawi mwenzake ataelewa anamaanisha nini.
Sasa basi baada ya zoezi la kuteketeza kwa moto maalumu uchawi alio tumiwa kijana Lugwisha, niligundua kuwa ametupiwa uchawi kutoka kijiji kimoja cha wilaya ya Rufiji na mwingine umetumwa kutoka kwenye kijiji kimoja cha wilaya ya Kasulu mkoani kibondo.
Uchawi alio tumiwa kutoka Rufiji ni aina ya uchawi ambao hujulikana kama Sunkwa.
Asili ya ya uchawi huu ni kijiji kimoja cha wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.
Sunkwa ni uchawi ambao lengo lake ni kumfukuza mtu kwa kutumia uchawi na kumfunga asirudi tena katika eneo alilo fukuzwa.
Zipo njia nyingi sana ambazo wachawi huzitumia kutengeneza uchawi wa sunkwa na kuutuma kwa watu walio wakusudia.
Katika kitabu hiki nitaelezea njia moja wapo. Njia hii ndio ambayo imetumika dhidi ya Lugwisha .
Jinsi uchawi wa sunkwa unavyo fanyika; Kwanza inachukuliwa miti saba ambayo hutumiwa na sokwe kutengeneza kitanda .
Miti hii lazima ichukuliwe katika maeneo tofauti tofauti saba na huchukuliwa kwa tambiko maalumu.
Porini sokwe mtu huwa na vitanda vyao. Hutengeneza vitanda vyao kwa kutumia miti mbalimbali.
Kuhusu vitanda vya sokwe mtu huwa kuna sifa moja kuu nayo ni kwamba, sokwe mtu huwa hawezi kutengeneza kitanda cha kudumu na wala hawezi kukaa sehemu moja kwa muda mrefu.
Sokwe mtu anapotengeneza kitanda chake huwa anakaa kwa muda mfupi sana na baada ya hapo huhama katika eneo hilo na kuhamia sehemu nyingine ambako nako huko ataenda kutengeneza kitanda kingine. Hali hii huwa hivi katika maisha yote ya sokwe mtu.
Sasa basi, miti inayo tumika kutengeneza kitanda cha sokwe mtu , pamoja na kazi nyinginezo, huwa pia inachukuliwa na kutumika katika kutengeneza uchawi wa kumfukuza mtu na kumfanya aishi maisha ya kuhamahama na kutanga tanga.
Kinacho fanyika huwa hivi; Kwanza inachukuliwa miti au fimbo zilizo tumika kutengeneza kitanda cha sokwe mtu, zinagawanywa katika mafungu mawili, fungu la kwanza linatumika kutengeneza kijimtumbwi kidogo na fungu la pili linasagwa pamoja na mafuta ya usiku.
Baada ya hapo yanachukuliwa majani yaliyo peperushwa na kimbunga ambayo yaidakwa juu kwa juu kabla hayaja tua chini, unachukuliwa mchanga na uchafu wa kutoka kwenye njia na barabara arobaini zap kutoka sehemu tofauti tofauti, mchanga na udongo wa kutoka kwenye mikoa yote ya Tanzania, anachukuliwa kimburu; kimburu ni paka aliye asi nyumbani na kwenda kuishi porini, huyu paka anaunguzwa kwenye chungu cha kichawi akiwa mzima mzima hadi anaua majivu, kitu kingine wanachukuliwa vibinya mapumbu saba wa kwenye mgodo, vibinya mapumbu ni wadudu mijusi aina ya gomamli ambao huishi kwenye miti tu.
Sasa katika zoezi hili huwa wanachukuliwa gomamli wanao patikana kwenye mti wa porini unaoitwa mgodo. Kitu kingine kinacho ongezwa hapo ni mpanzi bukta kumi na tatu. Hawa mpanzi bukta ni aina ya panzi wanaoishi porini.
Vitu vyote hivyo vinasagwa pamoja kisha vinachanganywa na dawa inaitwa kishinda wachawi na mfalme wa pori halafu mhusika anaenda kuvichoma njia panda pamoja na fusho moja chafu .
Fusho hili ni miongoni mwa mafusho machafu kabisa na hufanana na lami nyeusi.
Wakati uchawi huu unachomwa mchomaji ana hakikisha moshi haueleke upande wake.
