Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2017

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani

Mamlaka ya hali ya hewa yatoa tahadhari kwa wakazi wa ukanda wa pwani Mamlaka ya hali ya hewa imetoa tahadhari  kubwa kwa wakazi wa ukanda wa pwani kuwa kutakuwepo na upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya bahari ya Hindi. Aidha, katika Maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na hali hiyo ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo, imesema kuwa kunatarjiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2 baharini hivyo watumiaji wote wa bahari wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa. Hata hivyo, hali hiyo inasababishwa na msukumo wa upepo wa kusi unaotokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda pwani hivyo kusababisha hali hiyo kutkea.

Wenger aongezwa mkataba wa miaka 2 Arsenal

Wenger aongezwa mkataba wa miaka 2 Arsenal Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekubali kuchukua mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo, hatua itakayoendeleza muda ambao amekaa katika klabu hiyo. Mfaransa huyo amekuwa meneja wa Arsenal kwa miaka 21 sasa. Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke walikutana Jumatatu kuamua hatima ya meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa kwa mkutano wa bodi Jumanne. Arsenal wanapanga kutangaza rasmi uamuzi huo Jumatano. Gunners walimaliza Ligi ya Premia wakwia nafasi ya tano, mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nafasi ya nne tangu Wenger alipojiunga nao mwaka 1996. Walimaliza alama 18 nyuma ya mabingwa Chelsea, lakini walifanikiwa kuwachapa Blues katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley Jumamosi. Mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya Premia na pia vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza kwenye usukani. Mwaka 2003-04, aliibuk...

Walemavu walioungana wampata kijana wa kuwaoa

Walemavu walioungana wampata kijana wa kuwaoa Kwa yeyote aliyewahi kukutana nao, mapacha wawili ambao ni walemavu walioungana matumbo, Maria na Konsolata hatabisha kwamba pamoja na hali yao, watoto hao ni wacheshi, wakarimu na wanaoweza kukufanya utabasamu hata kama moyoni mwako, ulikuwa na huzuni Wiki hii walifanyiwa mahojiano na Gazeti la Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha yao pamoja na ishu yao ya kufikiria kuolewa.     Si rahisi kufikiria maisha ya ndoa ya Maria na Consolata kwa jinsi walivyo, lakini pacha hawa walioungana wako wazi kuhusu matamanio yao ya maisha ya ndoa.     Katika mazungumzo yao na gazeti hili, Maria na Consolata waliweka bayana mipango yao ya ndoa mara watakapomaliza elimu ya chuo kikuu.     Ingawa ni kitu cha kushangaza, Maria na Consolata hawatakuwa mapacha wa kwanza katika maisha ya ndoa. Chang na Eng Bunker ni pacha wanaume waliozaliwa mwaka 1811 nchini Thailand ambako zamani kuliitwa ...

Kairuki: Serikali Haitaajiri Walimu wa Masomo ya Sanaa

Kairuki: Serikali Haitaajiri Walimu wa Masomo ya Sanaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari. Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao "Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalim...

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kupunguza tumbo, Kuongeza nguvu za Kiume na Mvi

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kupunguza tumbo, Kuongeza nguvu za Kiume na Mvi (OFFER OFFER OFFER) NATURAL BEAUTY COSMETIC INAKUPATIA OFA YA PUNGUZO LA BEI KWA KILA BIDHAA PUNGUZO LA  %10 KWA MWEZI HUU WA RAMADHANI.    PATA BIDHAA HIZI ZILIZOTENGENEZWA KWA MIMEA NA MATUNDA UFURAHIE MATOKEO MAZURI BILA KEMIKALI WALA MADHARA YOYOTE PIA NI GUARANTEE. Bidhaa tulizonazo÷   πŸ‰πŸ“πŸ‡πŸ…πŸŠπŸ’πŸπŸŒ΄πŸπŸ§€πŸ§€πŸ§€πŸ§€πŸ…πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸπŸπŸŒ³πŸπŸπŸŒΆπŸ‰πŸ†πŸ†πŸ’. Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi. 1. YODI PILLS _ Ni vidonge vya kuongeza hips na makalio @170,000/= 2. BOTCHO CREAM_ Ni dawa ya kupaka ya kuongeza shepu (hips na makalio) @150,000/= 3. BOTCHO MULT PLUS_ Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza shepu (hips makalio na mapaja) @200,000/= 4. PANNAMAS BREAST_ Ni dawa ya kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walio nyonyesha. Inapatikana kwa Tsh @120,000/= 5. DISCREET_Hii ni kwa ajili ya kuondoa mvi milele na zisiludi tena. @120,000/= 6. BODY...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 30

