Skip to main content

Baraza La Madiwani Manispaa Ya Ubungo Laagiza Idara Ya Mipangomiji Kufuatilia Na Kutwaa Maeneo Ya Umma

Baraza La Madiwani Manispaa Ya Ubungo Laagiza Idara Ya Mipangomiji Kufuatilia Na Kutwaa Maeneo Ya Umma


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakiwa kwenye Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam

Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo kwa kauli moja limeridhia na kuagiza Idara ya Mipangomiji na Mazingira kufuatilia na kutwaa maeneo kwa ajili ya matumizi ya Umma hususani maeneo ya Shule.

Aidha Baraza la madiwani limeagiza Idara hiyo ya Mipango Miji kutembelea na kupima eneo la shule ya Sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba ambalo eneo lake limesalia ekari 31 kati ya 22 huku eneo jingine likitumiwa na wananchi kinyume na utaratibu.

Pia imebainika kuwa hali ya ukusanyaji mapato inaendelea kukua kutokana na juhudi na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato tangu kuanza kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo baada ya mgawanyo wa Halmashauri hiyo kutoka Manispaa Mama ya kinondoni.

Akijibu swali lililoulizwa kuhusu ubovu wa mashine za kukusanyia mapato POS Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa hajawahi kupokea malalamiko juu ya mashine hizo na kubainisha kuwa Manispaa imepata mtaalamu anayeshughulikia mashine hizo ambapo atatoa taarifa juu ya kiasi kilichokusanywa tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo za POS.

Akiongelea kuhusu semina kwa madiwani MD Kayombo alikiri kuwa kuna umuhimu wa madiwani kupata semina hususani kwenye eneo la kanuni na sheria mbalimbali na pia katika sheria za manunuzi hivyo ameahidi kuandaa semina hiyo ili waweze kuelimika zaidi.

MD Kayombo akizungumzia suala la maendeleo ya jumla katika kuboresha miundo mbinu katika shule za Manispaa ya Ubungo alisema kuwa zitakuwa zikifanyika hatua kwa hatua katika kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa huku akibainisha kuwa katika kuinua elimu katika Shule za Manispaa ya Ubungo ujenzi wa Madarasa, Vyoo sambamba na Ukuta vitaanza kujengwa hivi karibuni katika shule ya Msingi Ubungo Plaza.

Popular posts from this blog

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime

Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara akemea uwindaji haramu Tarime MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mkuu wa Majeshi mstaafu (CDF), Jenerali George Waitara, amewataka wanachi wilayani Tarime, kuachana na uwindaji haramu, badala yake watumie fursa zilizopo kukuza vipato vyao iii kuondokana na umasikini katika ngazi ya familia.  Pia, amewataka wananchi hao watumie fursa hizo kuwekeza katika miradi na biashara mbalimbali katika maeneo jirani na Hifadhi ya Mbuga ya Serengeti, itakayowawezesha kuwaingizia vipato.  Waitara alitoa wito huo mjini Tarime, juzi, alipokutana na baadhi ya wananchi na kubadilishana nao mawazo, wakati akielekea nyumbani kwake k ij iji cha  Itiry o   kusherekea sikukuu ya Pasaka.  Alitoa ushauri kwa watu wenye nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji mali wilayani humo, watumie nafasi hiyo iii kukuza na kuendeleza mji waTarime na wilaya hiyo kwa ...

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4

Ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge Linaloanza Leo Jumanne April 4 Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt Philip Mpango anatarajiwa kusoma Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 siku ya Alhamisi, Juni 15 mwaka huu. Tarehe hiyo ni kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Saba wa Bunge unaoanza leo  Jumanne (Aprili 4) katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, mkutano ambao ni maalum kwa ajili ya bajeti. Ratiba hiyo inaonesha shughuli ya kwanza kuwa ni uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki siku ya Jumanne, na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu itasomwa siku ya Alhamisi, Aprili 6 na kujadiliwa kwa siku nne, ikifuatiwa na bajeti ya Rais (siku 4) na Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Siku 1) kabla ya bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba Aprili 25. Mbali na bajeti za wizara, mkutano huo pia utajadili na kupitisha miswada kadhaa ya sheria ukiwemo Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka, 2017 ==>Itazame hapa ratiba kamili ya mkutano huu...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...