Ulozi huu unachomwa kwa manuizi maalumu ya kumnuia mkusudiwa kwanza ahame katika eneo alilokusudiwa kuhama lakini pili awe ni mtu wa kuhamahama na kutanga tanga katika kila sehemu atakayo kwenda katika siku zote za maisha yake.
Uchawi huu huwa unafanya kazi kwa haraka sana na kinga yake ni ima uwe na zindiko kali, au uwe mcha Mungu.
Ile miti iliyo tumika kutengenezwa mtumbi, zinachukuliwa dawa zile zilizounguzwa pamoja na jina, nguo, au picha ya mkusudiwa na karatasi iliyo andikwa maneno maalumu ya kilozi, kisha mtumbw huo unaenda kuwekwa kwenye mtu unao tembea kwa manuizi maalumu ya kumhamisha mhusika na kumfanya atange tange katika maisha yake yote.
Basi unaambiwa mtu aiyefanyiwa uchawi huu huwa haichukui muda ataondoka sehemu aiyo fukuzwa kichawi na kuiona kama jehanamu na anaanza kuwa mtu wa kuhamahama na kutanga tanga.
Ama kwa upande wa uchawi wa kumfilisi mtu, huwa upo uchawi wa aina nyingi sana, kuanzia uchawi wa kumlisha mtu kumtegea njia panda, kuzika uchawi mtoni kadhalika.
Lakini katika kitabu hiki nitaelezea kuhusu aina ya uchawi ulio tumika kumuumiza Lugwisha pamoja na namna ya kujikinga nao.
Uchawi ulio tumika kumuumiza Lugwisha ni uchawi wa kwanza kumtia nuksi, mikosi na mabalaa na pili ni kumfilisi, kumfilisi ikiwa ni mojawapo kati ya matokeo ya mabalaa.
Ni uchawi hatari sana na umeumiza watu wengi sana. Kabla ya kupiga kombora la kumfilisi mkusudiwa. Huwa linaanza kwanza zoezi la kumtia uchizi.
Katika zoezi la kumtia uchizi huwa vinakusanywa vizimba mbalimbali vya hatari. Baadhi ya vizimba hivyo ni pamoja na uchafu wa binadamu. Hapa kwenye uchafu wa binadamu ngoja nifafanue kidogo.
Katika viumbe wote wa Mwenyezi Mungu, hakuna kiumbe mwenye harufu mbaya kama binadamu.
Mbwa anaweza kukaa mwezi mmoja bila kuoga laini harufu yake haiwezi kufanana na binadamu alie kaa wiki moja bila kuoga. Binadamu anapiga mswaki kila siku lakini akikaa masaa kumi bila kuongea kinywa chake kinakuwa kinatoa harufu mbaya.
Linganisha harufu ya maiti ya mwanadamu na mzoga wa mnyama yoyote yule unae mfahamu.
Harufu ya mzoga wa mwanadamu ni kali kuliko kiumbe yoyote ile. Mfano mzuri, unaweza kukaa kwenye eneo ambao kuna mzoga wa mbwa, paka , kuku nakadhalika hata kwa siku mbili au tatu lakini huwezi kukaa mahali kwenye mwili wa mwanadamu ulio fariki na kuachwa kwa siku moja tu.
Hata katika roho , mwanadamu ndio kiumbe mwenye roho mbaya kuliko mnyama yoyote yule.
Simba hawezi kula simba mwenzake lakini binadamu wanakulana wao kwa wao.
Ndio maana wanasema hata silaha kubwa kubwa kama vile mabomu na bunduki vimewekwa kwa ajili ya kumdhibiti mwanadamu na sio wanyama.
Sasa basi wachawi hutumia uchafu wa mwanadamu kama moja wapo kati ya viambato vikolezo katika kutengeneza ulozi wa kuwatia watu nuksi, mikosi na mabalaa.
Uchafu wa mwanadamu huweza kutumika katika ulozi kwa namna nyingi sana. Mfano mchawi mwenye pepo la uchawi linalo tenda kazi, anaweza kulala saa moja usiku na kuamka sea kumi na moja alfajiri mdomo wake ukiwa unanuka halafu akaroga biashara ya mtu , kuvunja ndoa ya mtu au kumtia mtu mkosi kwa kutumia harufu ya mdomo wae kama kizimba pamoja na mti mmoja wa kichawi.
Tukirudi katika uchawi ulio tumika kumuumiza LUGWISHA. Hutafutwa watu arobaini wenye shida, nuksi na mabalaa ya kutisha ambayo ni tofauti tofauti. Watu hawa hupatikana kwa msaada wa wakonikoni.