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya May 30

Wanaosafiri kati ya Tanzania na DRC kupimwa Ebola, Waziri Ummy aeleza hali ya ugonjwa huo nchini.

Wanaosafiri kati ya Tanzania na DRC kupimwa Ebola, Waziri Ummy aeleza hali ya ugonjwa huo nchini. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Ally Mwalimu amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa wa Ebola wala anayehisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo nchini Tanzania huku Tsh. bilion 1.5 zikiwa zimetumika kuukabili ugonjwa huo   Ummy amebainisha hayo leo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema wananchi wasiwe na hofu ila wanapaswa kuchukua tahadhari huku akisisitiza kuwa wameweka kifaa maalum 'register' ambacho kitawalazimu wasafiri wote kujaza wakiwa wanakwenda  katika nchi ya DRC na pindi wakiwa wanatoka huko kuingia nchini. "Hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa Ebola wala mwenye virusi Tanzania, tumechukua tahadhari katika mikoa yote inayopakana na nchi ya Congo DRC. Wasafiri wote wanaotoka DRC wakifika Tanzania lazima waandikishwe kimaalum ili kufuatiliwe kama huko alikotoka hali ikoje na kam...

Nape Awaponda Wabunge Wanaoisifia Serikali kwa Kila Kitu

Nape Awaponda Wabunge Wanaoisifia Serikali kwa Kila Kitu Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kusema wabunge wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaishauri na kuikosoa serikali ni watu ambao wana mapenzi mema na Rais na serikali yake kuliko wanao sifia kila kitu. Nape Nnauye amedai wabunge ambao kazi yao ni kusifia kila kitu hata kama kuna mapungufu hao hawana mapenzi ya kweli kwa Rais Magufuli na serikali kiujumla na kudai yeye anaitumia nafasi yake vizuri kutoa ushauri kwa serikali kupitia bunge sababu ndiyo njia sahihi aliyonayo kwa sasa. "Kimsingi kazi kubwa ya Mbunge hasa wabunge wa CCM ni kuishauri serikali yake sisi tunaoshauri tunampenda zaidi Rais na tunaipenda zaidi serikali ifanye vizuri kuliko wale ambao watakuja na kusifu na kupongeza kwa kila kitu, hata pale wanaona kabisa hapa tungeweza kushauri na mambo yakarekebishika"  alisema Nape Nnauye Mbali na hilo Nape Nnauye amedai kuwa watu ambao wanashangaa yeye kuishauri serikali sasa...

Diamond: Sitaki Tiffah awe msanii, naogopa ataliwa sana na Wanaume

Diamond: Sitaki Tiffah awe msanii, naogopa ataliwa sana na Wanaume Diamond Platnumz amefunguka kwa kudai kuwa hataki mtoto wake wa kike Tiffah awe msanii kwa madai akiwa msanii atatembea kimapenzi na wanaume wengi. Muimbaji huyo amedai mtoto wake huyo akiwa msanii, wanaume wengi watamiminika kumtaka kimapenzi. “Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana,”  alisema Diamond weekend iliyopita  akiwa katika kipindi KTN nchini Kenya.  “Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha,” Aliongeza,  “Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,” Muimbaji huyo Jumanne hii anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zazi, Ivan aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa ...