Skip to main content

Watano wakamatwa kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya

Watano wakamatwa kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watano kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kilo mia moja, mirungi kilo sitini, heroine kete tatu na vifungashio vya dawa hizo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, ikiwa ni jitihada za kuendeleza vita dhidi ya matumizi na uuzaji wa dawa hizo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro ikiwemo wilaya za Mvomero, Morogoro manispaa na Kilombero,wakiwemo watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha dawa hizo  kwa magari ya abiria, basi la BM Coach huko Mkindo Turiani, na gari ndogo aina ya Hiace maeneo ya Kihonda, pamoja na pikipiki maarufu kama boda boda.

Baadhi ya watuhumiwa waliohojiwa kuhusiana na dawa hizo, wamekuwa na majibu tofauti, wengi wakidai kutumwa na watu mizigo hiyo ikiwemo mirungi na bangi, ambapo aliyekuwa amebeba debe nne za bangi kwa kuficha ndizi mbichi juu ya kiroba kilichokuwa na mzigo huo akidai alitumwa na mtu bila kujua mzigo huo kama ni bangi, ambapo polisi wameomba ushirikiano zaidi kuwabaini na kufichua matukio ya dawa za kulevya na watuhumiwa wake.

Popular posts from this blog

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU” kama  ifuatavyo : SEHEMU  YA  PILI   YA  KITABU  “ KITANDA  CHA  SOKWE  MTU “ Wachawi   wakishindwa  kukutengenezea  kesi  kubwa  basi  waatakufunga  kwenye  kifungo  cha  mapenzi.  Katika  vifungo  vyote anavyo  fungwa  mwanadamu  hakuna  kifungo  kibaya  kama  kifungo  cha  mape

Faida nyingine za kula chungwa

Faida nyingine za kula chungwa Siku kadhaa zilizopita tuliangalia kwa uchache kuhusu faida za kula chungwa hivyo, pia siku ya leo naomba tuendelee kwa kuangalia faida nyingine za kula chungwa. 1. Ulaji wa machungwa husaidia kutibu mapafu. Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu. 2. Husaidia kuimarisha mifupa ya meno. Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno. 3. Husaidia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini. Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake. 4. Hupunguza kupatwa magonjwa wa figo. Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaid

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi?

Je, unajua Binadamu anatakiwa kulala masaa mangapi? Unafikili ni wazo zuri kuamka  saa 11 za asubuhi na kufanya mazoezi? Je, ingekuwa vipi kama ungetumia muda huo kulala? Wataalamu wa afya wanashauri kuwa binadamu kwa kwaida anapaswa kulala angalau masaa 7 wakati wa usiku ili kuupa mwili afya bora. Kulala kwa muda mfupi au masaa machache husababisha matatizo ya afya, ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, unyogovu, ugonjwa wa kisukari, na kupunguzwa kinga kukabiliana na chanjo. Ni vyema ukatumia muda wako vizuri mchana ili usiku ukapata muda mwafaka wa kuweza kuupumzisha mwili ili kuepukana na magonjwa hatari ya shinikizo la damu, kisukari na kupungua kwa kinga mwilini. Najua mazingira yetu waafrika ya kimaisha wakati mwingine yanachangamoto nyingi, lakini pale upatapo mwanya kidogo tu, basi utumie yani "kila penye tundu, penyeza lupia" au wawenzetu wazungu wanasema "one chance two goals".