Watu hawa hupiga kambi maalumu ya kichawi kwa muda wa siku arobaini bila kuoga. Siku ya arobaini ndio linaanza kufanyika zoezi la kupika uchawi huu.
Watu hao wake kwa waume watajipaka dawa fulani ya kichawi halafu wataanza kukwangua uchafu wao kutoka kwenye sehemu mbalimbali za miili yao huku yakitamkwa maneno maalumu ya kichawi. Kila mmoja wao atapulizia pumzi yake kwenye kitambaa cheusi ambacho kitafungwa baada ya hapo na atafanya hivyo huku aitamka maneno maalumu ya kichawi.
Kumbuka hawa watu hupatikana kwa msaada wa wakonikoni. Watu hawa wanakuwa wameenda kwa wakoni koni kwa ajili ya kutolewa mabalaa, nuksi na mikosi mbalimbali.
Kwa wakoni koni nuksi na mabalaa ya watu ni bidhaa adimu. Badala ya kuitoa wao huvichukua kwa ajili ya kutengeneza uchawi wa kuwaumiza watu.
Siku hiyo yakwenda kutoa hizo nuksi, kila mmoja kati ya watu hao wenye nuksi hutamka maneno maalumu wakati anatoa uchafu kwenye sehemu mbaimbali zap mwli wake kama vile kwenye masikio, mdomoni, kwapani, sehemu zap siri nakadhalika.
Kwa mfano, mimi fulani Bin Fulani ambae ninasumbuliwa na magonjwa kadha wa kadha, ninasumbuliwa na matatizo kadha wa kadha, ninayatoa magonjwa yangu yote, nuksi zangu zote pamoja na matatizo yangu yote na kuyahamishia kwa fulani bin fulani nakadhalika.
Uchafu wote huu utausanywa pamoja na kuhifadhiwa kwenye chombo maalumu. Zile harufu zitatumika wakati wa kupika hii nuksi katika hatua ya mwisho kabisa.
Baada ya hapo vitachukuliwa vitu vingine kama vile mavi ya sokwe, mavi ya nyani, mavi ya ngedere, mavi ya bundi, mavi ya ndege wa porini ajulikanae kama mpambe wa bundi, mavi ya ndege wa porini anaitwa Mkatasanda “ Ndege huyu mkatasanda akilia kwenye nyumba yenu lazima msiba mkubwa utokee”, uchafu kutoka kwenye majalala arobaini, uchafu kutoka kwenye misiba arobaini, vizimba vya wanunguli , mafusho sea machafu pamoja na miti mingine kumi na tatu ya porini.
Vitu vyote hivi vinasagwa pamoja na kwenda kunuizwa makaburini. Wakati wa manuizo wale watu arobaini wanakuwa wanalia na kuimba nyimbo za kichawi na maombolezo huku waitaja jina la mkusudiwa kana kwamba amefariki dunia.
Baada ya zoezi la kumtumia nuksi, balaa na mikosi mkusudiwa, zoezi linao fuata huwa ni kufanya tambiko au uchawi wa kumfilisi mkusudiwa.
Katika tambiko hili wachawi huchukua mzizi wa mbono kaburi, mzizi wa mti unaitwa mshindwi , mzizi wa mtopetope , mzizi wa mfausiku, mzizi wa mgodo, pamoja na mizizi ya miti mingine 33. Mizizi yote hiyo niliyo itaja hapo juu husagwa kwa pamoja na kuhifadhiwa kwenye kitambaa cheusi.
Baada ya hapo unachukuliwa mzizi au mizizi iliyo okotwa wakati kaburi linachimbwa. Mzizi huu wakati unachukuliwa huwa hauchukuliwi na mhusika mwenyewe bali hutuma mtu akauchukue.. Huu ni uchawi mkubwa sana na unatumika kwenye mambo mengi sana ya kichawi,. Ni hatari sana. Narudia tena ni uchawi sana.
Huo mzizi ulio chukuliwa wakati kaburi linachimbwa, unapaluliwa vizuri kwa tambiko maalumu la kichawi, wakati mzizi huu unapaluliwa mpaluaji anakuwa amejipaka dawa maalumu na anakuwa amevaa vazi maalumu.
Mzizi huu ukishapaluliwa unawekwa kwenye chungu cheusi.
