Skip to main content

Charles Hillary Ateuliwa Kamati Ya Kuhamasisha Serengeti Boys

Charles Hillary Ateuliwa Kamati Ya Kuhamasisha Serengeti Boys

MWANDISHI nguli wa habari na mtangazaji nyota wa kimataifa, Charles Hillary ameteuliwa kuongoza Kamati ya watu 10 watakaohamasisha kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia timu ya vijana chini ya umri wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys.

Uteuzi huo umetangazwa leo na Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye mbele ya wanafamilia ya mpira wa miguu waliohudhuria kongamano ya kujadili juu ya ushiriki wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mada ilikuwa ni Tanzania kushiriki michuano ya Olimpiki Tanzania, lakini kwa kuwa kuna jambo la usoni la timu ya Serengeti Boys kucheza fainali za Kombe la Dunia huko Gabon kuanzia Mei 21, mwaka huu, Waziri Nape atakatangaza kamati ya kuhamamsisha ili Watanzania kwa pamoja waweze kuchangia.

Akitangaza kamati hiyo, Nape alisema kwamba Katibu wa Kamati hiyo atakuwa Mwesigwa Selestine ambaye ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Mtangazaji wa Radio ya EFM, Maulidi Kitenge; Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu.

Pia wamo Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas; Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo; bosi wa radio Clous, Ruge Mutahaba pamoja wa wasanii wa kizazi kipya Diamond Platnums na Ally ‘King’ Kiba.

Pamoja na hayo, katika kongamano hilo na wadau wa soka wadau ikiwamo Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.

Wameazimia kuwa na chanzo cha fedha cha kueleweka ili kufanikisha program mbalimbali za timu za taifa ikiwamo ya U23 ambayo inatakiwa kushiriki kwenye michuano ya Olimpiki. Serikali imepanga kuwa pamoja badala ya kile kinachoitwa kudandia matokeo mafanikio bila kushiriki maandalizi.

Kadhalika wameazimia mpira kuwa jambo la nchi ili hamasa inayotangazwa iguse wadau wote kwa maana ya Watanzania wote.

Pia chanzo cha kupata vipaji kiwe pia kutoka mashuleni (Umitashumta na Umiseta) ambako Mheshimiwa Waziri Nape mbali ya kuthibitisha kuwa mwaka huu itafanyika tofauti na mwaka jana, pia aliagiza kuwa isiwe kama matamasha.

Popular posts from this blog

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent

Lema ahoji kushikiliwa mmiliki wa shule ya Lucky Vincent Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema   Dodoma. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35. Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda. Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo. Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali.

Jinsi Wachawi Wanavyo Tumia Mafiga Mabichi Ya Mti Wa Mfausiku Kupika Uchawi Wa Kumvuta Kimapenzi Mtu Aliye Mbali. Na. DOKTA  MUNGWA  KABILI …0744 -000  473.  Wachawi  wanaweza  kutumia  uchawi  kumvuta  kimapenzi  mtu  aliye  mbali. Moja  kati  ya  vitu  vinavyo  tumika  katika  uchawi  huu  ni  pamoja  na  mafiga  mabichi  ya  mti  wa  mfausiku  ambayo  hukokwa  kwenye  majani  makavu ya  mgomba  ambayo  hutumika  kama  kuni  au  moto,  kipande  cha  sanda  alichovalishwa  maiti, herufi za  moto,  mti wa hina, pamoja na  vitu  vingine  lukuki. Kufahamu  kuhusu  uchawi wa aina  hii  na  jinsi  ya  kujikinga  nao, fuatilia  sehemu  ya  nne  ya  kitabu “ ...

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC

SADC YALIPONGEZA BARAZA LA USALAMA LA UN KWA KUONGEZA MUDA KWA MISHENI YA ULINZI DRC 1 2 3 4 5 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika New York, Marekani na kupitisha Azimio la kuongeza muda kwa vikosi vya usalama vilivyopo DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Mahiga (hayupo pichani). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb). akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa...