Taarifa
ya TFDA kuhusu dawa P-500® Paracetamol kuingia Tanzania


Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo imeeleza kuwa Dawa hiyo inayotengenezwa na kampuni ya Apex Laboratories Private Limited-Tamil Nadu ya India haijasajiliwa nchini na haipo kwenye soko la Tanzania.
Aidha Mamlaka imewataka Wananchi kutoendelea kusambaza taarifa za uvumi ambazo zina lengo la kuwaogopesha na kuzua taharuki kwa wananchi kabla ya kupata ufafanuzi kutoka mamlaka husika.