Halafu anatafutwa ogoo mwekundu au mweusi . Huyu jogoo mweusi au mwekundu analishwa dawa maalumu ya kichawi na kwenda kufungwa porini chini ya mti wa mgodo kwa muda wa siku saba. Atauwa anapelekewa mchele kila siku kwa muda siku hizo saba.
Baada ya siku saba mchawi atamchukua yule jogoo na kulala nae ndani. Mahali atakapo kuwa amelala huyo mchawi lazima pembeni yake kuwe na kile chungu cheusi chenye ile mizizi ya kaburini iliyo paluliwa na kusagwa kisha kuwekwa ndani yake.
Ikifika alfajiri, jogoo akiwika mara moja , anakamatwa na kuchinjwa kisha damu yake inawekwa kwenye kile chungu cheusi chenye ile dawa ya kichawi.
Mchawi huyu anakuwa makini mno kuhakikisha kuwa jogoo hawiki zaidi ya mara moja. Yaani jogoo akiwika mara moja tu,anakamatwa hapohapo na kuchinjwa na kisha damu yake inamiminwa kwenye hicho chungu chenye huo uchawi. Hapa sasa damu ya kuku inakuwa imechanganyikana na hii dawa.
Zoezi hili likikamilika, yule jogoo anaachwa sakafuni pale pale alipo chinjwa na ile damu yake ambacho imechanganywa na ile dawa inaachwa kwenye chungu kisha mchawi huyu anaenda kulala na kuamka jua litakapo chomoza.
Akisha amka anaenda kukausha dawa ile pamoja na damu kisha anaisaga hadi inakuwa unga unga. Ukisha patikana unga unga wa dawa hii unahifadhiwa kwenye chungu cheusi.
Ndani ya chungu hicho cheusi vinaongezwa vitu vifuatavyo ; sindano saba, viwembe saba ambavyo vyote vinakatwa, mafuta ya maiti vichupa saba ( mafuta haya hutumika kuwapaka maiti, karafuu maiti ya kidonge vidonge saba, mafuta ya usiku kiasi cha kifuniko kimoja cha soda, kishinda wachawi kijiko kimoja, mti mkuu kijiko kimoja, mfalme wa porini kijiko kimoja, unga wa mdudu kusahau kijiko kimoja, Huyu mdudu kusahau hupatikana porini na nyikani. Sifa yake ni kwamba, ukimkanyaga utapotea mahali unapokwenda. Ana majini wakali sana wa usahaulifu.
Vitu vingine vinavyo chukuliwa ni pamoja na magunzi ya maindi yaliyo liwa na nyani shambani, mabai ya mazao na mchanga wa kwenye shamba lililo liwa na nyani, mabaki ya mazao mchanga wa kwenye shamba la mihogo lililo vamiwa na kuliwa na nguruwe mwitu , nzige walio kaushwa na kusagwa, mabaki ya mazao au mimea iliyo shambuliwa na kuliwa na nzige, ubao au vitu vilivyo toka kwenye mafuriko pamoja na vizimba vingine vingi.
Vyote hivi vinasagwa kwa pamoja na kuchanganywa kwenye chungu cheusi.
Baada ya zoezi hili , mchawi anachukua zile dawa alizo saga pamoja mara ya kwanza ambazo ni mizizi ya mbono kaburi, mfausiku, mshindwi,mtopetope na miti mingine 33 ya kichawi,na kuzichangaya kwenye hicho chungu ambacho uchawi huo hapo juu umewekwa.
Baada ya hapo chungu hicho kinafungwa kwa kitambaa cheusi juu na kwenye shingo.
Zoezi hili hufanyika kwa kufuata hatua zote bila kuruka au kusahau hata hatua moja.
Baada ya zoezi hili kukamilika mchawi huyu pamoja na timu yake, watavaa kaniki nyeusi na kujipaka unga wa mti maalumu wa kichawi, bila kuvaa nguo yoyote ndani, watasubiri hadi saa sita za usiku na kwenda hadi kwenye makaburi yaliyo sahaulika.
Ninaposema makaburi yaliyo sahaulika nazungumzia makaburi ambayo marehemu walizikwa zaidi ya miaka 20, 30 hadi 50 au hata mia iliyopita, ambayo ndugu zao wameisha ya sahau au na wao walisha kufa zamani,.
Ipo njia ya kiganga na kichawi ambayo inatumika kujua kama kaburi fulani limesahaulika au la.
Wanapokwenda kwenye makaburi haya ni lazima wawe bila viatu na kama makaburi yapo kwenye maeneo yenye miba mingi basi watavaa viatu vya asili kama vile katambuga, na pia lazima wapitie kwanza njia panda kufanya tambiko maalumu.
Wakifika kwenye makaburi hayo huanza kwa kupiga hodi mara saba huku wanajiitikia wenyewe. Husema “ HODI!” na kujiitikia wenyewe “ KARIBU! “. Watafanya hivyo hadi mara saba . Baada ya kufanya hivyo mara saba , wataanza kusema maneno yafuatayo :
“ WAZEE NIMEKUJA NINA NGORANI YANGU. WAZEE NIMEKUJA MIMI FULANI BIN FULANI, SHIDA YANGU NI FULANI BIN FULANI. NATAKA MTU HUYU AFILISIKE NA ASHUKE HADI CHINI AWE KAMA MIMI AU SISI KAMA WAPO WENGI AU AWE CHINI YETU KABISA!
FULANI BIN FULAN AMEPATA PESA AMEPATA MALI, AMESOMA SANA, NA SASA ANATUDHARAU KWA KUWA AMESOMA SANA! ANATUONA SISI HATUNA MAANA !
PESA ZAKE , ELIMU YAKE, MALI ZAKE NDIO ZINAMTIA JEURI NA KIBURI NA KUMFANYA ATUDHARAU. TUNAOMBA MUENDE MKAMFILISI NA KUMSHUSHA CHINI HADI AWE KAMA SISI.
NINYI MIZIMU WA HAPA. NINYI WAFU MLIOLALA HAPA. WAZEE KWA VIJANA, WAKE KWA WAUME. SIKUWA NAWAJUA WAKATI WA UHAI, WENU ILA NIMEKUJA KUWAAMSHA NA KUWATUMA KWA FULANI BIN FULANI, NENDENI MKAMFILISI NA KUMSHUSHA CHINI KABISA HADI AFANANE NA MIMI AU ASHUKE KABISA AWE CHINI YANGU.
MAMBO YAKE YOTE YAHARIBIKE., MALI ZAKE, PESA ZAKE, NA KILA KITU CHAKE. VYOTE VIFE KAMA JINSI NINYI MLIVYO KUFA NA KUJA KU LALA MAHALI HAPA. KAMA N I MASHAMBA YAFE. BIASHARA ZOTE ZIFE..N.K
AUZE KILA KITU CHAKE NA PESA ATAKAZO ZIPATA ZITUMIKE KUMUANGAMIZA YEYE MWENYEWE. AKINUNUA CHAKULA NA KINYWAJI VIMLETEE KISUKARI NA PRESHA, AKINUNUA GARI LIMLETEE AJALI NA KUMSABABISHIA ULEMAVU WA KUDUMU, AKINUNUA NGONO BASI IMLETEE UKIMWI. AUGUE KILA AINA YA MARADHI. ADHALILIKE. AFEDHEHEKE..NAKADHALIKA.
Wakati huyu mtu anazungumza maneno haya, mkonikoni au mchawi anakuwa anafanya tambiko maalumu kwenye makaburi hayo huku akipuliza na kutupa dawa maalumu za kichawi kwenye makaburi hayo.
Na kama hawa washirikina walioenda kumroga ndugu, jamaa au rafiki yao wapo zaidi ya mmoja, basi kila mmoja atatamka maneno yake.
Wakimaliza mmoja wao anachukua kile chungu na kukiweka sehemu ya kifua kwenye kaburi lolote ambalo atalichagua lililopo katika eneo hilo. Na huwa ni mwiko kuzika chungu hiki cha kichawi. Huwa kinawekwa tu juu juu.
Sasa basi mtu huyu anapokuwa anaweka hungu hiki, hutamka maneno yafuatayo :
“ NA KAFARA YENU NDIO HII HAPA NIMEWAPA ! HII NDIO NGORANI YANGU! AMKENI MKATENDE KAZI YENU ! HII NI VITA ! HAYA NI MAPAMBANO! UENI KILA KITU CHAKE CHOTE, ABAKI KAMA ALIVYO ZALIWA !
Skadi hili huwa linaondoka hapo hapo na huanza kufanya kazi siku hiyo hiyo.
Ni uchawi mkubwa na wa hatari sana. Usiombee utupiwe skadi kama hili.
Watu walio tupiwa skadi hili wote walipata matatizo katika maisha yao. Pona pona yako ni kama una kinga kubwa au ni mtu wa maomba au swala yaani mtu wa ibada, vinginevyo ndugu yangu.Utadhalilika na kufedheheka katika maisha yako.
Mtu aliye tupiwa skadi hili kwanza huwa anapewa dawa ya kutapika au kuharisha uchawi aio tupiwa , baada ya hapo anasafishwa mwili, anapikwa na kisha anapandishwa nyota yake na kutambikiwa upya. Aanze maisha yake upya. Kama kuna mali alizo dhulumiwa basi zitaanza kurejeshwa moja baada ya nyingine.
Tambiko la kumrejesha muhanga wa uchawi huu katika hali yake ya kawaida huwa lina hatua ndefu sana. Si rahisi kuzielezea zote hapa. Hila kwa ufupi tambiko hili hufanywa na mganga chini ya mti mmoja wa porini ambao haukaliwi na kitu chochote kichafu au kibaya kiwe jinni au awe mdudu mbaya kama vile nyoka nakadhalika.
Mambo yanayo fanyika katika tambiko hilo ni pamoja na kupiga hodi kwenye mti huo kwa tambiko maalumu linalo husisha kuku weupe, kondoo, punda na pemba nyeupe.
Kufanya tambiko maalumu la kumrudisha upya duniani kwa kutumia mayai ya kuku . Tambiko hilo ni kubwa sana na lina nguvu sana.
Kwa ufupi tambiko la kubatilisha uchawi huu na kumrudisha mhusika katika hali yake ya kawaida linahusisha vizimba vingi sana. Vichache kati ya vizimba hivyo ni pamoja na maji ya kwenye chemu chemu ya mlima mrefu, maji ya kwanza ya mtoni, Asali ya nimba, Nimba ni mnyama wa porini anaefanana kama nyumbu, mnyama huyu huwa anatembea na mzinga wa nyuki kichwani. Ni mnnyama mwenye maajabu sana na haonekani ovyo ovyo pia ana sifa ya kupotea. Sasa asali ya mnyama huyu ndio inayo tumika hapa.
Vitu vingine ni pamoja na miko iliyo tumika katika maeneo mbalimbali yenye mkusanyiko mkubwa wa watu kama vile gerezani nakadhalika, mzizi ulio kata njia, mti ulio ungua ukulunoni, maji ya mchele, marashi ya waridi, mafuta ya mcheka na mbingu, maji makuu, mti mkuu, kishinda wachawi, mfalme wa pori, mzungu pori, Mkurungu, mkubashengelo, picha yako ya utotoni, kibiringisha mavi; hawa vibiringisha mavi hupatikana sana sana kwenye mavi ya ng’ombe na siku zote hujongea kinyume nyume , msuswe aliye gongwa na gari akiwa anakatisha njia; msuswe ni aina ya panya ambao hutoa sauti inayo fanana na jina lao.
Kitu kingine unachukua mzizi ulio jitokeza nje ambao majani na matunda yake huliwa na ndege mmoja wa porini. Huyu ndege wa porini ana sifa moja kubwa, wachawi wanapenda sana kumtumia kwenye shughuli zao. Ukichukua nyoya lake, ukaweka kwenye mto wa kitanda ambacho analalia mgonjwa basi mgon jwa huyo atafariki dunia. Kuweni makini sana na mito mnampokuwa na wagonjwa iwe ni hospitalini au majumbani.
Pamoja na vizimba vingine vingi.
Vitu vyote hivyo vinatumika katika kutengeneza tambiko la kubatilisha uchawi wa aina hii pamoja na kumrejesha muhanga katika hali yake ya awali.
Hatua ya mwisho ya tambiko hili, mganga humchukua mgonjwa na kumtamkia maneno mbalimbali. Baadhi ya maneno hayo ni pamoja na :
“ KUANZIA LEO NIMEKUTOA CHINI WALIKOKUWA WAMEKUWEKA WACHAWI, MAJINI, MASHEITWANI NA WATU WABAYA. NAKUWEKA JUU NA UTABAKI KUWA JUU KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO
iIi kuepukana na kutupiwa na uchawi wa aina hii au uchawi wa aina yoyote ile, unatakiwa uwe Mcha Mungu na kama sio Mchanga Mungu basi ni lazima uwe na kinga kubwa. Baadhi ya kinga hizo ni kama nilivyo zielezea katika sehemu zap mwanzo zap kitabu hiki.